Kanda ya Tyson akifanya mazoezi yazua mshawasha duniani

Zaidi ya miaka 33 baadaye, bondia huyo wa zamani alietia fora bado anaweza kujivunia kuwa mtu hatari zaidi duniani.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Zaidi ya miaka 33 baadaye, bondia huyo wa zamani alietia fora bado anaweza kujivunia kuwa mtu hatari zaidi duniani.

Katika mazungumzo ya wiki hii kuhusu ndondi , tunaangazia jinsi kanda ya video ya sekunde tano ya bingwa wa ndondi wa zamani Mike Tyson akipiga begi la mazoezi ya masumbwi ilivyozua hamu miongoni mwa mashabiki wa mchezo huo, waliotaka bingwa huyo kurudi ulingoni.

Tarehe 22 mwezi Novemba 1986 ndio siku ambayo Mike Iron Tysyon alikuwa na umri wa miaka 20 ambapo alishinda ubingwa wa ndondi katika uzani mzito zaidi duniani akiwa na umri wa miaka 20 na hivyobasi kutangazwa kuwa bondia mchanga zaidi wa uzani mzito kuwahi kushinda taji hilo baada ya kumshinda Trevor Berbick.

Zaidi ya miaka 33 baadaye, bondia huyo wa zamani alietia fora bado anaweza kujivunia kuwa mtu hatari zaidi duniani.

Tyson mwenye umri wa miaka 53 anathibitisha kwamba tabaka linaweza kudumu baada ya kuchapisha kanda yake ya video akifanya mazoezi ya kupiga begi na kufanya mazoezi ya ndondi.

Iwapo ulikosa kanda hiyo ya video hiki hapa kionjo chake ambacho huenda kikakupa hamu ya kutaka kumuona tena mkongwe huyo wa ndondi kwa kuangalia jinsi anavyopiga begi hilo la mazoezi kama bondia mchanga.

Kasi, nguvu na ukali: Ilikuwa video ya sekunde tano ambayo ilisambaa kwa kasi kote duniani.

Watu maarufu katika ndondi, na burudani walikuwa wa kwanza kutoa maoni yao.

Mwanamieleka aliyebadilika na kuwa muigizaji wa filamu kwa Jina Dwayne ama 'The Rock' Johnson alisema: Narudi katika mazoezi.

Nyota wa mchezo wa UFC Khabib Nurmagomedov alisema: Siwezi kuamini. hiki ni kiwango chengine.

Nyota wa filamu Will Smith alimuita ''shujaa wangu'' huku Mfalme wa Podcast Joe Rogan alitumia lugha tofauti kuonyesha furaha yake.

Chanzo cha picha, Twitter

Hivyobasi tunauliza swali ni kwa nini Tyson amekuwa akifanya mazoezi? Sio bure.

Katika chapisho la Instagram aliloshirika na msanii T.I , alifichua kwamba anapanga kurudi katika ulingo wa ndondi ili kuchangisha fedha za hisani.

''Nimekuwa nikifanya mazoezi katika kipindi cha wiki moja iliopita'', alisema Tyson.

Chanzo cha picha, Twitter

''Nataka kwenda katika mazoezi na kurudia hali yangu ya maungo ili kushiriki katika pigano la maonyesho la raundi tatu ama nne la hisani''.

Ukweli ni kwamba kila wakati bingwa wa zamani wa ndondi anaporudi ulingoni akiwa na umri wa miaka 50 sio wengi wangependelea uamuzi huo katika sekta ya ndondi, lakini wengi wameonekana kufurahia uamuzi wake.

Chanzo cha picha, Twitter