Virusi vya corona: Wafanyabiashara wadogo Kenya walivyoathirika

Virusi vya corona: Wafanyabiashara wadogo Kenya walivyoathirika

Huku virusi vya Corona vikiendelea kusambaa barani Afrika, wafanyibiashara wengi nchini Kenya wamelazimika kuratibu upya jinsi wanavyoendesha shughuli zao ili mradi wauze bidhaa zao wakizingatia amri ya kutotoka nje usiku.

Soko la Eastleigh jijini Nairobi, linaloendeshwa ndani ya masaa 24 na kuhudumia wateja kutoka sehemu mbali mbali za nchi na hata nchi jirani, linaendelea kukaridia hasara kubwa kutokana na makali ya virusi vya Corona.

Mwandishi wa BBC Hudheifa Aden anatupa tathmini ya kina.