Virusi vya Corona: Kwa nini ugonjwa huo ni hatari zaidi kwa wanaume zaidi ya wanawake

Wagonjwa wa virusi vya corona nchini India

Kitu cha kushangaza kuhusu virusi vpya vya corona ni kwamba ni hatari zaidi kwa wanaume zaidi ya wanawake.

Kufikia tarehe 7 mwezi Aprili takriban wanaume 2,232 walikuwa wamefariki kutokana na virusi hivyo mjini New York - Kitovu cha maambukizi nchini Marekani ikilinganishwa na wanawake 1,309 kulingana na idara ya afya nchii humo.

Katika mahospitali kulikuwa na wagonjwa wanaume 40,000 ikilinganishwa na wanawake 34,000.

Kiwango cha vifo vya Covid 19 miongoni mwa watu 100,000 mjini New York kilikuwa na wanaume 55 na chini ya wanawake 30.

Wanaume wengi wamekutwa na ugonjwa huo zaidi na wanaonekana kupatwa na maafa mabaya.

Mshirikishi wa Ikulu ya whitehouse kuhusu maswala ya Covid-19 Dkt Deborah Birx awali alizungumzia kuhusu suala hili linalotia wasiwasi baada ya kuchunguza takwimu nchini Itali, ambapo picha za vyumba vya wagonjwa mahututi zilionyesha wanaume wenye umri mkubwa wakipumua kwa usaidizi wa mashine.

Data ya idadi ya vifo iko juu miongoni mwa wanaume

Idadi ya vifo miongoni mwa wanaume inaonekana kuwa maradufu katika kila umri wa wanawake.

''Hilo ni suala ambalo linafaa kutuamsha sote ili kuendelea kuwalinda wenzetu walio katika vyumba vya uuguzi'', alisema Birx wakati alipokuwa akitoa habari kwa jopo la utawala wa Trump linalokabiliana na virusi vya corona.

Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa nje ya China ulibaini kwamba kiwango cha vifo miongoni mwa wanaume ni asilimia 2.8 ikilinganishwa na asilimia 1.7 ya wanawake.

Uchanganuzi mwengine wa China ulibaini kwamba kati ya watu waliofariki na virusi hivyo asilimia 60 walikuwa wanaume.

Wakati Itali ilivyoripoti vifo vyake hivi majuzi , asilimia 72 ya wale waliofariki walikuwa wanaume . Utafiti mwengine uliiweka idadi hiyo kuwa zaidi huku asilimia 80 wakiwa wanaume.

Je ni sababu gani zinazowafanya wanaume kuwa hatarini zaidi?

Wataalam wametoa sababu kadhaa ambazo zinaweza kuelezea tofauti hiyo kubwa, ikiwemo mfumo wa kinga kati ya wanaume na wanawake, tofauti ya homoni mwilini, maisha, na uwezekano wa wanaume kujiweka katika hatari nyingi.

Kwa mfano , wanaume wana uwezekano wa kuvuta sigara - huku asilimia 40 wakitumia bidhaa hiyo duniani ikilinganishwa na asilimia 9 ya wanawake , kulingana na shirika la afya duniani - suala linalowaweka katika hatari kubwa ya kukutwa na magonjwa ya mapafu.

Wanaume pia hunywa pombe nyingi na mara nyengine hukataa kwenda hospitali wakati wanapokuwa katika hali mbaya ya kiafya.

Wakati huohuo wanawake wana uwezo mkubwa wa kukabiliana na maambukizi ya virusi ikilinganishwa na wanaume

"Kuna kitu kuhusu mfumo wa kinga ya wanawake ambacho ni zaidi," Dk Janine Clayton, mkurugenzi wa Ofisi ya Utafiti juu ya Afya ya Wanawake katika Taasisi za Afya za kitaifa, aliambia New York Times.

Chanzo cha picha, WHO

Wanawake pia wana nafasi nzuri ya kinga kwa kumiliki kromosomu mbili za X , ambazo zinaweza kuchangia katika kuimarisha kinga miongoni mwao wanapokabiliana na maambukizi ya virusi .

"Baadhi ya sababu zizsizojulikana kwanini Covid-19 huenda ni hatari zaidi miongoni mwa wanaume zaidi ya wanawake ni kwamba ugonjwa wa moyo hupatikana sana miongoni mwa wanaume wenye umri mkubwa zaidi ya wanawake'', alisema Dkt Stephen Berger, mtaalam wa magonjwa ya maambukizi na mwanzilishi mwenza wa shirika la Global Infectious Diseases and Epidemiology Network (GIDEON).

Tafiti pia zimebaini kwamba shinikizo la juu la damu na magonjwa ya ini hupatikana sana miongoni mwa wanaume suala linalochangia vifo vya Covid-19.

Tatizo hilo limesababisha uzinduzi wa vipimo viwili nchini Marekani.

Katika vipino hivyo , wanasayansi wanawapatia wanaume walio na COVID-19 homoni za kike ili kuona iwapo zinaweza kuwasaidia kupona Covid-19.