Virusi vya corona: Je ni viumbe gani wataishi binadamu watakapoangamia?

Dinosaurs walitawala dunia hadi walipoangamia zaidi ya miaka milioni 60 iliopita. Je ni nani atakayechukua mahala pao.

Chanzo cha picha, iStock

Maelezo ya picha,

Dinosaurs walitawala dunia hadi walipoangamia zaidi ya miaka milioni 60 iliopita. Je ni nani atakayechukua mahala pao.

Kutokanana matishio kama vile mabadiliko ya tabia nchi au janga la sasa la virusi vya corona, watu wengi zaidi na zaidi wanaonya kuwa uhai wetu uko hatarini.

Lakini nini kinaweza kutokea iwapo siku moja binadamu wataacha kuishi?

Inawezekana kabisa kuwa mwisho wa mwanadamu hauna maana kuwa mwisho wa dunia…dunia iliishi kwa kipindi cha mabilioni ya miaka kabla ya kuwepo binaadamu na hakika itaendelea kuishi muda mrefu zaidi bila sisi.

Zaidi wana mazingira wanasema kuwa bila uwepo wa binaadamu, kuna uwezekano mkubwa kuwa dunia itaendelea kuwepo kwa muda mrefu zaidi haijapata kutokea.

Lakini ulimwengu bila binaadamu unakuwaje? Aina gani nyingine ya viumbe ingetawala?

Hili ni swali ambalo msikilizaji wa kipindi cha BBC aliuliza, kipindi ambacho hujibu maswali ya kisayansi yanayoulizwa na wasikilizaji.

Kupata jibu kwa nadharia hii, wanasayansi Hannah Fry na Adam Rutherford, watangazaji wa kipindi , walimuuliza mwanabaiolojia wa wanyama Matthew Cobb.

Kwa mujibu wa Cobb kuna namna mbalimbali za kuelezea kuhusu viumbe watawala.

Chanzo cha picha, iStock

Maelezo ya picha,

Kuna wadudu wengi zaidi ya binadamu duniani hatua ambayo inamaana ya kuwez akuishi hata baada ya watu kuangamia

Moja pengine wadudu wadogo. Kwa wazo hilo Coob anazungumzia kuhusu wadudu ambao hii leo ndio wengi zaidi

Viumbe wadogowadogo

Hata hivyo, mtaalamu Kate Jones anasema kama tutapima kwa kutazama idadi, basi washindi ni wale viumbe wadogo sana.

''Ninafikiri viumbe wanaotawala wamekuwa na wataendelea kuwa pengine wakati wote vijidudu.'' Anasema.

Waliishi miaka mingi kabla yetu : karibu miaka bilioni 3.5 iliyopita (tumekuwepo miaka milioni 6 tu iliyopita)

Na tayari walishatutawala, kuanzia kwenye miili yetu kuna vijidudu vingi kuliko seli za mwanadamu!

Washindi

Lakini ikiwa tunazungumza kuhusu kutawala kwa njia ambayo viumbe vimeshinda au kuangamiza wengine, au mazingira yao, hakuna shaka kwamba wanadamu wamepata "nambari ya kwanza."

"Kimsingi popote tunapokwenda tunawaangamiza wanyama wakubwa - kuanzia mamalia na vifaru - na tunapozunguka dunia tunakokwenda wanapotea," anasema Cobb.

Chanzo cha picha, iStock

Maelezo ya picha,

Binadamu wameweza kutawala dunia lakini wamekuwa kwa madhara makubwa kwa sayari hii

Kwa kupotea kwa wanyama hawa, kazi yao kwenye mfumo wa ikolojia pia ulipotea, hivyo kuwasili kwetu kulibadilisha mfumo wa ikolojia wa dunia nzima,'' anaeleza.

Binadamu amefanikiwa sana katika ushindi huu wa maangamizi ambayo wanasayansi wengi wanaamini kuwa tuko kwenye njia ya kupotea kwa robo tatu ya viumbe vyote duniani.

Ikiwa hali hii itatokea viumbe gani wataishi?

Jibu linaweza kupatikana kwa kutathimini kilichotokea wakati viumbe walipoangamia nyakati hizo.

Mtaalam wa sayansi ya nyota Phil Plait, anasema kupotea kwa viumbe kulileta mabadiliko makubwa katika mazingira ya sayari.

"Kulikuwa na mabadiliko ya hali ya hewa ya ghafla, mabadiliko ya ghafla ya mazingira, mabadiliko katika kemia ya mchanga, mabadiliko ya joto la maji na hewa, na labda ndiyo yaliyosababisha kutoweka hivi."

Lakini kama vile maangamizi ya mwisho yalipoondoa dinosaur (dinosaurs ) mwishowe ikisababisha kuibuka na kutawala kwa mwanadamu, ni njia gani nyingine ya maisha ambayo inaweza kuchukua nafasi yetu ikiwa tutafutwa?

Chanzo cha picha, St. Martin's Griffin

Maelezo ya picha,

Kitabu 'baada ya mwanadamu': Kinazungumzia kuhusu kiumbe kitakachotawala baada ya binadamu kuangamia

''Ninafikiri kutakuwa na viumbe vitakavyorithi na hali mpya,'' anasema Kate Jones. ''kwa mfano kitu kinachoweza kula plastiki.''

Hatahivyo, suala hili ni gumu sana kukisia.

''Tunajua kutakuwa na vitu vyenya macho, mabawa, kutakuwa na wanaokula nyama, mimea na plastiki, lakini zaidi ya hapo sitaki kukisia moja kwa moja.'' Anasema.

Mwanasayansi mmoja anasema kuwa miaka 50 baada ya binaadamu kupotea, dunia itatawaliwa na viumbe wakubwa kama popo wenye miguu mitano.

Kama ina uhalisia au la, hatuwezi kuthibitisha kwa kuwa hatutakuwepo duniani.