Virusi vya corona: WHO yaidhinisha Kenya kufanyia majaribio chanjo ya Covid-19

Chanjo

Chanzo cha picha, Getty Images

Kenya imeungana na ulimwengu katika juhudi za kutafuta chanjo ya COVID-19 baada ya Shirika la Afya Duniani(WHO) kuidhinisha ombi lake la kushiriki katika majaribio ya pamoja ya kutafuta tiba ya virusi hatari vya corona.

Kundi la watafiti kutoka taifa hilo la Afrika Mashariki sasa linasubiri idhini ya mwisho kutoka kwa Baraza la Kenya la Sayansi na Teknolojia kabla ya kuanza mchakato wa kuwapata wagonjwa watakaoshirikishwa katika utafiti huo.

Endapo majaribio ya dawa hizo itaidhinsishwa, Wakenya ambao wamepatikana na virusi vya corona wataorodheshwa na kufanyiwa majaribio ya dawa aina nne ambazo zimeonesha matumaini ya kukabiliana na virusi hivyo.

Wanasayansi wa Kenya watafanyia majaribio dawa tatu ili kubaini ikiwa dawa hizo zinaweza kutibu ugonjwa huo.

Lakini Je dawa hizo ni zipi?

WHO lilichagua dawa nne ambazo ziolinesha ushahidi wa kutibu virusi baada ya uchunguzi wa maabara kuonesha inaweza kutibu wanyama kutokana na uchunguzi wa kimatibabu uliofanywa na wataalamu kutoka maeneo tofauti duniani. The drugs include; Remdesivir, an antiviral originally developed to treat Ebola, Lopinavir/Ritonavir which are licensed HIV drugs, , used to treat multiple sclerosis and Chloroquine, an anti-malarial drug.

Watafiti sasa wamepata idhini ya kufanyia majaribio ya dawa aina nne ikiwa ni pamoja na:

  • Remdesivir, ambayo ambaro awali ilitengenezwa kutibu Ebola
  • Dawa ya kutibu malaria ya hydroxychloroquine.
  • Lopinavir/ritonavir, ambayo pia imeidhinishwakuwatibu wagonjwa walio na virusi vya HIV.
  • Interferon beta-1a

Kufikia sasa hakuna tiba ya rasmi ya COVID-19 lakini maafisa wa afya kutoka sehemu tofauti duniania wana matumaini majaribio ya pamoja ya chanjo itasaidia kupatikana kwa chanjo haraka iwezekanavyo.

Zaidi ya nchi 35 barani Afrika zimeonesha nia ya kushiriki katika majaribio hayo lakini ni mataifa sita pekee yaliyopewa idhini

Kando na Kenya mataifa mengine yaliyopewa idhini ni pamoja na: Afrika Kusini, Misri, Zambia, Nigeria na Tunisia.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Remdesivir, ambayo iliidhinishwa na Marekani kama dawa ya dharura ya kutibu Covid-19.

Kenya imefika wapi katika majaribio hayo?

''Tuko katika awamu amabapo hatuwezi kubaini moja kwa moja nini kinafanya kazi'' anasema Dkt Loice Achieng Ombajo, ambaye ni mkuu wa kitengo cha magonjwa ya kuambukiza katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta.

Aliongeza kuwa katika majaribio ya tiba wagonjwa wengi wanashirikishwa bila mpangilio maalu lakini wote wanapewa dawa tofauti na wenzao.

''Kuna uwezekano wa dawa moja ikafanya kazi lakini wataalamu wanatakiwa kufuatilia kwa makini mienendo ya mgonjwa," alisema katika mahojiano na gazeti la Nation.

Kufikia sasa Dkt Ombajo, na wenzake wamepata idhini kutoka kwa kamati ya maadili ya Chuo Kikuu cha Nairobi na mapendekezo yao kuchunguzwa na bodi ya dawa nchini Kenya.

Watafiti hao kwa sasa wanasubiri tamko la mwisho kutoka kwa bodi hiyo na Baraza la kitaifa la Sayansi,Teknolojia na Ubunifu (NACOSTI).

Hatua nyingine muhimu kwa mujibu wa watalamu hao, ni kuhamasisha umma kuhusu majaribio hayo ya tiba kabla ya watu ''kufanya maamuzi'' ikiwa wanataka kushiriki katika zoezi.

Dkt Ombaja anasema kabla ya mtu kushiriki katika majaribio ya tiba wale wanaoendesha shughuli hiyo lazima watoe maelezo kwa muhusika.

''Kwanza anaambiwa huu ndio utafiti tunaofanya, hizi ndizo dawa tunazofanyia majaribio, Hii ndio sababu tunazifanyia majaribio, na hivi ndivyo tutakavyokulinda. Ukiwa mgonjwa tuna bima ambayo itakuhudumia. Je unakubali kusiriki?,Na endapo mhusika atakubali anapewa fomu ya kutoa idhini. Kisha tunafanya tunafanya majaribio. Ni mchakato mrefu," alisema Dkt Ombajo.

Wiki moja iliyopita Watafiti kutoka nchini Uingereza walisema wanafikiria kufanyia majaribio chanjo ya virusi vya corona nchini Kenya.

Tangazo hilo lilizua ghadhabu miongoni mwa Wakenya ambao walitumia mitandao ya kijamii kupinga hatua hiyo.

Shirika la Afya duniani pi ailiwahi kuyaonya mataifa ya Ulaya kwamba bara la Afrika sio uwanja wa majaribio ya chanjo.

Maelezo ya picha,

Mkuu wa shirika la Afya Duniani Dkt Tedros Adhanom Ghebreyes amesema kwamba bara la Afrika halitakuwa uwanja wa majaribio ya chanjo ya corona

Mkuu wa Shirika hilo Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus alilaani kauli alizoziita za "kibaguzi" kutoka kwa madaktari wawili wa Ufaransa ambao walitaka chanjo ya virusi vya corona kufanyiwa majaribio barani Afrika.

"Afrika sio na haitakuwa uwanja wa majaribio ya chanjo yoyote," alisema Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus.