Virusi vya Corona: Wagonjwa 9 wapya wathibitishwa Kenya

rais Uhuru Kenyatta

Chanzo cha picha, Ikulu ya rais Kenya

Idadi ya waliombukizwa kenya na virisi vya corona imefikia 234 baada ya wagonjwa wengine tisa kutangazwa Alhamisi.

Akihutubia taifa rais Uhuru Kenyatta amesema kwamba watu 704 walipimwa katika kipindi cha saa

Aidha kiongozi huyo wa taifa alisema kwamba watu 53 wamepona huku idadi jumla ya walioambukizwa ikifikia 234.

Rais Kenyatta amethibitisha kwamba uwezo wa kupima virusi hivyo unaendelea kuimarika na kwamba upimaji wa watu wengi kwa wakati mmoja utaanza katika maeneo yaliyolengwa kwanza kabla ya kupelekwa hadi maeneo mengine.

Pia alitangaza Kwamba takriban watu 1000 walikuwa wamewekwa katika karantini huku wengine 156 wakiwa katika vituo vya kujitenga

Juhudi za kuwalinda Wakenya dhidi ya virusi vya corona kufikia sasa zimemfanya rais Uhuru Kenyatta kutoa agizo la amri ya kutotoka nje kuanzia mwendo wa saa moja usiku hadi saa kumi na moja alfajiri.

Wakenya waliopo katika kaunti za Nairobi, Mombasa Kilifi na Kwale pia wameagizwa kutotoka katika kaunti hizo mbali na kupiga marufuku kuingia na kutoka kwa ndege za kigeni.

Baadhi ya hatua zilizotangazwa na rais Uhuru Kenyatta.

1.Wizara ya Afya na huduma za umma itaanzisha hazina ya kuwasaidia wafanyakazi wa Afya wanaokabiliana na mlipuko wa virusi vya corona

2. Wizara ya elimu itachukua hatua kuwalinda wanafunzi kutokana na athari mbaya za hatua zilizochukuliwa kukabiliana na Covid-19

3. Mamlaka ya usambazaji wa tiba nchini Kenya itaondoa masharti ya ununuzi wa vifaa vya kujilinda dhidi ya Covid-19 kwa takriban miezi mitatu ili kurahisishia kaunti kununua vifaa hivyo.

4. Nyumba za watu wasiojiweza jijini Nairobi zitafaidi kutokana na fedha zilizotengwa na serikali kusaidia familia zisizojiweza

5.Bunge litapitisha tena mapendekezo na miswada kuhusu vichocheo vya uchumi.

6. Ili kuhakikisha msaada unagawanywa kwa njia salama, mfuko wa hali ya dharura wa kukabiliana na Covid-19, Kenya na mashirika mengine ya usalama yatashirikiana kuratibu miradi kama ule wa Adopt a Needy Family, ambapo raia wa Kenya wanasaidiana kipindi hiki cha janga kuhakikisha hatua zinachukuliwa bila kufuata urasimu

7.Afisa yeyote wa polisi atakayekiuka sheria wakati anatekeleza hatua za kukabiliana na usambaaji wa virusi atakabiliwa na mkono wa sheria.

Unaweza pia kutazama:

Maelezo ya video,

Coronavirus: Utajuaje kuwa umeathirika na virusi?

Upimaji

Wakati huohuo, Kenya imepokea karibia vifaa 40,000 vya kupimia Jumatano ikiwa ni katika kuimarisha hatua za kuimarisha uwezo wa kupima watu kunakoendana na lengo la kupima, kutengwa walioathirika na kutibu.

Wizara ya afya imetangaza Jumatano kwamba nchi hiyo imepokea vifaa vya kupimia mfano wa vijiti 18,900, vifaa vya kuwekea vipimo 18,912, sare na vifaa vya kujikinga kwa wahudumu wa afya 3,790, vipimajoto vya kushikililiwa, glavu na mashine za kupuma kutoka kwa mfanyabiashara wa kundi la Alibaba, Jack Ma.

Waziri amesema Kenya pia ilikuwa imepokea shehena ya glavu, vifaa vya kujikinga kwenye uso na barakoa zinazovaliwa wakati wa upasuaji kutoka China, Ufaransa na Ujerumani kupitia Shirika la Afya Duniani (WHO).