Maandamano Marekani: Je Trump anaweza kutuma majeshi kudhibiti vurugu?

Black woman in front of police in riot gear

Chanzo cha picha, Google

Wakati maandamano yakishika kasi nchini Marekani, Rais wan chi hiyo, Donald Trump ametishia kutuma majeshi yake ili kutuliza ghasia.

Bwana Trump amesema atatuma vikosi vyake kama miji na majimbo yatashindwa kutatua tatizo.

''Kama mji au jimbo litakataa kuchukua hatua ambazo ni muhimu...basi nitatuma jeshi la Marekani'', alisema rais Trump.

Maelezo ya picha,

Rais Donald Trump

Lakini magavana wa majimbo wamesema serikali haina mamlaka ya kupeleka vikosi bila ridhaa ya mamlaka za majimbo.

Rais anaweza kutuma vikosi vya kijeshi?

Kwa kifupi, ndio lakini katika mazingira fulanifulani.

Tayari kuna maelfu ya vikosi vilivyosambazwa kutoka jeshi la ulinzi la taifa hilo, ambavyo ni vikosi vya akiba vya jeshi la Marekani.

Kuna zaidi ya majimbo 20 nchini humo yanayojaribu kutuliza maandamano, lakini vikosi hivi vimeombwa na miji na majimbo yenyewe.

Hatahivyo, Sheria ya Marekani iliyopitishwa katika karne ya 19 inaeleza mazingira ambayo serikali ya Washington DC inaweza kuingilia kati bila ridhaa ya mamlaka ya jimbo.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Wanajeshi wa kikosi cha ulinzi cha akiba cha taifa cha Marekani

Sheria hiyo inasema ridhaa ya magavana haitakiwi pale rais anapothibitisha kuwa hali katika jimbo inawia ngumu kusimamia sheria nchini Marekani, au wakati haki za raia zinapotishiwa.

Sheria hiyo ilipitishwa mwaka 1807 kuruhusu rais kutoa majeshi yake kwa ajili ya kulinda dhidi ya ''hatari ya mashambulizi ya raia wa India''- na ilitoa nguvu zaidi kwa kuruhusu jeshi la Marekani kuingilia kati hali ya vurugu nchini humo ili kulinda haki za raia.

Sheria nyingine ilipitishwa mwaka 1878 ikitaka mamlaka ya bunge kuidhinisha matumizi ya jeshii, lakini mtaalamu wa masuala ya sheria ameiambia BBC kuwa sheria ya kupambana na vitendo vya uvamizi ina nguvu ya kusimama yenyewe ambapo rais huwa na mamlaka kisheria kupeleka jeshi bila kuomba idhini kutoka kwenye majimbo katika mazingira ya sasa.

''Suala muhimu'' anasems Robert Chesney, Profesa wa sheria katika Chuo Kikuu cha Texas, '' ni maamuzi ya rais kuchukua; magavana hawana haja ya kuomba msaada wake.''

Unaweza pia kusoma:

Sheria hii iliwahi kutumika kabla?

Kwa mujibu wa huduma ya utafiti ya bunge, sheria hii iliwahi kutumika mara kadhaa zamani, ingawa si kwa takribani miongo mitatu.

Mara ya mwishi ilitumika mwaka 1992 na rais mstaafu George HW Bush wakati wa vurugu za mjini Los Angeles.

Sheria ilitumika miaka ya 1950 na 60 na marais watatu tofauti walioongoza miaka hiyo.

Rais Dwight Eisenhower alikabiliwa na upinzani wa magavana alipotumia sheria hiyo mwaka 1957 alipopeleka vikosi Arkansas kudhibiti maandamano shuleni, ambapo watoto wenye asili ya weusi na weupe walikuwa wakisoma pamoja.

Tangu mwishoni mwa miaka ya 1960, matumizi ya sheria hii yalikuwa kwa nadra. Bunge lilifanya marekebisho mwaja 2006 baada kimbunga cha Katrina ili kulipa jeshi ufanisi , lakini marekebisho yaliondolewa baada ya magavana kupinga hatua hiyo.