Virusi vya corona: Ni nini kinasababisha vifo visivyoelezeka katika jimbo la Kano Nigeria

Rais Muhammadu Buhari amesema kuwa atarefusha zaidi muda wa kukaa nyumbani katika jimbo la Kanowakati masharti yatakapolegezwa kwingineko Nigeria

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Rais Muhammadu Buhari amesema kuwa atarefusha zaidi muda wa kukaa nyumbani katika jimbo la Kanowakati masharti yatakapolegezwa kwingineko Nigeria

Rais wa Nigeria ameonesha wasiwasi wake juu ya idadi ya vifo inayoongezeka huko kaskazini jimbo la Kano, huku kukiwa na wasiwasi kwamba vifo hivyo huenda vinatokana na ugonjwa wa Covid-19.

Rais Muhammadu Buhari amesema jimbo la Kano litawekewa kanuni za kusalia ndani kwa wiki mbili zaidi na kwamba anatuma timu ya uchunguzi.

Waziri wa afya wa Nigeria Dr Osagie Ehanire amesema hali hiyo inafuatiliwa kwa karibu.

hatua hiyo inajiri baada ya maafisa nchini humo kusema rais wa Marekani, Donald Trump ameahaidi kutuma mashine za kusaidia kupumua katika mataifa ya magharibi ya Afrika ili kukabiliana na mlipuko wa Corona.

Katika mazungumzo ya simu kati ya rais Muhammadu Buhari na Trump, rais huyo wa Marekani alikuhakikishia rais huyo kuwa Nigeria wategemee msaada wote kutoka Marekani katika kipindi hiki cha mlipuko.

Lakini uchunguzi wa awali wa serikali umeondoa uwezekano kwamba vifo hivyo vinahusiana na ugonjwa wa virusi vya corona.

Mamia ya watu inasemekana kwamba wamekufa lakini serikali haina idadi rasmi ya wanaoendelea kuangamia.

Awali wachimbaji wa makaburi walipaza sauti kwamba walikuwa wanazika watu wengi zaidi kuliko kawaida.

Ali, Mchimbaji kaburi katika makaburi ya Abattoir, ameiambia BBC: "Hatujawahi kushuhudia kitu kama hichi, tangu kulipotokea mlipuko wa kuhara ambao huwa tunahadithiwa na wazazi wetu. Hiyo ilikuwa ni miaka 60 iliyopita."

Maelezo ya picha,

Mchimbakaburi Ali anasema anawazika watu wengi zaidi

Wiki hii, gavana wa jimbo hilo alitoa taarifa akisema "vifo vya ajabu vinatokea" ambavyo havihusishwi na virusi vya corona.

Lakini baada ya uchunguzi wa kina wa kiini cha vifo hivyo", kwa matokeo ya awali unaonesha kwamba vifo hivyo havina uhusiano wowote na ugonjwa wa Covid-19.

Serikali imesema "taarifa kutoka wizara ya afya imeonesha kwamba vifo vingi vilisababishwa na matatizo yanayotokana na shinikizo la juu la damu, ugonjwa wa kisukari, malaria na maradhi ya utando wa ubongo.

"Gavan Abdullahi Umar Ganduje anasubiri taarifa kamili kutoka kwa wizara ya afya ili hatua stahiki ziwezi kuchukuliwa."

Vitui vya kibiashara na kiviwanda upande wa kaskazini, Kano imekuwa kitovu cha virusi vya corona kaskazini mwa Nigeria. Eneo hilo lina idadi kubwa ya watu bado limewekewa kanuni ya kutotoka nje katika juhudi za kudhibiti usambaaji wa virusi hivyo.

Upimaji wa corona umefikia wapi?

Maafisa wa serikali walianza kupima ugonjwa wa Covid-19 wiki mbili zilizopita na maabara moja imelazimika kufungwa kwasababu ya maambukizi.

Vipimo vinatumwa katika mji mkuu wa Abuja ambapo mamlaka inasema hilo linachelewesha mchakato wa kutangaza ni visa vingapi vimebainika katika jimbo hilo.

Dr Sani Aliyu, mratibu wa taifa katika jopo lililotangazwa na rais kukabiliana na Covid-19 amesema timu ya wataalamu watano wa kimatibabu wamepelekwa katika jimbo la Kano kusaidia katika mchakato wa kufunguliwa tena kwamba kituo cha kupima virusi hivyo wiki hii baada ya kufungwa kwa muda.

Maafisa pia wana mpango wa kufungua maabara ya pili katika chuo kikuu cha Bayero, kupima ugonjwa wa Covid-19 kuanzia wiki ijayo.

Ni watu wangapi waliokufa?

Bado haijafahamika ni watu wangapia ambao wamekufa wakati hilo linaendelea kuzua taharuki miongoni mwa jamii. Vifo katika sehemu nyingi nchini Nigeria havisajiliwi na hivyo basi wale wanaokufa manyumbani idadi yao haijulikani.

Hilo linafanya iwe vigumu kufahamu idadi kamili ya waliokufa katika wiki za hivi karibuni.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Wahudumu wa afya wakiandaa vitanda kwa ajili ya kituo cha kujitenga cha wagonjwa wa corona mjini Abuja mwezi Aprili

Sabitu Shaibu, naibu wa jopo kazi lililoundwa na serikali kushughulikia Covid-19, ina matumaini ya kutoa taarifa ya awali kufikia wiki ijayo lakini inasemekana kwamba vifo 640 vilivyorekodiwa vimetokana na sababu za asili.

Jopo hilo limesema waliokufa watafanyiwa uchunguzi wa kina ili kusaidia kubaini chanzo cha vifo vyao.

Ikiwa sio virusi vya corona, ni kitu gani ambacho huenda kinaendelea?

Hospitali za kibinafsi ambazo zinachukuliwa kama kiungo muhimu katika sekta ya afya eneo hilo, zimefungwa kwasababu ya hofu ya virusi vya corona. Hilo linaweza kumaanisha wale wenye kuuguwa huenda wanakosa kusaidiwa na pengine hilo limechangia vifo hivyo.

Daktari Nagoma Sadiq anayefanyakazi katika hospitali ya Aminu Kano, anasema huenda hiyo imeongezea idadi ya vifo vilivyotokea lakini hajaondoa uwezekano wa virusi vya corona pia kuchangia hali hiyo.

"Idadi ya vifo inashangaza. Lakini pengine ni kwasababu ya kupungua kwa idadi ya taasisi za afya katika jimbo hilo.

"Kwasababu kuna wagonjwa wengi wa shinikizo la juu la damu, kisukari, asthma, saratani ambao hawawezi kupata matibabu hospitalini. Amri ya kusalia ndani inaathiri kila mmoja.

"Idadi ya wengi ambao ni maskini hawana hata uwezo wa kupata gari la kuwapeleka hospitali."

Image captionMore funerals are happening

Mchimbaji makaburi Ali, anakubali na kuongeza kwamba "hali ilivyo kwasasa huenda inachangiwa na janga la corona, wengine wanasema ni changamoto za maisha. Watu wana matatizo mengi maishani mwao, pia wanakosa amani moyoni."

Hata hivyo Covid -19 inafahamika kuathiri zaidi wale wenye matatizo mengine ya afya na pengine hilo linaweza kuwa na uhusiano na virusi vya corona. Namna pekee ya kufahamu hilo ni kupima virusi vya corona.

Daktari Sadiq pia anasema kwamba bado kuna wasiwasi kuhusu maambukizi ya homa ya Lassa katika jamii. Jimbo hilo limethibitisha visa vitano na kifo kimoja, kulingana na taarifa za hivi karibuni kutoka Kituo cha Kudhibiti Maambukizi cha Nigeria.

Jimbo la Kano lina visa 77 vya virusi vya corona na vifo vitat tayari vimethibitishwa.

Mamlaka imetaka raia kutokuwa na wasiwasi.

Kipi kingingine alichosema Rais?

Rais Buhari alitangaza kuanza kulegeza masharti polepole katika mji wa Abuja, Lagos na jimbo jirani la Ogun kuanzia Jumatatu ijayo.

Lakini pia alisema kwamba serikali itatangaza amri ya kutotoka nje kote nchini humo kuanzia saa mbili usiku hadi kumi na mbili asubuhi, kila mmoja anahitajika kuvaa barakoa na kutosafiri baina ya maeneo.

Marufuku ya mikusanyiko ya watu na kidini bado imepigwa marufuku.