Iran yawakamata waliopigana busu juu ya nyumba

Iran yawakamata waliopigana busu juu ya nyumba

Mwanamichezo wa Iran anayefahamika kwa kufanya michezo hatari ya kuruka juu ya mijengo amekamatwa baada ya video inayomuonesha akimpiga busu msichana juu ya nyumba kuvuma mitandaoni.

Familia ya Alireza Japalaghy, imeambiwa na polisi kuwa video hiyo iliyochapishwa kwenye mtandao wa Instagram haiambatani na ‘maadili ya Kiislam’.