Virusi vya corona: Wakenya waelezea hofu ya kuwekwa karantini ya lazima

  • Na Basillioh Mutahi
  • BBC Nairobi
Wakenywa waliowekwa karantini katika chuo kikuu cha Kenyatta karibu na Nairobi walalamikia kutelekezwa - Aprili 15, 2020

Chanzo cha picha, Reuters

Kama watu wengine kote duniani, Rachel Gichuma ana wasiwasi mkubwa kuhusu kuambukizwa virusi vya corona.

Lakini pia ana hofu zaidi kuhusu kutengwa kwa lazima katika vutuo vya karantini nchini kenya.

Mama huyo anayeishi pekee na wanawe pacha wa mwaka mmoja anaamini kwamba wale ambao tayari wametengwa katika vituo vya serikali, hawapo katika mazingira bora zaidi ya jela.

''Vyoo vyao ni vichafu na hata waoshaji wake mara nyengine hulalamika jinsi vyoo hivyo vilivyovichafu'', mwanamke mmoja ambaye ametengwa aliambia BBC.

Ni kwa sababu hakuna maji, hivyobasi watu wanagusa mifereji hiohio wakati unapotaka kuosha mikono hata iwapo kuna maji.

''Najaribu kuwa makini wakati ninapoingia nyumbani'', lazima nioge kabla ya kushika wanangu, anasema Rachel Gachuna.

Maelezo ya video,

Virusi vya Corona: Jinsi marufuku ya misongamano inavyokumbana na vikwazo Afrika

Watu wanaowasili nchini Kenya kutoka mataifa yalioathirika na maambukizi na wale waliokaribiana na wagonjwa wamepelekwa katika vituo vya lazima vya karantini kwa siku 14.

Hatahivyo muda wa karantini umeongezwa mara mbili kwa kila mtu katika vituo hivyo ambapo mtu ameonyesha kuwa na dalili za virusi hivyo - na pia wanalazimishwa kulipia mahitaji.

Kumekuwa na malalamishi kwamba masharti ya kutokaribiana hayawezi kuafikiwa katika vituo vingine kwa sababu watu ni wengi.

''Omba Mungu kwamba haitakufanyikia kwasababu kwa kweli sijui nitafanyaje'', bi Gachuma aliambia BBC.

Kwa sasa yuko likizo baada ya kuamua kufanyia kazi nyumbani katika mji mkuu wa Nairobi, licha ya kwamba wakaazi wa mji wanaweza kwenda nje wakati wa mchana.

Jaribio la kutoroka

Ili kuilinda familia yake dhidi ya maambukizi, yeye huenda dukani ili kununua bidhaa muhimu na asingependelea hata kidogo kutoka nje.

Wakenya sasa wanalazimika kuvalia barakoa katika maeneo ya umma na mabasi yamelazimika kubeba abiria wachache, lakini agizo la kutokaribiana lina changamoto.

Najaribu kuwa makini.

''Wakati ninapoingia nyumbani, lazima nioge kabla ya kuwashika wanangu. Huwezi kujua iwapo nguo zako zimeshikwa na nini'', alisema.

Pia alilazimika kumuachisha kazi yaya wake mmoja ambaye alikuja ili kumsaidia kuwalea watoto wake wiki hiyo.Escape attempt

Na hofu yake iliongezeka wiki iliopita baada ya makumi ya watu kujaribu kutoroka karantini katika chuo kikuu cha Kenyatta mjini Nairobi , kutokana na mazingira duni ya kituo hicho.

''Kwanza kwa sababu kutoweza kulipa na pili kwasasbu haileti maana yoyote ya kisayansi kusalia katika kituo hicho'', Simon Mugambi , mmoja ya waliojaribu kutoroka alisema,

Wengine walizungumzia athari zao za kisaikolojia na kiakili baada ya serikali kuwaongezea muda wa kuishi katika vituo hivyo kwa zaidi ya siku 14.

Lakini kundi hilo lililazimishwa kurudi. Mtu mwengine aliyelalamika alisema: Ni kama hutakikani tena , ni kana kwamba upo chini ya mikono ya serikali.

Unaweza kusoma zaidi:

Hakuna kusafiri kuingia ama kutoka mjini Nairobi na maeneo mengine ya mji. Masharti kama hayo pia yamewekewa kaunti za pwani.

Shule, klabu za burudani, maeneo ya burudani makanisa na misikiti

kila mtu anahitajika kuvalia barakoa katika maeneo ya umma na wale watakaokaidi watakamatwa.

Waajiri wametakiwa kuwaruhusu wafanyakazi wao kufanya kazi nyumbani

Maeneo yote ya kufanya kazi yanahitajika kuwa na eneo la kuosha mikono , maji na sanitizer

Ulipaji wa fedha usiotumia malipo ya moja kwa moja unahitajika.

Hatua za kukabiliana na virusi vya coronaKenya's :

  • Kufungwa kwa mipaka na kuwekwe kwa marufuku ya usafiri wa ndege za abiria
  • Kuwekwa kwa kafya kuaniza saa moja usiku 19:00 and 05:00 local time
  • Marufuku ya usafiri kuingia na kutoka jiji la Nairobi na maeneo yaliyo karibu. Hatua kama hizo zimechukuliwa katika miji mitatau ya pwani ya nchi hiyo.
  • Shule, baa, kumbi za burudani, makanisa na misikiti kufungwa.
  • Watu watakiwa kuvalia barakoa wakiwa sehemu za umma la sivyo wakamatwe
  • Waajiri waombwa kuwaruhusu wafanyikazi wao kufanya kazi nyumbani.
  • Maeneo yote ya kazi yatakiwa kutenga sehemu ya kunawa mikono kwa maji safui na sabuni au kutumia vyeyuzi vilivyoidhinishwa.
  • Watu wahimizwa kutotumia pesa taslimu na badala yake kutumia mfumo wa kielektroniki kunua bidhaa au kulipia huduma.

Kufikia mwisho wa mwezi Machi, serikali ilikuwa na zaidi ya watu 50 waliowekwa karantini katika mahoteli , nyumba za kulala za wanfunzi, shule na vyuo vikuu ambazo gharama yake ni kati ya dola 20 na hadi 200 kwa siku.

Baadhi yao sasa zimefunga - lakini vitano vipo katika awamu ya tatu ya karantini .

Kati ya watu 2,336 waliowekwa karantini 425 bado wanahudumia masharti hayo.

Wengine wanaishi vyema

Rubani mmoja aliyewasili kutoka Dubai tarehe 24 Machi, aliambia BBC kwamba kampuni hiyo ya ndege ilikuwa ikiwalipia gharama yao ya karantini na pia imesema kwamba itawafanyia ushauri nasaha baada ya kumaliza muda waliowekewa.

Kusalia karantini kwa muda mrefu mbali na familia yako nio ni hali ngumu sana , alisema rubani huyo ambaye hakutaka kutajwa.

Maelezo ya video,

Coronavirus: Wafanyakazi wa kipato cha chini Kenya kama Esther wahofia

Maisha yawekwa hatarini

Kundi moja la wanaharakati , Kelin , limewasilisha malalamishi kuhusu hali ya mazingira na ukosefu wa habari wanazopatiwa wale waliopo katika karantini.

"Serikali haijakuwa wazi kuhusu ni nani anayesimamia gharama, serikali haijakuwa wazi kuhusu ni lini watu wanapaswa kufanyiwa vipimo, lilisema.

Wizara ya afya imesema kwamba inajua kile kinachowakwaza, lakini inasisitiza kwamba agizo hilo linatekelezwa kwa lengo la kuulinda umma kwa kuwa baadhi ya wale waliowekwa karantini wamepatikana na ugonjwa huo wa Covid 19 unaosababisha magonjwa ya mapafu.

Patrick Amoth, ambaye anasimamia afya ya umma katika wizara ya Afya pia alitaja vituo vitano wakati walipoongezewa muda wa kusalia karantini kwa mara ya pili baada ya watu kushindwa kufuata maagizo ya kutokaribiana.

Mkuu wa hospitali kuu ya Kenyatta nchini humo pia alikosoa tabia ya baadhi ya wale waliopo karantini.

"Wamekuwa maadui ata kwa wafanyakazi , hata baadhi ya wafanyakazi wangu wamepigwa'' , alisema Evanson kamuri.

"Wanaweka maisha yao hatarini , kile kitu kidogo ambacho unaweza kuwafanyia kama Wakenya , ni usaidizi na kuwanyosha heshima'', alisema daktari huyo.

lakini kuongezwa kwa muda katika karantini kunamaanisha kwamba watu wamepoteza kazi zao mbali na kukabiliwa na gharama za juu.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Maeneo ya umma jijini Nairobi yamekuwa yakinyunyuziwa dawa nyakati za usiku

Kwa Bi Gachuna, meneja wa mipango hatua hiyo itakuwa janga.

Tayari ana wasiwasi kuhusu fedha baada ya kampuni yake kufungwa kutokana na masharti hayo ya virusi vya corona. Na sasa atalazimika kuwalea watoto wake yeye mwenyewe.

Rubani wa shirika la ndege la Kenya Airways ambaye anahitajika kujitenga nyumbani kwa wiki moja zaidi, anawashauri wengine kufanya kila kitu ili kuepuka kuwekwa katika karantini ya lazima.

''Karantini sio eneo zuri la kuishi,hivyobasi iwapo unaweza kuepuka kwenda katika eneo hilo, kuwa msafi na kutokaribiana na watu wengine ili kuzuia matatizo yote haya'', alisema.

Hiyo ndiyo hali inayomtia tumbo joto Bi. Gachuna na wengine kama yeye.