Virusi vya corona: Watu 'wasiojua wana virusi’ wanavyochangia kuongezeka kwa maambukizi

wanasayansi wamepata ushahidi wa kushangaza kuhusu jinsi virusi vya corona vinavyosambazwa
Maelezo ya picha,

wanasayansi wamepata ushahidi wa kushangaza kuhusu jinsi virusi vya corona vinavyosambazwa

Ulimwengu unapoendelea kukabiliana na janga la corona, wanasayansi wamepata ushahidi wa kushangaza kuhusu jinsi virusi vya corona vinavyosambazwa. Japo watu wengi wanaopata maambukizi huonesha dalili za kukohoa, homa na kupoteza ladha ya chakula, miongoni mwa dalili zingine bila kujua wanaugua ugonjwa wa Covid-19.

Watafiti wanasema ni muhimu kuelewa ni watu wangapi wameathiriwa na virusi kupitia njia hizi na ikiwa "wasiojua wana virusi" wanachangia kuongezeka kwa janga la corona.

Watu walipokusanyika katika kanisani nchini Singapore Januari 19, hakuna aliyejua ibada hiyo ya kidini ingeligeuka kuwa janga la kimataifa na chanzo cha kuenea kwa kasi kwavirusi vya corona duniani.

Ilikuwa siku ya Jumapili, na kama kawaida moja ya ibada ilikuwa inaendeshwa kwa Kimandarin. Miongoni mwa waliohudhuria ibada katika kanisa la The Life Church, ni mume na mke, walio na miaka 56, ambao waliwasili nchini humo, Jumapili asubuhi kutoka China.

Walionekana kuwa wenye buheri wa afya kwa hiyo hapakuwa na sababu yoyote ya kuwa na hofu wameambukizwa virusi. Wakati huo kukohoa mara kwa mara kulijulikana kuwa dalili kuu ya Covid-19 na ilionekana kama chanzo kikuu cha kueneza maambukizi. Bila kuwa na dalili hiyo inamaanisha hakuna uwezo wa ugonjwa kusambazwa.

Ibada ilipomalizika wanandoa hao walisafiri na kurejea kwao China. Lakini siku chache baadae hali yao ya kiafya ilibadilika ghafla na kuwa mbaya.

Mke alianza kuwa mgonjwa Januari 22, na kufuatiwa na mume wake siku chache baadae. Hilo halikuwa la kushangaza wengi, kwa sababu walikuwa wamesafiri kutoka Wuhan, kitovu cha mlipuko wa virusi vya corona.

Lakini wiki kadhaa baadae, wakazi pia walianza kuwa wagonjwa, hali ambayo iliifanya Singapore kuwa na kisa cha kwanza cha kushangaza cha maambukizi ya corona. Kuchunguza ni nini hasa, kilichotokea huenda kukabaini njia mpya ambayo inasaidia virusi hivyo hatari kusambaa.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Singapore ilishuhudia ongezeko la maambukizi baada ya kuonekana kufanikiwa kudhibiti virusi

Kuwashirikisha 'Wachunguzi wa magonjwa'

"Tumeshangazwa sana," anasema Dkt. Vernon Lee, mkuu wa kitengo cha maradhi ya kuambukiza katika Wizara ya Afya ya Singapore.

''Watu ambao hawakujuana wameambukizana virusi," bila kuonesha ishara ya dalili zozote. Mbinu hii mpya ya maambukizi haieleweki kabisa, kwa mujibu wa kile kilichojulikana mwanzoni kuhusu ugonjwa wa Covid-19.

Kutokana na hilo Dkt Lee na wanasayansi wenzake, wakishirikiana na maafisa wa polisi na wataalamu wa kudadisi magonjwa, walizindua uchunguzi, inayojumuisha ramani ya kina inayoonesha nani alikuwa wapi na lini.

Huu ni mpango wa hali ya unatumiwa kuwatafuta waliotangamana na watu waliopatiikana na virusi - ambao pia umenza kutumiwa nchini Uingereza. Unaonekana kama njia bora ya kuwatafuta watu wote waliohusika katika mzunguko wa mlipuko wa maambukizi ili kuzuia kuenea zaidi kwa maambukizi hayo.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mwanzoni,Singapore ilionekana kuwa mfano katika mapambano dhidi ya virusi vya corona

Cha kutia moyo ni kuwa, ndani ya siku chache, wachunguzi walikuwa wamezungumza na waumini karibu 191 wa kanisa hilo na kugundua kuwa 142 kati yao walifika kanisani Jumapili hiyo. Moja kwa moja walithibitisha kuwa raia wawili wa Singapore waliambukizwa katika hafla hiyo hiyo iliyohudhuriwa na wanandoa wa China.

"Huenda walizungumza nao au kusalimiana nao, katika shughuli za kawaida za ibada kanisani," anasema Dkt Lee.

Hiyo ndio ilikuwa hatua ya kwanza muhimu ya kuelezea jinsi maambukizi yalivyosambaa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine, tofauti na dalili moja kuu ya kawaida. Hata hivyo haikujibu swali la jinsi virusi huenda vilisambazwa na Wachina wawili ambao walikuwa wana virusi japo hawakuonesha dalili za kuwa na ugonjwa.

Zaidi ya hayo kulikuwa na kitendawili kikuu ambacho kilihitaji kuteguliwa. Ilithibitishwa kuwa raia wa tatu wa Singapore kuambukizwa virusi vya corona alikuwa, mwanamke wa miaka 52, amble pia alihuduria ibada nyingine katika kanisa hilo baadae siku hiyo, swali ni je huenda alipata maambukizi ya virusi hivyo mahala hapo?

Ushahidi ambao hakuna mtu alitarajia

Wachunguzi waliamua kufuatilia rekodi za kamera ya CCTV katika kanisa hilo Jumapili hiyo kutafuta ushaidi zaidi. Waligundua kitu ambacho hawakutarajia- mwanamke aliyehudhuria ibada ya pili baada ya wanandoa hao wa Kichina kuondoka, alikalia kiti walichotumia saa kadhaa baadae.

Hii inamaanisha, licha ya kutoonesha dalili zozote za kuwa wagonjwa, wanandoa hao wa Kichina walifanikiwa kusambaza virusi. Pengine kupitia mikono yao walipogusa viti, ama walipozungumza matone ya mate yalipakia kwenye viti, japo haijabainika wazi, madhara ni makubwa.

Kwa sasa Dkt Lee, anaunganisha pamoja matokeo ya uchunguzi huo, ili kupata kubaini - ikiwa vuirusi vya corona vinaenezwa na watu ambao wameambukizwa lakini hawana habari wana virusi hivyo.

Lakini ikiwa virusi vya corona vinaweza kuenezwa kimya kimya na watu wasio na dalili zinazoonekana, ugonjwa utakomeshwa vipi?

Baadhi ya watu hawaoneshi dalili

Hii ni swali ambalo linaendelea kuwashangaza wanasayansi wengi kwasababu hawana jibu sahihi. Ni kitu kimoja kufahamu kuwa watu wanaweza kuambukizwa virusi kabla ya mifumo ya miili yao kuonesha dalili, na ni kitu kingine kabisa wakati watu wameambukizwa virusi lakini hawaoneshi kabisa dalili kwamba wanaugua.

Hii ni hali inayojulikana kama "asymptomatic" kwa sababu waliobeba virusi vya ugonjwa hawaathiriki kwa njia yoyote japo wanaeneza virusi bila kujua.

Mfano mzuri wa muuguzi Amelia Powell ambaye alishtukia ameambukizwa virusi vya corona lakini hakuonesha dalili zozote za maambukizi.

Amekuwa akijihisi vyema na kwamba yuko salama kutokana na vifaa kinga anavyovalia kila anapokuwa katika mazingira ya kazi na anapowahudumia wagonjwa wa Covid-19.

Lakini matokeo ya uchunguzi yalipotolewa aligundulika kuwa ameambukizwa virusi .

"Ni sawa na kupata taarifa za kifo kumhusu mtu wa familia yako, inashutua sana. "Nilidhani siwezi kupata corona'', alisema Amelia,23.