Virusi vya corona: Unyanyasaji wa wenza majumbani

  • Azeezat Olaoluwa, George Wafula
  • BBC
Picha ya mwanaume akimfokea mwanamke ambaye anasoma kitabu bila kumjibu

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Picha ya mwanaume akimfokea mwanamke ambaye anasoma kitabu bila kumjibu

Umoja wa Mataifa umeeleza kuwa vitendo vya unyanyasaji dhidi ya wanawake wakati wa marufuku ya kutotoka nje ni kama ''kivuli cha janga''. Barani Afrika, serikali, polisi na wanaharakati wameripoti ongezeko la vitendo vya mashambulizi dhidi ya wanawake na wasichana ambao wako ndani na wapenzi wao au walezi wao ambao ni wanyanyasaji.

Hivyo utafanya nini ikiwa utajikuta kwenye hali hii? Tuliwauliza wataalamu na waliopitia vitendo vya unyanyasaji kutoa ushauri wao.

''Unapokuwa kwenye mahusiano yenye manyanyaso, unapata viashiria,'' Esther ananiambia, akikumbuka miaka mitatu nyuma aliyokuwa kwenye ndoa na mwanaume ambaye Esther anasema alikuwa akimdhalilisha kwa kumpiga na kwa maneno.

''Mwishoni mwa juma huwa ni mbaya zaidi kuwa kuwa kila mtu yuko nyumbani. Mwenzi wako anakuwa na muda mwingi hivyo wanakuwa wamechoka. Hivyo unaona kuwa wanatafuta sababu ya ugomvi. Wanakuchokoza- wanasema mambo ambayo yatakukasirisha kisha wanakupiga kwa kuwa umejibu.

''Ikiwa siku mbili zinaweza kumchosha mtu na kumfanya atake kukupiga, fikiria hali inakuwa vipi kwa mwezi mmoja wa kukaa ndani ulivyo waathiri watu, si kwa kuchoka wakati huu, ni msongo wa mawazo, ni hofu.''

Maelezo ya picha,

Esther says women in abusive relationships usually observe a pattern to the abuse

Ni miaka kadhaa sasa tangu Esther aachane na mumewe. Na ingawa wakati huo ilikuwa rahisi kuondoka kuliko wakati huu, bado ilichukua muda na ujasiri.

''Nilijihisi nilikuwa gerezani na sikuweza kwa kuwa nilikuwa vibaya kiuchumi, kisaikolojia, ilikuwa ngumu sana- na pia kulikuwa na watoto wangu. Pia mama yako ana furaha kuwa umeolewa, hivyo unafiria kuendelea kukaa kunamuweka katika hali ya furaha. Usiondoke.''

Kwa wanawake wanaotaka kuwaacha wapenzi wao wakati wa huu wa kukaa ndani, changamoto ni kubwa zaidi. Ikiwa wanajaribu kuondoka, wanaweza kupata changamoto ya kushikwa na polisi kwa makosa ya kuvunja sheria ya kukaa ndani na pia wanaweza kupata shida ya usafiri wa Umma.

Nchi nyingi zimeweka nambari za msaada kwa ajili ya waathirika. Uhitaji wa huduma hiyo umekuwa mkubwa.

'Ongezeko kubwa la vitendo vya unyanyasaji'

Wakati wa wiki ya kwanza ya marufuku ya kutotoka nje nchini Afrika Kusini, polisi walipokea ripoti 2,320 za unyanyasaji kijinsia, idadi kubwa kwa 37% zaidi ya kawaida.

Nchini Zimbabwe, mtandao wa kutoa msaada ulisema kuwa idadi ya ripoti kuhusu vitendo hivyo ni kubwa mara tatu zaidi, wakati wakili wa masuala ya jinsia nchini Nigeria, Dorothy Njemanze, aliiambia BBC kuwa alikuwa na hofu kuhusu ongezeko la vitendo vya udhalilishaji nchini mwake: ''Tuna hofu kuwa iwapo hali hii itaendelea hivi, tutarekodi vifo kabla ya marufuku ya kutoka nje haijakamilika.''

Baadhi ya nchi za kiafrika zinachukua hatua za kuwasaidia wanawake. Nchini Tunisia, ambako kumeshuhudiwa ripoti za ongezeko la vitendo vya unyanyasaji majumbani, serikali imeweka mtandao wa msaada na kufanikiwa kusaidia kutoa msaada wa malazi kwa waathirika wanane na watoto wao.

Maelezo ya picha,

Baadhi ya serikali za kiafrika zimetoa namba za misaada kwa ajili ya wanawake waathirika wa unyanyasaji

Kwingineko, makazi yamewekwa wazi na watu wengine wamejitolea kuwasaidia wanawake kuondoka kwenye nyumba zenye madhila hayo.

Nchini Zimbabwe, hifadhi moja iitwayo Roots One Stop inawatunza wanawake 21 na watotot saba. Mkurugenzi wake Beatrice Savadye, amesema waliweza kuwaokoa wanawake hao kutoka majumbani mwao na walikuwa watolewa polisi.

'Nyumba salama kwa wanawake'

Nchini Kenya, afisa wa ustawi wa jamii Dianah Kamande anasema makazi yameweza kuwahifadhi wanawake na kuwa taasisi yake imewaokoa wanawake 17 jijini Nairobi pekee.

Nchini Nigeria, ingawa makazi mengi ya wanawake yamefungwa kipind hiki, watu wanaojitolea bado wameweza kuwasaidia wanawake kutoroka na kwenda kuishi kwa ndugu zao, anasema Titilayo Vivour, mratibu wa timu ya kupambana na vitendo vya unyanyasaji wa majumbani na kingono.

Lakini nyumba inayotoa msaada wa makazi kwa wanawake nchini Ghana, Ark, Picha inayoonesha watu wakiwa wananyoosha mikono kwa mwanamke aliye kwenye kifungo, mkurugenzi wake Nasa Sunnu amesema kuwa walishindwa kuwapata wateja wapya kwa sababu ya hatari ya maambukizi na ukosefu wa vifaa vinavyohitajika wakati wa karantini.

Esther ambaye alinusurika kwenye ndoa iliyokuwa na unyanyasaji na sasa anafanya kazi na wenzake walionusurika, amesema wanawake wanapaswa kupiga simu ya msaada hata kama nyumba za msaada wa malazi zimefungwa

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Picha ya mwanaume akimfokea mwanamke ambaye anasoma kitabu bila kumjibu

Tunajaribu kuishi

Jumuiya zinapaswa kuwatazama kwa karibu majirani ambao wanafikiri kuwa wanaweza kukabiliwa na vitendo vya unyanyasaji, anasema mwanasaikolojia Nthabiseng Ramothwala. Pia anashauri wanawake kutafuta msaada kutoka kwa watu wanaowazunguka.

''Fahamu maafisa polisi na namba za dharura ambazo unaweza kuzipiga,'' aliiambia BBC.

Na kwa wale ambao hawawezi kutoroka, Esther ana ushauri wa mwisho.

''Ukiwa kwenye hali hii, kama wataongea jambo la kukuumiza, wapuuze. Kama watakuchokoza, nenda kasome kitabu au fanya kitu kingine ambacho kitakuondolea mawazo.

''Ikiwa unaweza kuishi kwa mwezi mmoja, miwili au mitatu...kisha fanya unachotaka kufanya. Sijui kama tunaweza kuita hatua hii kuwa suluhu. Ni hatua za muda mfupi tu.

''Kwa sasa tunajaribu kuishi, hivyo sema wanachotaka kusikia, fanya wanachotaka ufanye. Ili tu uweze kuondokana na hali hii.''