Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 13.05.2020: Bale, Ndombele, Sancho, Ighalo, Pogba, Messi

mshambuliaji wa Real Madrid forward Gareth Bale

Newcastle wako tayari kutumia £53m kumpata mshambuliaji wa Real Madrid, Gareth Bale, 30, mpango ambao ukifanikiwa utamrejesha ntota huyo katika ligi kuu ya England msimu huu. (Daily Mail)

Tottenham haitakubali Tanguy Ndombele, 23, kuondoka klabu hiyo msimu huu. Kiungo huyo wa kati wa Mfaransa amehusishwa na tetesi za kujiunga na Barcelona na Liverpool. (Independent)

Dejan Lovren anakaribia kuondoka Liverpool, huku Roma ikitarajiwa kuwasilisha ofa ya kumnunua beki huyo wa Croatia wa miaka 30. (Gazzetta dello Sport, via Liverpool Echo)

Liverpool imeungana na miamba wengine wa Ulaya kumsaka kiungo wa kati wa Red Bull Salzburg na Hungary Dominik Szoboszlai,19. (Tuttosport, via Daily Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images

Manchester United wanataka kuwasajili wachezaji watatu wa Uingereza msimu huu akiwamo- mshambuliaji wa Borussia Dortmund Jadon Sancho, 20, kiungo wa kati wa Aston Villa Jack Grealish, 24, na kiungo wa kati wa Birmingham wa miaka 16, Jude Bellingham. (Daily Star)

Hata hivyo huenda, mshambuliaji Odion Ighalo, 30, akacheza mechi yake ya mwisho Manchester United maada y amazungumzo ya kurefusha makataba wa mkopo wa kiungo huyo wa kimataifa wa Nigeria kutoka Shanghai Shenhua nchini China kugonga mwamba. (Standard)

Chanzo cha picha, Getty Images

Juventus wamekuwa klabu ya kwanza ya Italia kuweka kanuni ya mshahara kwa wachezaji wake, hatua ambayo imewafanya kujiondoa katika kinyang'anyiro cha kumnunua kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba,27 . (Daily Mail)

Lionel Messi, 32, na baadhi ya wachezaji wenzake nchini Uhispania huenda wakapunguziwa mshahara kwa asilimia 30 msimu ujao huku Barcelona na Real Madrid wakitathmini hatua ya kupunguza marupurupu ya wachezaji kutokana na athari iliyosababishwa na virusi vya corona. (Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images

Chelsea wana uhakika wa kumsajili kiungo wa Manchester United, Angel Gomes mwenye umri wa miaka 19. (Mirror)

West Brom itachuana na Tottenham kumsajili mshambuliaji wa Fenerbahce na Kosovo Vedat Muriqi, 26, mwenye thamani ya £uro milioni 18 iwapo atafanikiwa kupanda daraja. (Aksam, via Birmingham Mail)

Crystal Palace inamtaka bosi wa Burnley Sean Dyche kuwa meneja wao. (Mirror)