Kenya, Somalia na Rwanda zakumbwa na mafuriko makubwa

Mwanamume akimbeba mwanamke ndani ya maji ya mafuriko

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Watu wamelazimika kuondoka katika nyumba zao baada ya mito kuvunja kingo

Mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha hivi karibuni katika mataifa ya Afrika mashariki imewaua watu 260.

Kuanzia Ethiopia , Uganda na Kenya, mito imevunja kingo zake na kusababisha mafuriko yaliyowalazimu maelfu ya watu kukimbia makazi yao.

Kenya ndio iliyoathiriwa zaidi na mafuriko hayo baada ya serikali kuthibitisha vifo vya watu 194.

Mataifa hayo ya Afrika mashariki pia yanakabiliwa na uvamizi wa nzige na mlipuko wa ungonjwa wa Covid-19.

Magharibi mwa Kenya huko Budalangi, wakazi wa eneo hilo iliwabidi wabebe mizigo yao kwa kutumia mitumbwi na bodaboda mara baada yam to Nzoia kufurika.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Mvua kubwa inatarajiwa kuendelea kunyesha kwa wiki kadhaa

Msemaji wa serikali, Cyrus Oguna aliandika kwenye kurasa yake ya Twitter wiki tatu zilizopita, kuwa mafuriko yalihamisha watu 100,000 na hali imekuwa ngumu zaidi kutokana na jitihada za kulinda watu kupata maambukizi ya virusi vya corona ambavyo vimeua watu 24 nchini humo.

Serikali imekuwa inatoa chakula na maji kwa watu waliopoteza makazi yao kutokana na mafuriko na wizara ya afya imetoa barakoa ikiwa ni hatua za kujikinga na maambukizi.

Mvua kubwa zimekuwa zinanyesha zaidi magharibi mwa Kenya na tayari watu 194 wamefariki kutokana na maruriko, waziri wa mahusiano ya serikali na mikoa alisema.

"Jana tu, tulipoteza watu 30 ndani ya saa 24," alisema Wamalwa.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Baadhi ya wakaazi Magharibi mwa Kenya wamelazimika kutafuta maeneo salama baada ya mto nzoia kuvunja kingo zake

Nchini Rwanda, watu 55 wamefariki huku mafuriko hayo pia yakiwaua watu 16 nchini Somalia.

Baadhi ya watu wamefariki kutokana na maporomoko ya ardhi katika maeneo ya milima ya kaskazini magharibu mwanchi hiyo.

Nyumba, barabara na mimea zote zimeharibiwa huku mamia ya watu wakiachwa bila makao, mameya wa wilaya zilizoathiriwa wameiambia BBC Idhaa ya Great Lakes.

Maelezo ya picha,

Hizi ni nyumba zilizoharibiwa na maporomoko ya udongo nchini Rwanda

Hali ikoje Uganda?

Nchini Uganda viwango vya maji vimeripotiwa kupanda na kusababisha wagonjwa 200 kukwama ndani ya hospitali.

Katika eneo la magharibi mwa nchi hiyo mto mmoja umevunja kingo zake na kusababisha watu kikimbilia maeneo salama katika mji wa riKasese.

Kwa sawa waokoaji wapo karibu na hospitali ya Kilembe, wakijaribu kuwafika wagonjwa waliokwama hapo na kuwapeleka katika kanisa lilipo karibu.

Njia kuu katika mji huo pia zimefungwa na maji.

Maelezo ya picha,

Baadhi ya watu karibu na ziwa Victoria wamelazimika kutafuta makazi ya muda

Mvua kubwa zimekuwa zinanyesha katika mataifa ya Afrika mashariki tangu mwishoni mwa mwaka jana na wataalamu wa hali ya hewa wameonya kuwa zinaendelea mpaka mwezi Mei