Virusi vya Corona: Kuganda kwa damu, tatizo linalowakumba wagonjwa wengi walio katika hali mahututi lazua hofu

Wongonjwa wengi ambao wamekuwa na tatizo la damu kuganda katika mishipa wamekuwa wakitumia dawa za kujaribu kuyeyusha damu

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Wongonjwa wengi ambao wamekuwa na tatizo la damu kuganda katika mishipa wamekuwa wakitumia dawa za kujaribu kuyeyusha damu

Wangonjwa wengi ambao wamekuwa na tatizo la damu kuganda katika mishipa wamekuwa wakitumia dawa za kujaribu kuyeyusha damu hiyo na kufanya tatizo hilo lisilo la kawaida kuwa la kipekee.

Huku idadi ya wagonjwa waliopo na waliofariki ikiongezeka, madaktari wamegundua kwamba Covid-19, ugonjwa unaosababisha virusi vya corona ni ugonjwa usiofahamika kwa rahisi zaidi ya ilivyodhaniwa.

Ugonjwa huo unaweza kuathiri viungo kama vile ini, figo, utumbo, moyo na ubongo.

Tatizo kubwa lakini ni jinsi damu inavyoganda katika mishipa ya wagonjwa wanaopewa dawa za kufanya migando hiyo ya damu kuyeyuka.

Migando hiyo ya damu inaweza kufika katika viungo kama vile mapafu, moyo, ubongo na kusababisha mshtuko wa moyo unaoweza kusababisha kifo.

Siku chache zilizopita, madaktari katika hopsitali ya Mount Sinai mjini New York walichapisha utafiti unaosema kwamba mgando wa damu hususana katika mapafu unawaathiri vibaya wagonjwa wa Covid-19 walio mahututi.

Maelezo ya video,

Virusi vya corona: Je, Madagascar wamepata dawa ya mitishamba kutibu virusi vya corona?

Wataalamu hao pia walifichua kwamba migando hiyo ya damu inaweza kusababisha ugonjwa wa kiharusi miongoni mwa wagonjwa vijana walioambukizwa virusi vya corona.

Madaktari katika mataifa tofauti wameripoti tatizo sawa na hilo.

Uchanganuzi wa wagonjwa 183 wa Covid-19 uliofanywa na wanasayansi wa China umebaini kwamba asilimia 71 ya wale waliofariki walikuwa na mgando wa damu.

Nchini Uholanzi utafiti uliofanyiwa wagonjwa 184 waliokuwa wamelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi thuluthi moja ya wagonjwa hao walikuwa na mgando katika damu.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Coronavirus inaweza kuathiri sio tu mfumo wa kupumua lakini pia viungo vingine kama vile ini, figo, matumbo, moyo na ubongo

Nchini Marekani madaktari wengi wamesema kwamba migando hiyo ndio sababu kuu ya vifo miongoni mwa wagonjwa wa Covid 19.

Ijapokuwa migando ya damu sio tatizo lisilo kuwa la kawaida kwa wagonjwa walio katika hali mahututi, maafisa hao wa afya wameshangazwa na idadi ya wagonjwa wa Covid 19 walio na tatizo hilo.

Je tatizo hilo husababishwa na nini?

Bado hakuna uamuzi wa pamoja kuhusu sababu za migando hiyo ya damu katika mishipa . Kufikia sasa kuna uvumi chungu nzima , alisema Coopersmith mtaalam wa chumba cha wagonjwa mahututi na profesa wa chuo kikuu cha tiba cha Emory University School mjini Atlanta, USA, akizungumza na BBC Brazil.)

Anasema kwamba kuna sababu nyingi ambazo lazima ziweko kwa damu kuganda na mwili hushindwa kuamua kati ya kuvuja damu na kuganda kwa damu hiyo.

Haijulikani iwapo migando hiyo husababishwa na virusi vya corona ama kinga katika hali yake ya kukabiliana na Covid-19.

Wagonjwa wengi huwa wamelazwa hivyobasi inaongeza hatari ya damu kuganda.

Taarifa zaidi kuhusu virusi vya corona:

Haijulikani iwapo migando hiyo ya damu ni madhara ya kandokado ya mgonjwa ama iwapo migando hiyo inasababisha kufeli kwa viungo mwilini.

Kukatwa mguu, mshtuko wa moyo na kiarusi

Migando ya damu pia imeonekana miongoni mwa miili ya wagonjwa wengine.

Dkt.Gregory Piazza, mtaalamu wa magonjwa ya moyo mjini Birmingham na hospitali ya wanawake mjini Bostona pamoja na kuwa profesa katika chuo kikuu cha tiba cha Havard, anaammbia BC Brazil kwamba pia yeye alianza kugundua migando ya damu miongoni mwa wagonjwa waliokuwa katika cumba mahututi walio na virusi vya corona ambao walikuwa katika hali mbaya.

"Katika visa vingine tunagundua migando mikubwa katika mishipa ya damu iliopo karibu na moyo, alisema Piazza''.

"Inaweza kuwa katika mishipa ya kupeleka damu katika moyo na hivyobasi kusababisha mshtuko wa moyo au katika mkishipa inayopeleka damu katika ubongo na hivyobasi kusababisha kiarusi ama mara nyengine katika mishipa inayopeleka damu katika miguu na mikono na hivyo usababisha hatari ya mtu kukatwa mguu ama mkono''anasema.

Kisa kimoja kilichovutia watu nchini Marekani ni kile cha muigizaji Nick Cordero , 41 ambaye alilazwa hopsitalini mjini New York , aliambia BBC Brazil.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Damu kuganda kunaweza kusababisha matatizo kadha wa kadha kwa mgonjwa ikiwemo kifo

Wiki iliopita madaktari waliopo katika hospitali hiyo walitoa maelezo kuhusu wagonjwa watano wa virusi vya corona waliougua kiarusi.

Walikuwa kati ya umri wa miaka 33 hadi 49, na walikuwa na dalili chache ama hata bila ishara zozote za Covid-19.

Baadhi yao hawakujua kwamba wameambukizwa ama hata kubaini walikuwa na kiarusi, na hawakuulizia usaidizi kwa hofu ya kusababisha maambukizi hospitalini.

Kulingana na madaktari mgando wa damu katika miguu huonekana mara kwa mara miononi mwa wagonjwa wa Covid-19.

Baadhi ya hospitai zimekuwa zikitumia tiba ya kuyeyusha mgando wa damu katika mishipa kwa wagonjwa wote wanaougua Civid-19.

Lakini wataalama wanaonya kwamba tiba hiyo inahitaji makini kwa kuwa inaweza kuongeza hatari ya kuvuja damu na kusisitiza kwamba utafiti zaidi unahitajika.