Félicien Kabuga: 'Huo wote ni uongo, sikumuua Mtutsi yeyote'

Interpol handout photos of Félicien Kabuga

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Félicien Kabuga, alikuwa mtu tajiri zaidi Rwanda, alitumia utajiri huo kutoroka kukamatwa

Mshukukiwa mkuu wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda anayetuhumiwa kwa kufadhili mauaji hayo amekanusha madai hayo.

"Huo wote ni uongo. Sikumuua Mtutsi yeyote. Nilikuwa nafanya nao kazi," Félicien Kabuga aliiambia mahakama ya Ufaransa wakati wa kusikilizwa kwa kesi yake.

Mfanyabiashara huyo mwenye umri wa miaka 84 alikamatwa mapema mwezi huu viungani mwa mji wa Paris baada ya kutafutwa kwa miaka 26.

Bwana Kibuga anadaiwa kuwafadhili silaha jamii ya kihutu ambao waliwauwa watu wapatao 800,000 mwaka 1994.

Kwa zaidi ya siku 100, mauaji hayo yalilenga jamii ya kabila la Watutsu ambao walikuwa wachache na wapinzani wao wa kisiasa bila kujali asili ya kabila lao.

Bwana Kabuga pia alifadhili kituo maarufu cha radio na televisheni cha Libre des Mille Collines (RTLM), kituo hicho cha matangazo ambacho kilikuwa kinatangaza kwa lugha ya kinyaruanda kilikuwa kinahamasisha wahutu kuwatafuta jamii ya watusi na kuwauwa.

Mwaka 1997 bwana Kibuga alitajwa kuwa na mashtaka saba ya mauaji ya kimbari na uhalifu dhidi ya ubinadamu katika kitengo cha umoja wa mataifa cha kusikiliza uhalifu uliofanyika Rwanda.

Mahakama ya Umoja wa mataifa ambayo mwaka 2015, iliamua kuhamishia shughuli zake na kupeleka The Hague mahakama ambayo itasikiliza wahalifu waliosalia wa kivita na mauji ya kimbari.

Dhamana kukataliwa

Mawakili wa bwana Kabuga,wametaka kesi ya mteja wao kusikilizwa Ufaransa badala ya kesi hiyo kuhamishwa.

Félicien Kabuga ni nani?

  • Alikuwa tajiri mkubwa nchini Rwanda kabla ya mauaji ya kimbari kutokea mwaka 1994.
  • Alipata utajiri wake kupitia biashara ya majani ya chai mnamo mwaka 1970 na kuanzisha makampuni mengi nchini humo na hata nje ya nchi.
  • Alikuwa karibu na chama tawala cha MRND - na alikuwa na ujamaa na rais Juvénal Habyarimana, ambaye alifariki mwaka1994
  • Anashutumiwa kuwa mfadhili mkubwa wa mipango ya mauaji ya kimbari na kutumia biashara yake na utajiri wake kupanga na kufadhili mauaji.
  • Mmiliki mkuu wa kituo binafsi cha radio ya RTLM ambayo ilikuwa inashutumiwa kuhamasisha wahutu kuwauwa watutsi.
  • Marekani iliweka dau la dola milioni tano kwa yeyote atakayetoa taarifa za kumkamata mtuhumiwa huyo.

Mwandishi wa BBC Great Lakes Samba Cyuzuzo anasema bwana Kabuga alikanusha madai dhidi yake mahakamani, alizungumza kwa lugha ya Kinyarwanda na kutafsiriwa na mkarimani, alijibu mashtaka dhidi yake kwa mara ya kwanza baada ya kutuhumiwa kwa Zaidi ya mion

Polisi wanasema katika kipindi hicho alichojificha, alitumia majina ya uongo 28 ili kukwepa asikamatwe.

Mahakama ilikataa maombi yake ya kupewa dhamana kwa sababu za kiafya na uzee kuwa ni hatari kwa mtuhumiwa kukaa gerezani.

Kesi ilihairishwa kusilikilizwa mpaka Juni 3.

Wakati huo huo bwana Kabuga alidaiwa kukaa katika mataifa mengi Afrika mashariki ikiwemo Kenya, ambako ana familia na kumiliki biashara.

Bado wanyaruanda wengine sita ambao wanatuhumiwa na mauaji ya kimbari wanatafutwa.

Wahutu wengi wamehukumiwa kwa kuhusika katika mauaji ya kimbari katika mahakama ya kimataifa ya ICTR na mamia wengine kesi zao zilisikilizwa katika mahakama za jamii za Rwanda.