Kim Jong-un: Kutoweka kwake, siasa ya kimataifa, malengo yake na jeshi la Korea Kaskazini

Vyombo vya habar vya habari vilimuona Kim akisherehekea kufuatia uzinduzi wa kombora la masafa marefu

Chanzo cha picha, KCNA

Maelezo ya picha,

Vyombo vya habar vya habari vilimuona Kim akisherehekea kufuatia uzinduzi wa kombora la masafa marefu

Katika siku za hivi karubuni kiongozi huyo wa Korea kaskazini alitoweka katika maeneo ya umma kwa siku 20 na kukosa sherehe za kuadhimisha siku ya kuzaliwa ya babu yake - ikiwa ni sherehe kubwa mwaka huu.

Baadhi ya vyombo vya habari vilisema kwamba alikuwa mgonjwa mahututi ama hata kufariki. lakini baadaye alionekana katika kiwanda kimoja cha mbolea. akiwa buheri wa afya.

Je majasusi wa Korea Kusini walisemaje?

Mkuu wa idara ya ujasusi nchini Korea Kusini Suh Hoon , alizungumza na kamati moja ya bunge siku ya Jumatano.

Alisema kwamba hakukuwepo na ishara kuhusu uvumi uliokuwa ukiendelea kwamba Kim jong un alikuwa na matatizo ya Kiafya , kulingana na chombo cha habari cha Korea Kusini Yonhap.

Kamati hiyo iliambiwa kwamba kiongozi huyo wa Korea Kaskazini ameonekana hadharani mara 17 mwaka huu. kufikia sasa mwaka huu atakuwa ameonakana mara hamsini.

Lakini hilo huenda lilisababishwa na mlipuko wa virusi vya corona , alisema mwanachama mmoja wa kamati - licha ya kwamba Korea kaskazini haina wagonjwa wowote waliotangazwa.

Lakini je kiongozi huyu ni mtu wa aina gani?

Kim jong-un alichukua uongozi wa taifa la Korea Kaskazini bila ujuzi wowote wa kisiasa na ule wa kijeshi.

Kim jong-il , babake , aliyekuwa kiongozi wa taifa hili alikuwa katika harakati za kumuandaa mrithi wake wakati alipofariki mwezi Disemba 2011.

Punde tu baada ya kifo cha babake, Kim aliyekuwa kijana mdogo aliungwa mkono kuwa mrithi wa babake. Alitangazwa kuwa kiongozi wa chama , taifa na serikali wiki moja baada ya kifo cha babake.

Tangu wakati huo , licha ya mazungumzo ya kihistoria na Marekani na hatua za kujaribu kuimarisha mahusiano na Korea Kusini ameonesha nia yake ya kuendeleza mpango wa Korea kaskazini kuimarisha silaha zake huku akifanya majaribio ya silaha za kinyuklia na makombora kadhaa.

Pia ameonyesha kwamba sio mtu mwenye huruma baada ya kumfungulia mashtaka mjombake na kudaiwa kutoa maagizo ya kumuua nduguye wa kambo.

'Mfalme mwenye nyota njema'

Kim Jong-un, ambaye ndie mwana wa mwisho wa kiume wa Kim Jong-il aliyemzaa na mkewe wa tatu ko Yong-hui alizaliwa 1983 ama 1984

Chanzo cha picha, Reuters

Hakadhuniwa kwamba alikuwa katika picha ya kumrithi babake. Wachanganuzi wa kisiasa hivyobasi walimlenga sana nduguye wa kambo Kim jong-nam na nduguye mkubwa Kim Jong-chol.

Hatahivyo kufurushwa kwa nduguye kutoka Japan mnamo mwezi Mei 2001 na nduguye wa katikati Kim jong-chol kuliimarisha fursa yake ya kumrithi nduguye.

Wachanganuzi waliomuona kuwa mrithi kamili wa babake baada ya kuzawadiwa nyadhfa kadhaa za kisiasa.

Akiwa msomi kutoka uswizi kama ndugu zake, Kim Jong-un alipuuzilia mbali ushawishi wa mataifa ya magharibi, akirudi nyumbani wakati ambapo hayupo shule na kujivinjari na balozi wa Korea Kaskazini wakati huo. Aliporudi nyumbani alidaiwa kujiunga na chuo kikuu cha kijeshi cha Kim II-sung.

Mamake alidaiwa kuwa mke aliyependwa sana na babake Kim Jong-un na alimsifu sana mwanawe akimuita 'Mfalme wa nyote njema ya alfajiri'.

Mnamo mwezi Agosti wakati kim Jong Un alitembelea China, ripoti moja ilisema kwamba Kim jong un aliandamana na babake safarini. Wakati huo alionekana pakubwa kuwa mrithi wake na wakati babake Kim Jong-il alipofariki hilo lilithibitishwa.

Kuimarisha jeshi la Korea kaskazini.

Hotuba ya kwanza kwa umma ya bwana Kim wakati Korea Kaskazini ilipokuwa ikiadhimisha miaka 100, ya siku ya kuzaliwa kwa mwanzilishi wa taifa hilo Kim II-sung tarehe 15 Aprili 2012, al

Aliunga mkono hatua ya kwanza ya kuliimarisha jeshi la taifa hilo akiapa kwamba wakati ambapo taifa hilo lilikuwa likitishiwa umekwisha kabisa.

Chanzo cha picha, AFP

Factory inspections are the mainstay of the North Korean leader's domestic media appearances

Under him, the development of North Korea's nuclear and missile programmes has continued and appears to have made rapid strides. Four more nuclear tests have taken place, bringing the regime's total to six.

Je majaribio ya makombora nchini Korea Kaskazini yamelipa ufanisi gani?

Pyongyang inasema kwamba imefanikiwa kufanyia majaribio bomu la hydrogen ambalo linaweza kuwekwa katika kombora la masafa marefu, lakini wataalam wanasalia kugawanyika kuhusu hatua zilizopigwa kuhusu mpango huo wa silaha.

Silaha za Korea Kaskazini zimefanikiwa kuweza kurushwa mbali. Mwaka 2017, utawala wake ulifanyia majaribio makombora kadhaa ambayo yangeweza kuruka hadi Marekani- hatua iliozua wasiwasi na uongozi wa rais Donald Trump na Umoja wa mataifa ukaimarisha vikwazo vyake dhidi ya taifa hilo.

Huku uhasama kati ya mataifa hayo mawili ukiongezeka, bwana Trump na Kim walirushiana cheche za maneno.

Bwana Trump alimuita kiongozi huyo wa Korea kaskazini, mtu wa roketi aliyekuwa katika harakati za kujilipua huku bwana Kim akimuita kiongozi huyo wa Marekani mtu mwenye 'akili punguani'.

Hatahivyo kinyume na matarajio ya wengi, Bwana Kim alitoa mkono wa amani kwa Korea Kusini katika hotuba yake ya mwaka mpya akisema yuko tayari kwa mazungumzo na kwamba alikuwa tayari kutuma ujumbe mnamo mwezi Februari 2018 wakati wa michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi nchini Korea Kusini.

Baadaye mikutano kadhaa ya kidiplomasia ilifuatia huku mataifa hayo ya Korea yakishirikiana katika michezo hiyo ya Olimpiki kwa mara ya kwanza yakitumia bendera moja wakati wa sherehe ya ufunguzi wa michezo hiyo.

Bwana Kim pia alifanya ziara yake ya kwanza nje ya Korea Kaskazini akitumia huduma ya treni kusafiri hadi Beijing .China ndio mwandani wa karibu wa Korea Kaskzini na mshiriki wake mkubwa wa kibiashara.

Bwana Kim pia alitaka kuimarisha uhusiano wake na rais Trump na mnamo mwezi Aprili 2018, viongozi hao wawili walifanya mikutano ya ana kwa ana ya kihistoria nchini Singapore iliolenga kulishawishi taifa lake kuwacha utenegenezaji wa silaha za kinyuklia.

Bwana Kim Baadaye alisema kwamba ameahirisha utengenezaji wote wa silaha za kinyuklia na majaribio yote ya silaha kwasababu tayari taifa lake lilikuwa limejiimarisha kinyuklia.

Ijapokuwa usitishaji huo wa mpango wake wa silaha uliungwa mkono kimataifa, wachunguzi walisema kwamba Pyongyang haikuahidi kuangamiza silaha ilizonazo, na kwamba awali ilikuwa imekaidi ahadi ya kusitisha utenegenezaji wa silaha za kinyuklia.

Mwaka uliofuatia , viongozi hao wawili, walijiunga na rais wa Korea Kusini Moon Jae-in , na kukutana katika mkutano usio wa kawaida katika eneo linalolindwa sana kati ya mpaka wa mataifa hayo mawili ya Korea DMZ.

Hatahivyo, uhusiano kati ya Marekani na Korea Kaskazini ulizorota , na mazungumzo kukwama baada ya rais Trump kukataa kuondoa vikwazo hadi pale Pyongyang itakapositisha kabisa mpango wake wa kinyuklia.

Baadaye mwezi Januari 2020, bwana Kim alisema kwamba alikuwa anaendeleza mipango ya kufanyia majaribio silaha zake za masafa marefu ilioahirishwa wakati wa mazungumzo na rais Trump na kutishia kwamba ulimwengu utashuhudia silaha mpya ya kimkakati.

Chanzo cha picha, KCNA

Maelezo ya picha,

Kim jong un akikikagua kiwanda kimoja nchini humo

Nyumbani , bwana Kim amekuwa akifuta mawaziri wake wa ulinzi kwa mfululizo - ikiwa amefuta takriban mawaziri sita tangu 2011- na kuonekana na wachanganuzi kama ishara kwamba hana imani na utiifu wa jeshi la taifa hilo.

Na ishara kwamba kulikuwa na vita vya madaraka katika serikali yake miongoni mwa maafisa wakuu ilionekana mwezi Disemba 2013, wakati Kim Jong-un aliagiza mauaji ya mjombake Chang Song -Thaek. Vyombo vya habari vya serikali vilisema kwamba alikuwa anapanga njama ya mapinduzi.

Bwana Kim pia anaaminika kuagiza mauaji ya babake wa kambo aliyekuwa mafichoni, Kim Jong-nam Februari 2017 katika uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur.

Maisha ya bwana Kim ya kibinafsi hayakuwa na umaarufu mkubwa hadi pale kanda ya video ya runinga ilipoonyesha mwanamke asiyejulikana akishiriki katika hafla naye ilipoonekana. Julai 2012, vyombo vya habari bwana KIm alikuwa anafunga ndoa na ''rafikiye Ri Sol-ju".

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Rais Trump akiandamana na bwana Kim kushoto na mwenzake wa Korea Kusini Moon-Jae -in

Bi Ri hana umaarufu wowote , lakini mavazi aliovalia yaliwafanya wachanganuzi kusema kwamba alikuwa anatoka katika familia ya haiba ya juu. Ripoti pia zimesema kwamba bi Ri huenda alikuwa mwimbaji ambaye alimvutia bwana Kim wakati wa maonyesho. Kulingana na majasausi wa Korea kusini wawili hao wana watoto watatu.

Dadake Kim, Kim Yo-Jong , ana wadhfa wa juu katika chama cha wafanyakazi wa Korea - analijipatia umaarufu wakati alipomwakilisha nduguye katika michezo ya majiri ya baridi nchini Korea Kusini Haijulikani iwapo nduguye mkubwa Kim Jong chol ana wadhfa wowote katika serikali.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Bwana Kim na bi Ri wanadaiwa kuwa na watoto watatu

Kim Jong un hakufanyiwa upasuaji wa moyo

Idara ya ujasusi nchini Korea Kusini imesema uvumi kuhusu afya ya Kim Jong un ulikuwa hauna msingi na kwamba hakuna ishara kwamba alifanyiwa upasujai wa moyo.