Virusi vya corona: Madaktari wanasema kwamba ni ugonjwa usioeleweka

Wangonjwa wengi ambao wamekuwa na tatizo la damu kuganda katika mishipa wamekuwa wakitumia dawa za kujaribu kuyeyusha damu

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Wangonjwa wengi ambao wamekuwa na tatizo la damu kuganda katika mishipa wamekuwa wakitumia dawa za kujaribu kuyeyusha damu

Unapozungumza na madaktari wa chumba cha wagonjwa mahututi nchini Uingereza na mataifa mengine duniani ambao wamekuwa wakikabiliana na athari mbaya za Covid-19 kwa wiki kadhaa , maneno wanayorejelea ni: Hatujaona kitu kama hiki.

Walijua kwamba kuna ugonjwa unaokuja: Ugonjwa unaoathiri mapafu ambao kwa mara ya kwanza uligunduliwa nchini China mwaka uliopita.

lakini dalili za ugonjwa huo zimewashangaza wataalamu wengi wa vyumba vya wagonjwa mahututi.

Jinsi virusi hivyo vinavyozaana na kubadilika

Watu wengi walioambukizwa virusi hivyo vipya vya corona walikuwa na dalili za kadri, huku wengine wakikosa kuwa na dalili.

lakini miongoni mwa wagonjwa wengi walio katika hali mahututi, ni ugonjwa usioeleweka.

Kinachofuatia ni kile ambacho madaktari wamejifunza katika miezi hii kuhusu jinsi Covid-19 inavyoshambulia mwili na kila kitu kisichoeleweka kuhusu ugonjwa huu.

Ni ugonjwa hatari zaidi ya homa ya mapafu

Huku madaktari wakitaraji kupata virusi vya homa ya mapafu vinavyosababisha homa hiyo, kitu kama homa ya msimu lakini yenye madhara makubwa ,ilibainika kwamba virusi hivyo vinaathiri zaidi ya pumzi za mwanadamu, alisema.

Anthony Gordon, daktari wa chumba cha wagonjwa mahututi ICU katika hospitali ya St Mary's mjini london akizungumza na BBC amesema kwamba homa ya virusi vya mapafu ni ugonjwa mbaya ambapo msururu wa maambukizi ya mapafu husababisha uvimbe huku kinga ikikabiliana nao - lakini ugonjwa wa Covid-19 ni tatizo jipya.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Coronavirus inaweza kuathiri sio tu mfumo wa kupumua lakini pia viungo vingine kama vile ini, figo, matumbo, moyo na ubongo

''Ni ugonjwa tofauti sana zaidi ya kile tulichokiona kufikia sasa kutoka kwa mgonjwa mmoja hadi mwingine tofauti na ugonjwa mwengine wowote ule'', anasema Ron Daniels, daktari wa ICU mjini Birmigham, UK.

Katika wagonjwa waliokuwa katika hali mbaya zaidi, virusi hivyo vimewasababishia uvimbe na mgando wa damu katika mishipa, kushambulia viungo tofauti mwilini na kusababisha matatizo ambayo yanamfanya mgonjwa kuwa hatarini.

Tumukuwa na wagonjwa walio katika hali mbaya sana ambao uzani wao unapitia mabadiliko makubwa, alisema Beverly Hunt mtaalamu katika chumba cha wagonjwa mahututi katika hospitali ya London akizungumza na BBC.

Oksijeni

Mnamo mwezi Machi, wakati virusi hivyo vilipoanza kusambaa kwa haraka nchini Uingereza, wagonjwa waliokuwa na tatizo la kupumua walilazwa hospitalini.

Lakini pia wagonjwa waliokuwa katika hali mahututi , ambao viungo vyao vya mwili vilikuwa na matatizo mengine mbali na tatizo hilo la mfumo wa kupumua, tabia yao ilikuwa tofauti suala ambalo madaktari wameshindwa kuelezea.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Damu kuganda kunaweza kusababisha matatizo kadha wa kadha kwa mgonjwa ikiwemo kifo

Mgando wa damu ndio tatizo kubwa linalowakumba wagonjwa walio katika hali mahututi.

''Hatujui kwa nini baadhi ay wagonjwa uhisi vyema mara ya kwanza licha ya kuwa na viwango vidogo vya Oksijeni katika damu, kulingana na Hugh Montgomery, daktari wa ICU katika hospitali ya London kaskazini.

Anthony Gordon anaamini hii inaweza kuhusishwa na uvimbe unaodaiwa kuathiri mishipa ya damu.

Uvimbe huo huzuia oksijeni kuingia katika damu hatua inayosababisha viwango vya chini vya damu , lakini mapafu hayaathiriki katika awamu hii ya mapema.

Hii ndio sababu madaktari wengi wamehoji iwapo utumizi wa mashine za kusaidia kupumua ni suluhu nzuri kwa ugonjwa huo.

Ijapokuwaiumechangia kupona kwa wagonjwa walio katika hali mahututi, kwa wengine imekuwa na madhara.

Kawaida, wale wanaothirika na maambukizi hatari ya virusi vya mapafu huwekewa mashine za kuwasaidia kupumua kwa wiki moja.

Chanzo cha picha, Getty Images

''Lakini katika ugonjwa wa Covid-19 , watu huwekewa mashine za kupumua kwa muda zaidi, na hatujui kwa nini'', anasema Danny Macauley , mtaalam wa chumba cha wagonwja mahututi katika hospitali ya Royal Victoria mjini Belfast Irelanda kaskazini.

Hii hutokana na sababu kwamba virusi hivyo vinaendelea kuharibu ama mfumo wa kinga kukabiliana na virusi hivyo ambavyo husababisha uvimbe huo hatua inayosababisha madhara kadhaa mwilini.

Na matatizo mengi yamesababishwa na damu.

Uvimbe na mgando wa damu

Kila mtu anakubali kwamba viwango vya juu vya maambukizi ya mapafu hufanya virusi vya Covid-19 kuwa ugonjwa tofauti.

Wakati nyuta za mishipa ya damu zinapovimba , damu huganda huku Covid -19 ikifanya damu kuwa nzito na inayonata miongoni mwa wagonjwa walio katika hali mahututi.

''Tumegundua migando midogo ya damu katika mishipa midogo katika mapafu, lakini pia migando mikubwa ya damu katika mishipa mikubwa'' , anasema Montgomery.

Zaidi ya asilimia 25 ya wagonjwa wana migando mikubwa ya damu , likiwa ni tatizo. Na jinsi damu inavyozidi kuwa nzito ndiposa tatizo hilo linazidi kuwa kubwa.

Mfuumo wa kinga na viungo vya mwilini

Katika baadhi ya wagonjwa wengine kuna maambukizi makali ambayo yanaweza kuhatarisha maisha ya mfumo wa kinga.

Uvimbe huo huwa mkubwa hali ya kwamba unaweza kuathiri viungo vya mwilini. Kwa upande mwengine ,seli za damu kwa jina T Lymphocytes hupungua kwa kiwango kikubwa.

Hivyobasi watafiti wanasema kwamba kuongeza idadi ya seli T kunaweza kumsaidia mgonjwa kupona.

Sababu hizo zote hufanya ugonjwa wa Covid-19 kuwa usioeleweka , Ni ugonjwa ambao wataalam wanasema una mifumo mingi.

Hii ndio sababu inayofanya ugonjwa huo kuwa vigumu kutibu kila mgonjwa binafsi, Na kufikia sasa hakuna muongozo unaoelezea kila ambacho unapaswa kufanya.

Sio mapafu pekee ambayo huathirika, anasema Hugh Montgomery. Pia unaathiri figo, moyo na ini.

Zaidi ya wagonjwa 200- nchini Uingereza waliolazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi wamepata tatizo la kufeli kwa figo.

Ubongo wa wagonjwa walio katika hali mahututi pia umeanza kuzua hofu. Sasa tumegundua kwamba idadi kubwa ya wagonjwa wa Covid-19 hukumbwa na uvimbe katika ubongo.

Ukosefu wa oksijeni na mishipa ya damu ilioharibika ni mojawapo ya maswali yanayoulizwa.

lakini kuna ushahidi kwamba viungo vingine hushambuliwa moja kwa moja na virusi ,na la kushangaza ni kwamba hali zinazohusishwa na madhara ya Covid 19 sio magonjwa ya mapafu kama vile pumu.

Changamoto

Hatahivyo, hii haielezi kwanini watu wengi walioathirika wana pumu ama hawana dalili kali , huku wengine wakiugua sana katika kipindi kifupi.

Madaktari wengi wanaamini kwamba jeni huenda ni miongoni mwa sababu katika baadhi ya wagonjwa ambao huugua sana na Virusi vya Covid-19.

Inawezekani kwamba tofuti ya jeni ambazo huvutia magonjwa kama vile shinikizo la damu na kisukari pia huvutia virusi hivyo. Kwa sasa kuna maswali mengi kama jinsi ambavyo kuna majibu mengi.

Barabara Miles anasema kwamba kukabiliana na ugonjwa huo kumempatia uzoefu mkubwa katika kazi yake.

''Tungependelea kujua zaidi jinsi ya kutibu na kuzuia mgando wa damu miongoni mwa wagonjwa''.