Kijiji cha Bedono kinachozama

Kijiji cha Bedono kinachozama

Kijiji cha Bedono katikati ya mji wa Java kuna wakati kilikuwa ni makazi kwa familia 200. Lakini kwa sasa ni familia moja pekee iliyosalia.

Kijiji hicho cha pwani ya Java nchini Indonesia moja ya kisiwa kilichokuwa na idadi kubwa zaidi ya watu, kwa sasa kinazama na kutishia maisha ya watu milioni tano.

Utafiti unaonesha uharibifu wa mikoko na kuongezeka kwa kiwango cha maji baharini kuwa miongoni mwa sababu ya mabadiliko ya hali ya hewa vinavyolaumiwa kwa kudidimia kwa kisiwa hicho.