Virusi vya corona: Je ni kwanini Idadi ya watu walioambukizwa virusi Uganda inapunguzwa?

Waziri wa Afya wa Uganda Jane Aceng amepunguza idadi ya maambukizi ya virusi vya corona Uganda

Chanzo cha picha, Dr. Jane Aceng/Twitter

Maelezo ya picha,

Waziri wa Afya wa Uganda Jane Aceng amepunguza idadi ya maambukizi ya virusi vya corona Uganda

Waziri wa afya nchini Uganda amerudisha nyuma namba za idadi ya watu waliopata maambukizi ya corona nchini Uganda baada ya rais Yoweri Museveni kutoa agizo kuondoa idadi ya madereva wote wageni katika orodha ya wagonjwa wa corona nchini Uganda.

Siku ya Jumatano, taifa hilo lilidhibitisha kuwa na visa vya corona 260 kwa mujibu wa shirika la afya duniani, lakini waziri anasema idadi ya watu waliopata virusi vya corona nchini humo mpaka sasa ni 145.

Jane Aceng alisema kama wakihesabu idadi ya madereva wote wa maroli ambao ni wageni nchini humo, idadi itafikia hapo, aliandika katika kurasa yake ya tweeter:

Chanzo cha picha, Dr.Jane Achieng/Twitter

Mei 20, 2020, visa vipya 10 vya ugonjwa wa corona vimedhibitishwa wakati tisa kati yao ni madereva wa roli huku mmoja akiwa mtu ambaye aliambukizwa .

Kufuatia maelekezo ya rais, kama tukiondoa idadi ya madereva hao , basi Uganda itakuwa na visa 145.

Waziri amesema ameondoa idadi ya madereva wageni 124, lakini hakutaja uraia wa madereva hao wageni waliokutwa na corona.

Hatua za kudhibiti corona miongoni mwa madereva

Aprili 29, Rais Museveni alitangaza hatua mpya za kudhibiti mienendo ya madereva wa malori yanayoingia nchini humo kutoka mataifa jirani baada ya zaidi ya madereva 20 kupatikana na ugonjwa wa Covid-19.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mwezi Aprili, Rais Museveni alitangaza hatua mpya za kudhibiti mienendo ya madereva wa malori yanayoingia Uganda kutoka mataifa jirani

Mataifa ya Uganda na Kenya yamekuwa yakiwafanyia vipimo wa virusi vya corona madereva wa malori katika mipaka yao hali ambayo imesababisha foleni ndefu ya magari hayo.

Madereva na wasaidizi wao upande wa Kenya wamelalamikia jinsi walivyosubiri kwa siku kadhaa kufanyiwa vipimo vya Covid-19 kabla ya kuruhusiwa kuvuka mpaka wa kuingia Uganda.

Njia ya usafirishaji mizigo kutoka bandari ya Mombasa nchini Kenya ni muhimu sana katika usafirishaji wa bidhaa muhimu kama vile chakula na dawa hadi Uganda, Rwanda, Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemocrasia ya Congo.

Lakini wasafirishaji wa mizigo hiyo sasa wanahofiwa huenda wakaeneza virusi vya corona katika kanda ya Afrika Mashariki.

Sasa Rais Museveni anasema hatua zaidi zitachukuliwa kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona.

Taarifa zaidi kuhusu virusi vya corona:

Hatua hizo ni pamoja na kila lori kuwa na mtu mmoja - dereva pekee yake ambaye hataruhusiwa kulala hotelini wala nyumbani kwa watu.

Katikati ya mwezi April, gumzo liliibuka mtandaoni kwa sababu serikali ya Uganda ilikuwa inamtafuta raia wa kigeni aliyepatikana na ugonjwa wa corona nchini humo kurudi kwao.

Waziri wa Afya Ruth Jane Aceng alisema kuwa mataifa wanachama wa Muungano wa Afrika Mashariki yalikubaliana kila raia wa nchi hizo ambaye atakayepatika na virusi vya ugonjwa wa corona atarejeshwa nyumbani kwa matibabu.

Unaweza pia kutazama:

Maelezo ya video,

Coronavirus: Utajuaje kuwa umeathirika na virusi?