Kwa nini ncha ya kaskazini ya dunia inaelekea Urusi kutoka Canada?

Sumaku ya dunia iliopo ardhini hupatika katika msingi wa dunia

Chanzo cha picha, ESA

Maelezo ya picha,

Sumaku ya dunia iliopo ardhini hupatika katika msingi wa dunia

Kundi moja la wanasayansi wa Ulaya wanaamini wamegundua sababu inayosababisha kusongea kwa ncha ya kaskazini ya dunia (North Pole).

Ncha hiyo katika miaka ya hivi karibuni imekuwa ikisongea na kuelekea Siberia, na Urusi kutoka Canada.

Tukio hilo limefanyika kwa kasi hali ya kwamba imelazimisha sahihisho la mara kwa mara la mifumo ya urambazaji ya GPS, pamoja na ile inayotumia ramani ya simu zetu aina ya smartphones.

Mabadiliko hayo ya haraka na ambayo hayakutarajiwa katika sumaku ya dunia yamewafanya wanasayansi kushindwa kuyaelezea.

Kundi hilo linaloongozwa na wanasayansi wa chuo kikuu cha Leeds nchini England , linasema kwamba tabia hiyo inaelezewa na ushindani uliopo kati ya sumaku mbili zilizopo katika msingi wa dunia.

Mabadiliko katika mtiririko wa nyenzo zilizoyeyuka ndani ya sayari yamepunguza nguvu katika maeneo ya chini.

"Mabadiliko haya ya mtiririko yamedhoofisha ardhi iliyopo chini ya Canada na kuongeza nguvu chini ya ardhi ya Siberia," alielezea Dk Phil Livermore.

Hii ndio sababu ncha hiyo inayootesha eneo la kaskazini la duniani imeacha msimamo wake wa kihistoria kwenye Arctic ya Canada na kuvuka mstari wa tarehe ya kimataifa.

Eneo hilo la Kaskazini mwa Urusi linashinda mvutano uliopo, "aliiambia BBC.

Ncha tatu

Dunia ina ncha tatu katika eneo lake la juu.

Ncha ya kijiografia ndio eneo ambapo mhimili wa sayari ya mzunguko unakutana na ardhi.

Ncha ya geomagnetic ni eneo ambalo msimamo wake hubadilika kidogo.

Na baadaye kuna ncha ya kaskazini ambayo ndio ambayo imekuwa ikisongea polepole.

Alipoingundua kwa mara ya kwanza miaka ya 1830, mtafiti James Clark Ross alikuwa Nunuvut , eneo lisilojulikana kaskazini mashariki mwa Canada.

Wakati huo haikuwa mbali sana na wala haikuwa ikisongea kwa kasi ya juu

Lakini katika miaka ya 90 lilianza kusongea katika maeneo ya juu zaidi , na kuvuka mpaka wa tarehe ya kimatifa mwishoni mwa mwaka 2017.

Katika harakati hiyo liliweza kukaribia ncha ya kijiogrophia umbali wa kilomita chache.

Chanzo cha picha, Getty

Maelezo ya picha,

Mfumo wa sumaku duniani unaendelea kubadilika.

Mfumo wa awali haukufaa

Kwa kutumia data ya setlaiti wamefanikiwa kupima mfumo wa maadiliko ya mvuto wa dunia katika kipindi cha miaka 20 iliopita.

Miaka miwili iliopita , wakati walipowasilisha mawazo yao katika mkutano wa muungano wa wanajeografia mjini Washington, walipendekeza kwamba kunaweza kuwa na uhusiano wa eneo linaloyeyuka ambalo linasukuma ncha hiyo kuelekea upande wa magharibi kutoka msingi wa nje wa dunia.

Lakini mifano hiyo haikufaa kabisa, na kundi hilo sasa limesahihisha tathmini yao ili kuendana na mfumo wa mtiririko uliopo.

''Pia kuna tatizo la muda. Mtiririko huo ulianza kusogea mwaka 2000 huku ncha hiyo ikianza kusogea 1990''.

Chanzo cha picha, Getty

Maelezo ya picha,

Mifumo yote ya dira inatokana na mvuto wa dunia ardhini

Kusogea huko kutapungua

Kundi hilo linasema kwamba ncha hiyo itaendelea kuelekea upande wa taifa la Urusi , lakini itafikia muda ambapo itapunguza kasi yake .

Katika kasi ya juu imekuwa ikisonga kwa kati ya Kilomita hamsini hadi 60 kwa mwaka.

" Hakuna anayejua iwapo itarudi nyuma katika siku za usoni'' , mwanasayansi huyo wa Uingereza aliambia BBC.

Kasi hiyo ya ncha ililifanya shirika la data ya kijiographia nchini Marekani na masoroveya wa Uingereza kutoa habari za mapema kuhusu mfumo wa sumaku ya dunia mwaka jana.

Mfumo huu unawakilisha mvuto wa sumaku ya dunia na umewekwa katika kila chombo cha kuonyesha mwelekeo ikiwemo simu aina ya smartphone ili kuweza kurekebisha makosa yoyote ya dira.

Livermore na wenzake walitegemea sana data iliopatikana katika setlaiti kutoka shirila la masuala ya angani la bara Ulaya.

Kundi hilo limechapisha utafiti huo katika jarida la asli kuhusu sayansi ya ardhini.