Vurusi vya corona: Jinsi kampuni ya ndege ya Mahan Air nchini Iran ilivyokaidi marufuku na kusambaza corona mashariki ya kati.

Mahan Air plane
Maelezo ya picha,

Idhaa ya BBC Kiarabu imechunguza data ya usafiri ya kampuni ya Mahan Air na kuzungumza na vyanzo ndani ya kampuni hiyo kuonyesha kwamba kampuni hiyo ilikiuka sheria za marufuku zilizotolewa.

BBC imefanya uchunguzi kuhusu jinsi ndege moja ya kampuni ya Iran, kwa jina Mahan Air ilivyochangia katika usambazaji wa virusi vya corona katika eneo lote la mashariki ya kati, baada ya kuendelea na operesheni zake licha ya baadhi ya mataifa kupiga marufuku ndege za Iran.

BBC News imefanya uchunguzi wa data ya usafiri wa kampuni hiyo na kuzungumza na wafanyakazi wa kampuni hiyo ili kuonyesha jinsi kampuni hiyo ya ndege ilivyoendeleza operesheni za ndege zake zaidi ya mara 100 kati ya mwisho wa mwezi wa Januari na mwisho wa mwezi wa Machi kwa kuendesha ndege zake Iran, Iraq na maeneo ya milki za Kiarabu pamoja na Syria bila kujali.

Mataifa yote hayo yalidaiwa kuziruhusu ndege za kampuni hiyo kutua katika vuwanja vyake vya ndege licha ya kupiga marufuku ndege zao kutoka.

Iran iliahirisha safari zake zote za ndege kwenda na kutoka China tarehe 31 Januari, na baadhi ya mataifa nayo pia yalipiga marufuku ndege zinazotoka Iran mnamo mwezi wa Februari na Machi, baada ya kutangazwa kuwa kitovu cha mlipuko wa virusi vya corona katika eneo la mashariki ya kati.

Hatahivyo kampuni hiyo iliendelea na operesheni zake na kuzua madai kwamba huenda ilikuwa ikiweka maisha ya wafanyakazi wake hatarini.

Wafanyakazi wake walinyamazishwa - wakitishiwa kwamba wangechukualia hatua za kisheria walipolalamika kuhusu kusambaza virusi vya corona kwa wapendwa wao na taifa zima kwa jumla.

Kampuni ya ndege ya Mahan Air haijatoa tamko lolote kwa BBC ilipotakiwa kuelezea kisa hicho.

Je kampuni ya ndege ya Mahan Air ni ipi?

Chanzo cha picha, Rudi van Goch - Aviation Videography

Maelezo ya picha,

Kampuni ya ndege ya Mahan Air ina takriban ndege 55 na husafirisha abiria milioni 5 kwa mwaka kote duniani

Mahan Air ni kampuni ya ndege ya kibinafsi.

Kampuni hiyo imesema kwamba inamiliki takriban ndege 55 na husafirisha abiria milioni tano kwa mwaka hadi mataifa 66 kote duniani.

Ina uhusiano na tawi la jeshi kuu la Iran IRGC. Cha kushangaza ni kwamba kampuni hiyo ilikosolewa awali - Mwaka 2011 ,Marekani iliiwekea vikwazo , ikiituhumu kwa kusafirisha silaha na maafisa wakuu wa jeshi la IRGC.

Kampuni hiyo ya ndege inaunga mkono oparesheni za Iran nchini Syria, Lebanon, Syria na Iraq mataifa yote hayo yakiwa na ushirikiano na jeshi kuu la Iran IRGC.

Ushauri wa kiafya kupuuzwa

Chanzo cha picha, BBC Arabic

Maelezo ya picha,

Mahan Air ni shirika kubwa zaidi la ndege la Iran

Kwa kutumia mchanganyiko wa data za ndege na baada ya kuzungumza na vyanzo mjini Lebanon na Iraq, BBC News Arabic imefanikiwa kuthibitisha kwamba mgonjwa wa kwanza nchini Iran alisafiri kwa kutumia ndege ya Mahan Air .

Mnamo tarehe 19 mwezi February , mwanafunzi wa Iran alisafiri kwa kutumia ndege ya Mahan Air nambari ya usajili W55062 kutoka mji mkuu wa iran Tehran , hadi mji wa Iraq wa Najaf. Aliripotiwa kuwa mgonjwa wa kwanza rasmi wa virusi vya corona nchini Iran tarehe 24 mwezi Februari.

Tarehe 20 February , mwanamke mmoja kutoka Lebanon mwenye umri wa miaka 41 aliyekuwa akirudi kutoka haji akielekea Qom alisafiri kutoka Tehran kwa kutumia ndege ya kampuni ya namba na ya usajili W5112 kuelekea mji mkuu wa Lebanon Beirut.

Aliripotiwa kuwa mgonjwa wa kwanza nchini Lebanon siku iliofuatia. Licha ya visa hivyo kusababisha hasira kutoka mataifa yote hayo , Mahan Air iliendelea na operesheni zake. Serikali ya Iraq ilipiga marufuku ndege zinazoingia na kutoka nchini humo tarehe 20 mwezi Februari.

Hatahivyo BBC inaweza kubaini kwamba safari nyengine 15 za ndege zilifanyika baada ya marufuku hiyo kupitia ruhusa ya serikali ya Iran. Safari hizo za ndege zilikuwa zikibeba mahujaji kutoka Iran na kuwapelekea katika maeneo matakatifu nchini Iraq.

Katika taarifa kwa BBC , serikali ya Iraq ilisema kwamba hizo zilikuwa ndege za kuwarudisha makwao raia wa kigeni walio nchini humo kwa njia haramu na kwamba zilipata ruhusa kutoka mamlaka ya usafiri wa angani nchini Iraq.

Operational during China and Iran's peaks

Maelezo ya picha,

Mahan Air iliendelea kusafiri kati ya Iran na miji minne ya China yaBeijing, Shanghai, Guangzhou and Shenzhen

Uchunguzi huo wa BBC unaonyesha kwamba wakati wa kilele cha mlipuko wa virusi vya corona nchini China, ndege za kampuni ya Mahan zilikuwa zikisafiri kati ya Iran hadi katika miji mikuu minne ya China, ikiwemo Beijing, Shaghai, Guangzhou na Shenzhen.

Iran huenda iliiruhusu Mahan Air kukiuka marufuku yake ya usafiri ya kutoka na kuingia kutoka China iliowekwa tarehe 31 Januari.

Kampuni hiyo ya ndege pia ilichapisha picha katika katika mitandao ya China ikionyesha kwamba ndege zake sita kati ya mwisho wa mwezi wa Januari na tarehe 20 mwezi Aprili zilitumika kutoa misaada, na kuonyesha ndege nne zilizotumika kuwaondosha raia wa Iran nchini China huku safari za mwisho za ndge hizo zikifanyika tarehe 5 mwezi Februari.

Uchunguzi wetu ulibaini zaidi kwamba safari 157 za ndege zilifanyika baada ya siku hiyo licha ya Iran kupiga marufuku ndege zake kutoka na kuingia kutoka China.

Huku kampuni nyengine za ndege zikisitisha usafiri wa ndege zake , data ya usafiri ilionyesha kwamba tarehe 31 mwezi Januari hadi Aprili 20, kamapuni ya ndege ya Mahan Air ilikuwa ndio kampuni ya pekee ya ndege iliokuwa ikiendelea na safari zake kati ya Iran na China.

Kampuni hiyo pia ilikuwa na jukumu muhimu katika kuwasafirisha abiria nje ya Iran hadi mataifa mengine wakati taifa hilo lilipokuwa katika kilele cha maambukizi yake ya corona. Syria ilipiga marufuku rasmi safari za ndege za kwenda na kutoka Iran tarehe 8 Machi.

Hatahivyo, kampuni ya Mahan Air ilifanya safari nyengine nane za ndege baada ya marufuku hiyo kuwekwa. Kampuni hiyo pia ilifanya safari 37 kuelekea Dubai, safari 19 kuelekea Uturuki na safari nyengine 18 zaidi katika mataifa ikiwemo Malaysia na Thailand.

Kulikuwa na kampuni tofauti za ndege zilizokuwa zikisafiri kuelekea na kutoka Iran wakati huo. lakini kampuni ya ndege ya Mahan Air ndio iliokuwa kampuni iliokuwa ikifanya safari nyingi za ndege kwa kiwango kikubwa.

Wafanyakazi walitishiwa

Chanzo cha picha, BBC Arabic

Maelezo ya picha,

Wafanyakazi wa Mahan Air walinyamazishwa kwamba watafunguliwa mashtaka ya jinai iwapo wangezungumza kuhusu hofu yao.

BBC imepata ushaidi kwamba wafanyakazi walinyamazishwa kuhusu jukumu lote la kampuni hiyo ya ndege katika usambazaji wa virusi licha ya kwamba lilikuwa suala lililozua wasiwasi.

Kufikia mwisho wa Februari, zaidi ya wafanyakzi 50 wa kampuni ya Mahan Air walikuwa wakionyesha dalili za virusi vya Covid-19 kulingana na vyanzo muhimu katika kampuni hiyo.

Wafanyakzi wake walichapisha katika mitandao ya kijamii kwamba hawapewi mavazi ya kujilinda dhidi ya virusi hivyo. Tarehe 27 mwezi Februari, wafanyakazi wa kampuni hiyo walizungumza kwa mara ya kwanza.

Taarifa moja ilionekana katika gazeti la kila siku la Shargh kwamba wafanyakazi walipatiwa muda wa kujitenga baada ya kusafiri kutoka China.

Tarehe 18 Aprili , wafanyakazi 1300 wa Mahan Air walitia saini barua ya wazi wakiishutumu kampuni hiyo ya ndege kwa kupuuzilia mbali ugonjwa huo.

Wakichapisha kupitia chombo cha habari cha Avia, barua hiyo pia ilisema kwamba wito wa wafanyakazi hao wa kutaka vifaa vya kujilinda , vinavyopendekezwa na sekta ya Kimataifa ya usafiri wa angani pia ulipuuzwa .

Na kwamba walikuwa wanalaumiwa kwa kueneza maambukizi ya ugonjwa huo kwa wapendwa wao na taifa zima jumla.

BBC vilevile imepata nakala ya makubaliano yaliopatiwa wafanykazi wa Mahan Air , wakitishiwa kuchukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo zile za jinai iwapo watalalamika hadharani kuhusu matatizo yao.

Kampuni ya Mahan Air na mataifa mengine ambayo yaliruusu kampuni hiyo kutua katika viwanja vyao vya ndege licha ya kuweka marufuku yamekataa ombi la BBC kuzungumzia suala hilo.