Virusi vya Corona: Taarifa ambazo si sahihi kuhusu corona zimetapakaa Afrika?

Large pot on cooking stove

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Steam from hot water is not yet proven to kill the virus

Mataifa mengi barani Afrika yanakabiliwa na ongezeko la idadi kubwa ya kesi mpya za coronavirus, na serikali nyingi zimekuwa zikisisitiza hatua kali za kuchukua tahadhari katika jamii.

Wakati huu wa mapambano dhidi ya homa kali ya mapafu, habari zakupotosha zimekuwa zikisambaa barani Afrika.

1. Kuvuta hewa yenye mvuke mkali sana ni hatari

Madai ya kuwa kuvuta pumzi kwa mvuke ni matibabu madhubuti dhidi ya homa kali ya mapafu umeenea tena, wakati huu nchini Tanzania na imeidhinishwa na ya rais wake.

Kama sehemu ya kuweka mkazo zaidi juu ya tiba za asili, Rais John Magufuli amesema kuwa kuvuta pumzi ya mvuke kunaua virusi kwenye pua na mdomo.

Bwana Magufuli alipendekeza kuwa joto la juu litafanya kazi dhidi ya virusi hivyo kama sehemu ya mkakati bora wa kukabiliana na janga hili la dunia.

Ingawa matibabu ya mvuke wa joto la juu hutumiwa kwa kusafishia viwandani katika maeneo kama vile hospitali, kuvuta pumzi kwenye joto hili kunaweza kuwa hatari sana kwa mwili wa binadamu, kulingana na Keith Neal, mtaalam katika kuenea kwa magonjwa ya kuambukiza katika Chuo Kikuu cha Nottingham huko Uingereza.

Maambukizi ya homa kali ya mapafu Afrika.

Anasema kwamba ikiwa mvuke wa moto unaingia ndani ya mwili wako kujaribu kuua virusi, mapafu yako yanaweza kuharibika kwa njia isiyoweza kutibika.

Pia, mvuke wa maji kutoka kwenye sufuria ya kuchemsha hupoa haraka pale unapoingia mwilini na sio moto kuwa na athari dhidi ya virusi.

Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) limeonya dhidi ya kutumia maji ya moto kwaajili ya kuoga kama sehemu ya kumaliza virusi, hii ni hatari sana unaweza kuungua.

2. Raia kutoka China wanaomiliki biashara nchini Nigeria hawajavamiwa

Kama ripoti zinavyo sema Waafrika wanao ishi nchini China wanaokabiliwa na ubaguzi, watu wengine wameanza kueneza video ambazo sio za kweli, wakidai kuwa wanaonyesha watu kulipiza kisasi dhidi ya jamii ya Wachina barani Afrika.

Kesi inayoonekana ni video iliyosambaa kuonyesha biashara zinazo milikiwa na China zikiwaka moto nchini Nigeria.

Picha hizo zinaonyesha maduka yakiwaka moto katika eneo maarufu la soko huko Ibadan kusini magharibi mwa Nigeria mwezi huu.

Gazeti la Punch huko Nigeria liliripoti juu ya moto huo na likiwahusisha wafanyabiashara wa Nigeria bila kutaja biashara za Wachina.

Video hiyo ambayo imetazamwa zaidi ya mara milioni baadaye ilitolewa na Twitter kwa sababu walisema "ilikiuka sheria za Twitter".

3. Utumiaji wa pombe hakuzui maambukizi dhidi ya Covid-19

Gavana wa mji mkuu wa Kenya, Nairobi, amekosolewa kwa maneno ya kupotosha kuhusu vileo na corona.

Gavana Mike Sonko alikuwa akielezea ni kwanini anajumuisha chupa za Hennessy cognac katika vifaa vya chakula kwa watu wanaoishi katika mazingira magumu katika jiji hilo, akisema kuwa ni "sanitiser ya koo".

"Kutokana na utafiti ambao umefanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) na mashirika anuwai ya afya imeonekana kuwa pombe inachukua jukumu kubwa sana katika kuua ugonjwa huo, au aina yoyote ya virusi," alisema.

Inaonekana amepotosha ushauri wa shirika la afya WHO.Inasema kunywa pombe haikulindi dhidi ya ugonjwa wa corona, lakini inazungumzia ufanisi wa gel inayotokana na pombe kusafisha mikono yako.

Ushauri wa WHO unaongeza kuwa unywaji pombe "kuna uwezekano wa kuongeza hatari za kiafya ikiwa mtu ameambukizwa na virusi".

4.Barakoa za rangi ya blu haziwezi kuambukiza

Machapisho mawili kwenye mtandao wa Facebook, ambayo yamekuwa yakiwasihi Waafrika kutovaa vifuniko vya uso wa samawati huku madai kwamba zimepuliziwa sumu zimesambaa sana.T

kuna madai ya kunukuu kutoka kwa mwanzilishi wa Amazon Jeff Bezos na mpango unaodhaniwa wa kusambaza barakoa ambazi si salama kwa matumizi ya binadamu.

"Wapendwa Waafrika, epukeni kuvaa barakoa za bluu ambazo zimetengenezwa Amerika na Ulaya kwa sababu barakoa zina sumu hatarishi[sic]" chapisho hilo linasema hivyo. lakini halijafafanua ni sumu gani wanayopaswa kuwa nayo.

chapisho kwenye ukurasa mwingine - wakati huu ikinukuu kwa uwongo, mkuu wa Shirika la Afya Ulimwenguni - pia inawahimiza watu kutovaa barakoa za bluu.

Mary Stephen, kutoka ofisi ya WHO bara la Afrika, aliiambia BBC shirika hilo halijapata ripoti yoyote kuhusu barakoa zina maambukizi.

"Nchi zinapata barakoa kutoka katika vyanzo tofauti, na hatuna taarifa za maambukizi," anasema.