Virusi vya corona: Mbinu ya kuwalaza wagonjwa wa corona kifudifudi inavyookoa maisha yao

Mwezi Machi Shirika la Afya Duniani pia lilipendekeza mwezi wagonjwa wanaougua Covid-19 ambao wana tatizo la kupumua kulazwa kifudifudi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mwezi Machi Shirika la Afya Duniani pia lilipendekeza mwezi wagonjwa wanaougua Covid-19 ambao wana tatizo la kupumua kulazwa kifudifudi

Kujipata katikati ya mgogoro unaosababishwa na janga la corona, ni tukio ambalo mara kwa mara hufanyika katika hospitali nyingi duniani.

Makumi ya wagonjwa husalia kwenye vitanda vyao, wakiwa wamewekewa vifaa vya kuwasaidia kupumua huku wakiangaliwa kwa makini na maafisa wa afya ambao hulindwa na nguo maalum pamoja na barakoa.

Lakini kuna kitu ambacho kinavutia katika picha hizi, baadhi ya wagonjwa wanaougua covid 19 hulazwa kifudifudi.

Lakini kwa nini walazwe hivyo?

kunaongeza kiwango cha oksijeni mwilini. Ni mfumo wa jadi ambao umethibitisha kufanya kazi kukabiliana na magonjwa hatari ya mapafu.

Mbinu hiyo inayojulikana katika taaluma ya afya kama kulala juu chini, imeanza kutumiwa kwa kiwango kikubwa miongoni mwa maelfu ya wagonjwa ambao ni waathiriwa wa mlipuko huo ambao wanaendelea kutibiwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi.

Mbinu hii inasaidia watu kuimarisha kiwango cha oksijeni kinachoingia katika mapafu.

Hii imeelezewa BBC na profesa wa tiba ya mapafu na chumba cha wagonjwa mahututi katika chuo kikuu cha tiba cha John Hopkins, Panagis Galiatsatos.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mbinu hii inasaidia watu kuimarisha kiwango cha oksijeni kinachoingia katika mapafu.

''Wagonjwa wengi waliyo na virusi vya corona hawapati oksijeni ya kutosha katika mapafu yao na hivyobasi huyaharibu.Na ijapkkuwa tunawapatia oksijeni katika vituo vya afya, mara huwa haitoshi. Na kile tunachofanya ni kuwalaza kifudifudi ili kuruhusu mapafu kupanuka tena'', anasema.

Mtafiti huyo anaongezea kwamba maeneo mazito ya mapafu huwa yako mgongoni hivyobasi mgonjwa anapolalia mgongo wake tatizo la wao kushindwa kupumua huongezeka.

Husaidia damu kusambaa

"Kufunguka kwa mapafu wakati mgonjwa anapolalishwa kifudifudi husaidia kusambaa kwa damu zaidi. Mbinu hiyo ina ufanisi na tumeithibitisha na wagonjwa wengi'', anasema.

''Mbinu hiyo imetambulika na madaktari wengi hali ya kwamba shirika la Afya Duniani pia limeipendekeza mwezi Machi mwaka huu kwa wagonjwa wanaougua Covid-19 ambao wanaugua magonjwa ya tatizo la kupumua, "anasema.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Pronation is an ancient technique that has been shown to be effective in fighting serious respiratory diseases.

Cha zaidi ni kwamba uchunguzi uliofanyiwa wagonjwa 12 waliokuwa katika hali mahututi waliotibiwa katika hospitali ya Jinyintan nchini China ulibaini kwamba wagonjwa ambao hawalazwi kifudifudi mapafu yao hukosa kupanuka vizuri ili kuingiza oksijeni ya kutosha mbali na damu kusambaa.

Uchunguzi huo ulibaini kwamba wagonjwa wanaolala kifudifudi hupata nafuu kutokana na oksijeni wanayopokea.

Je hatari za kulala kifudifudi ni zipi?

Kwa sasa kile ambacho kinaweza kuonekana kama utaratibu rahisi kinaweza kuchukua muda mrefu. WHO inasema kwamba kwamba ili kuweza kufanikiwa katika mbinu hiyo unahitaji watalaam kadhaa.

Panagis Galiatsatos anaelezea kwamba kwa mara ya kwanza kituo cha afya cha John Hopkins kiliunda kundi la maafisa wa Afya wenye utaalam wa kuwalaza wagonjwa kifudifudi .

''Katika hali hiyo, iwapo mgonjwa wa Covid 19 yupo katika chumba cha wagonjwa mahututi ambapo wafanyakazi hawajui kufanya utaratibu huo , huwaita wataalam ambao watamlaza mgonjwa kifudifudi'', anasema.

Kwa mgonjwa kulazwa kifudifudi kunaweza kuleta matatizo zaidi.

''Kunona kupitia kiasi ndio changamoto kuu. Uangalizi wa makini unafaa kutumiwa miongoni mwa wagonjwa walio na majeraha ya kifua. Ni vyema kuchukua tahadhari iwapo mgonjwa ana mrija wa kumsaidia kupumua shingoni'', anaelezea Galiatstos.

''Sio rahisi. Inawachukua takriban watu wanne ama hata watano kufanikiwa'', anaongezea.

"Uingizaji hewa kwa kutumia mashine wakati mgonjwa amelala kifudifudi hupendelewa sana miongoni mwa wagonjwa wa tatizo la kupumua wenye umri mkubwa. Mgonjwa huwekewa mashine hizo kumsaidia kati ya saa 12 hadi 16 kwa siku'' , linasema shirika hilo.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Virusi vya corona vinaweza kusababisha matatizo ya kupumua

Tafiti za jadi

Lakini je mbinu hii ilipatikana wapi?

Faida za kulala kifudifudi ziligunduliwa miaka ya 1970. Lakini ilichukua hadi mwaka 1986 ambapo mbinu hiyo ilianza kutumika zaidi duniani.

Mmoja wa madaktari aliyeongoza utafiti wa kwanza alikuwa Muitaliano Luciano Gattinoni, ambaye anafanya kazi kama profesa emiratus katika chuo kikuu cha Statale mjini Milan na anajulikana kama mtaalamu wa kuweka watu ganzi na ufufuzi.

Yeye pamoja na kundi lake , alianza kutumia mbinu hiyo mara kwa mara na kuchapisha utafiti wa kisayansi kuhusu faida zake.

''Katika mazungumzo na BBCMUndo, mtafiti huyo anasema kwamba , mara ya kwanza , mbinu hiyo ilipingwa sana kwa kuwa jamii ya tiba ilikuwa ya kihafidhina. lakini kwa sasa inatumika kote duniani'', anasema.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Janga la corona limesababisha maafa makubwa koto duniani

Mtaliano huyo anaelezea kwamba kumlaza mgonjwa kifudifudi sio tu kwamba kunamsaidia mgonjwa kupata oksijeni ya kutosha katika mapafu bali pia uzito unaokalia mapafu hupungua kwa kiwango kikubwa.

Sambamba na Gattinoni .

Tafiti nyengine zilifanywa mwaka 2000 ambapo ziliunga mkono mbinu hiyo ya mgonjwa kulazwa kifudifudi.

Hivi ndivyo Panagis Galiatsatos anaelezea.

Utafiti uliofanywa nchini Ufaransa 2000 ulionyesha kwamba wagonjwa waliimarika kwa kupata oksijeni ya kutosha lakini pia walikuwa na uwezo mkubwa wa kupona.