Virusi vya corona: Huenda Afrika iliyachelewesha maambukizi lakini haikuyadhibiti

Mwandamanaji nchini Afrika Kusini ambaye amekasirishwa na amri ya kutotoka nje - 20 Mei 2020 Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mwandamanaji nchini Afrika Kusini ambaye amekasirishwa na amri ya kutotoka nje

Nilitumia wakati wangu mwingi kuwafuatilia baadhi ya maafisa wa polisi wa Afrika Kuisni wakati wakipiga doria katika barabara nyembamba na zenye giza za mji wa Alexandria kandokando ya mji wa Johannesburg.

Lilikuwa tukio lisilo la kawaida kwakweli. Kila dakika maafisa wa polisi walisimamisha gari lao, kuruka nje na watu walio karibu yao walianza kupiga kelele na kutoroka - kuanza kuwafukuza raia kiholela kabla ya kuwakamata baadhi yao na kuwaingiza katika gari hilo.

Mwanmke mmoja alikuwa hakuvaa barakoa, afisa mmoja alielezea.

Mwengine alikuwa akiuza sigara bandia , na wengine wengi wakiwa wamesimama karibu ila kuheshimu masharti mapya ya kiafya ijapokuwa haikuwa rahisi kubanini.

Kukosa imani na serikali

Utaratibu wote ulikuwa na ubishi na wa kutisha - dhulma za wazi za mamlaka.

Lakini tangu siku hizo nimekuwa nikikumbuka usiku huo mjini Alexandria kwa njia tofauti , kufikiria kuhusu tabia ya maafisa wa polisi na jinsi raia walivyofanya baada ya kuwaona maafisa hao . Kutoroka.

Na wanapokamatwa wanalazimika kukubali makosa yao kwa haraka.

Nadhani, dhihirisho la wazi kabisa la mazingira magumui - tabia ya watu ambao wanahisi, hawana nguvu ya kupingana na serikali.

Nimeona tabia hiyo mara kwa mara kote hapa Afrika Kusini na maeneo mengine ya bara hili.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Jeshi la Afrika Kusini limetwa kuashinikiza sheria kali za kutotoka nje

Mambo kama hayo hutokea katika hospitali pia.

Nimesikia - mara ya kwanza na ya pili - juu ya watu ambao jamaa zao walilazwa katika hospitali za umma na "maumivu ya tumbo" au "baridi tu" na ambao walitangazwa ghafla kwamba wamekufa ndani ya siku.

Inanigonga kwamba kuna hali ya mazingira magumu - sio ya kipekee Afrika, kwa kweli - imeonyesha jinsi bara hili linavyokabiliana na janga hili pia.

Ni kweli kwamba kulikuwa na mazungumzo mengi katika siku za kwanza kuhusu Afrika pengine isiathirike - na bado tunasikia viongozi kama vile rais wa Tanzania John Pombe Magufuli akijaribu kupuuza athari za ugonjwa huo.

Lakini watu wngi niliozungumza nao , hususan wale watu maskini wameonyesha wasiwasi na kutafuta njia za kujilinda wao wenyewe na familia zao - na muhimu sio kutegemea serikali kuwafanyia.

Mafikra kama hayo ya kiongozi kamaa huyo pia yanatumiwa na serikali nyingi za Afrika.

Afrika ilichukua uamuzi wa haraka na wa busara

Hatahivyo ni bara lenye magonjwa kama vile kifua kikuu. Virusi vya ukimwi, malaria na kuharisha pia kunaweza kuua - licha ya kuimarika kwa mfumo wa afya ya umma.

Patients lie under mosquito nets in a health facility in Uganda
GETTY IMAGES
Six main causes of death in Africa

  • 1) Lower respiratory infections (10.4% of deaths):916,851

  • 2) HIV/Aids (8.1%):718,800

  • 3) Diarrhoeal diseases (7.4%):652,791

  • 4) Ischaemic heart disease (5.8%):511,916

  • 5) Malaria (4.6%)408,125

  • 6) TB (4.6%):405,496

Source: WHO - figures from 2016

Hivyobasi serikali nyingi zimejiandaa kukabiliana na changamoto mpya ya afya ya umma kama vile Ebola ama Covid-19.

Hiyo ndio maana hazikubabaika katika awamu za mapema za ugonjws huo.

Huku mataifa mengine yakijaribu kuimarisha kukabiliana na ugonjwa huo , na kuweka wazi viwanja vyao vya ndege na kuwataka raia wao kutokwenda katika baa, mataifa ya Afrika, yalikuwa katika harakati za kuidhinisha sheria za raia kutotoka nje na kuwafunza maafisa wao wa afya jinsi ya kukabiliana na wagonjwa wa virusi hivyo.

Ilichelewesha lakini haikuyathibiti maabukizi

Lakini swali ni- kwa taifa kama Afrika Kusini na bara zima la Afrika - ni iwapo mazingira hayo magumu yanaweza kuendelea kukabiliana na jinamizi hilo kwasababu ushahidi kutoka kwa Nigeria na Sudan Kusini unaonesha mikakati ya mapema ya Afrika huenda ilichelewesha maambukizi hayo lakini sio kuyadhibiti.

Utabiri wa wataalam kutoka timu moja mji Johannesburg unaonesha kwamba virusi hivyo - licha ya kupunguzwa makali ya maambukizi- bado vitawaua zaidi ya raia 40,000 wa Afrika kusini na huenda maambukizi yakafikia kilele chake nusu ya pili ya mwezi Julai.

Wakati huohuo uharibifu mbaya wa uchumi uliosababishwa na amri za mapema za kutotoka nje unaanza kupima subra na uchumi wa jamii na serikali ambazo hazina fedha za kutosha ikilinganishwa na mataifa ya Ulaya.

Baadhi ya maamuzi magumu na makabiliano dhidi ya ugonjwa huo yako mbele . Hii haimaanishi kwamba litakuwa janga Afrika.

A coronavirus billboard in Lagos, Nigeria - pictured in April 2020
AFP
The continent's early response - fuelled by a well-honed sense of vulnerability - has been world-class"
Andrew Harding
Africa correspondent, BBC News

Ulimwengu pengine umejisahau na hata mara nyengine kuchukua muda mwingi kufikiria kwamba bara hili huenda likaathirika polepole lakini vibaya zaidi na maambukizi yake kuyapiku mataifa yoye duniani , ama iwapo chanjo zake za TB , idadi kubwa ya vijana eneo ambalo kuna jua la kutosha huenda likatoa miujiza.

Ukweli ni kwamba Afrika inajiandaa kuishi na ugonjwa mwengine mbaya zaidi.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Afrika imeanza kuasisi maisha ya kuishi na virusi vya corona kama waumini hawa wa Kiislamu nchini Senegal

Kama sehemu zingine duniani, itapambana, na mwishowe itashinda, au angalau kuishi na virusi hivyo kwa muda mrefu .

Mwitikio wa mapema wa bara - uliochochewa na hisia nzuri ya mazingira magumu - umekuwa wa kiwango cha juu.

Lakini mifumo yake ya huduma ya afya imedhoofishwa, wengi wanaweza kusema, sio tu kwa umaskini na ufisadi, lakini kwa mfumo wa kuwachukua wahudumu wa matibabu wa Kiafrika kwa mataifa ya Magharibi kwa miongo kadhaa.