Bibi aagizwa na mahakama kufuta picha za wajukuu Facebook kwa kukosa kuomba idhini

A woman on a smartphone Haki miliki ya picha Getty Images

Mwanamke mmoja amelazimika kufuta picha za wajukuu zake alizoziweka kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook na Pinterest bila ya idhini yao, mahakama moja nchini uholanzi imesema.

Suala hilo limefika mahakamani baada ya mama huyo kutofautiana na bintiye.

Hakimu alitoa uamuzi kwa kuzingatia kanuni ya udhibiti wa data ya Umoja wa Ulaya.

Mtaalamu mmoja amesema uamuzi huo uliangazia msimamo wa mahakama ya Ulaya wa miaka mingi.

Kesi hiyo iliwasilishwa mahakamani baada ya mwanamke huyo kukataa kufuta picha za wajukuu zakee ambazo alikuwa ameziweka kwenye mtandao wa kijamii.

Mama na watoto wake walikuwa wamemuomba mara kadhaa kufuta picha hizo.

Kanuni iliyozingatiwa kwenye maamuzi na hakimu hata hivyo haizingatii data binafsi au ya mmiliki.

Lakini hilo halikutumiwa katika maamuzi kwasababu kuweka picha kwenye mitandao ya kijamii kuliwafanya wao kufahamika na wengi, uamuzi huo umesema.

"Kwa mtandao wa Fecebook, ni jambo linalowezekana kwa picha zilizowekwa kusambazwa na kuishia kwa mtu wa mwingine," hakimu alisema.

Mwanamke huyo ni lazima afute picha hizo au alipe faini ya €50 (£45) kwa kila siku ambayo picha hizo zitakuwa zinaonekana mtandaoni ikiwa atashindwa kutekeleza uamuzi huu hadi atakapofikisha faini ya €1,000.

Ikiwa ataweka picha zingine zaidi za watoto hao siku za usoni, atatozwa faini ya ziada ya €50 kwa siku.

"Najua uamuzi huu utashangaza wengi ambao huwa hawafikirii mara mbili kabla ya kuandika ujumbe au kuweka picha mitandaoni," amesema Neil Brown, wakili wa masuala ya teknolojia katika kampuni ya Decoded Legal.

"Bila kuzingatia msimamo wa kisheria, je inawezekena kwa wale ambao wametuma picha hizo kufikiria kwamba, 'yeye hazihitaji tena?"

"Cha kufanya kama mwanadamu - ni kuzifuta picha hizo."

Pia unaweza kusoma:

Mada zinazohusiana