Virusi vya corona: Je, Trump yuko sahihi kuikosoa WHO?

WHO iliisifia China jinsi ilivyokabiliana na mlipuko wa Corona

Chanzo cha picha, AFP/Getty

Maelezo ya picha,

WHO iliisifia China jinsi ilivyokabiliana na mlipuko wa Corona

Rais wa Marekani Donald Trump amelishutumu Shirika la afya duniani (WHO) kwa utawala mbaya na kuficha ukweli kuhusu kusambaa kwa virusi vya corona baada ya virusi hivyo kutokea Uchina.

Aliongeza kuwa atasitisha ufadhili kwa WHO wakati utawala wake ukitathmini hatua zake.

Peter Piot, Kutoka taasisi ya Uingereza ya mafunzo ya usafi na dawa za maeneo ya joto - London School of Hygiene and Tropical Medicine, anasema hii itakua ni ''hatari na kuona karibu"

Lakini Trump anasababu ya kukosoa jinsi WHO ilivyoshughulikia virusi?

WHO inafanya nini?

Shirika la WHO, lilianzishwa mnamo mwaka 1948, ni sehemu ya umoja wa Mataifa inayohusika na afya ya dunia ya umma, likiratibu kampeni za chanjo, dharura za kiafya na kusaidia nchi kwa huduma za kimsingi za afya.

Shirika hilo linadhaminiwa na ada na michango ya kujitolea kutoka mataifa 194 wanachama wa Umoja wa Mataifa, huku Marekani ikiwa mchangiaji mkuu zaidi wa ufadhili huo kama nchi.

Je WHO ilishindwa kuikabili Uchina?

Rais Trump amelishutumu shirika la WHO kwa kushindwa kuhoji maelezo ya mwanzo ya Uchina iliposema hapakua na ushahidi wa maambukizi kati ya binadamu na binadamu ya virusi vya corona.

China iliifahamisha kwa mara ya kwanza WHO kuhusu "homa ya mapafu ambayo chanzo chake hakifahamiki, tarehe 31 Disemba".

Chanzo cha picha, Reuters

Tarehe 5 Januarii, shirika hilo lilisema kuwa taarifa lilizokua nazo zilionyesha kuwa "hakuna ushahidi muhimu wa maambukizi kati ya binadamu na binadamu''.

Na tarehe 14 Januari, shirika hilo lilituma ujumbe wake wa twitter kwamba uchunguzi wa awali wa Wachina umebaini kuwa "hakuna ushahidi wa wazi wa maambukizi kati ya binadamu na binadamu" ya virusi.

Siku hiyo hiyo, hata hivyo , Tume ya afya ya Wuhan ilisema kuwa Wuhan ilisema uwezekano wa maambukizi ya binadamu na binadamu hauwezi kuondolewa, ingawa hatari ya kuhama kwa virusi kutoka kwa mnyama hadi binadamu ni ya kiwango cha chini.

Katika kipindi hicho hicho, taarifa nyingine za WHO zililiibua kuwepo kwa baadhi ya uwezekano wa maambukizi baina ya binadamu, ikiweleza kile kilichofahamika juu ya virusi vingine vya corona kama dalili ya ugonjwa mbaya wa mfumo wa kupumua (Sars).

Na Januari 22, WHO, kufuatia ziara fupi ya kikazi nchini Uchina , alitoa taarifa ya wazi zaidi iliyosema kwamba maambukizi ya binadamu kwa binadamu yapo Wuhan.

Je WHO ilipuuza wataalamu kutoka Taiwan?

Bwana Trump alisema kulikua na "taarifa za kuaminika za maambukizi kati ya binadamu na binadamu wezi Disemba ", akimaanisha onyo ambalo Taiwanilisema ililituma kwa WHO.

Wanasayansi wa Taiwan walikua wametembelea Wuhan muda mfupi baada ya kutokea kwa virusi vya corona kwa mara ya kwanza.

Chanzo cha picha, Getty Images

Lakini ushahidi uliochapishwa hadi sasa unaonyesha kuwa mawasiliano baina ya Taiwan na WHO hayakutaja kusambaa kwa virusi kati ya binadamu na binadamu.

Taiwan sio mmoja wa wanachama wa WHO kwa sababu haitambuliwi na Umoja wa Mataifa.

WHO inasema imesema imekua ikiwashirikisha wataalamu mawasiliano yake na Taiwan wakati wote.

Lakini mwezi uliopita baada ya afisa wa ngazi ya juu wa WHO kukataa kuzungumzia kuhusu jinsi Taiwan walivyoshulikia mlipuko, shirika hilo lilishutumiwa kwa kushawishiwa na Uchina.