Kifo cha George Floyd: Maelfu wajitokeza Marekani kushiriki mandamano usiku kucha

Melfu ya watu wamejitokeza kote New York kwa maandamano yaliyoendelea usiku kucha juu ya kifo cha George Floyd

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Melfu ya watu wamejitokeza kote New York kwa maandamano yaliyoendelea usiku kucha juu ya kifo cha George Floyd

Maandamano juu ya kifo cha raia mweusi wa Marekani George Floyd bado yanaendelea kwa usiku wa nane mfululizo.

Kifo cha Floyd kilichotokea Mei 25, mikononi mwa polisi huko Minneapolis kimesababisha maandamano makubwa katika maeneo mbalimbali nchini huko.

Waandamanaji wameamua kukiuka hatua ya kusalia ndani iliyowekwa katika miji mbalimbali.

Katika eneo la Fort Worth, Texas, inasemekana kundi dogo la watu lilisalia nje hata baada ya kuanza kwa muda wa kutoka nje saa mbili usiku.

Waandamanaji katika mji wa New York pia nao walikiuka hatua ya kutoka nje iliyowekwa kuanzia saa mbili usiku.

Meya wa mji alisongeza mbele muda huo kwa usiku wa pili mfululizo baada ya waandamanaji kupora eneo la kibiashara la Manhattan Jumatatu.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Wanajeshi wa Marekani wakiwa mitaani kuzuwia maandamano

Na katika mji wa Washington DC, kundi kubwa la watu limeendelea kukusanyika nje hata baada ya kuanza kwa muda wa kutoka nje saa moja usiku.

Aidha, Takriban wanajeshi Taliban1,600 wamepelekwa katika maeneo ya mji wa Washington DC.

Msemaji wa serikali amesema vikosi vilikuwa katika tahadhari ya juu.

Katika jimbo la Minnesota waandamanaji wamewasilisha kesi mahakamani dhidi ya polisi kwasababu ya kifo cha Floyd. Gavana Tim Walz ameambia vyombo vya habari kwamba uchunguzi wa kifo hicho utalenga kumaliza tatizo la ubaguzi wa rangi ambalo limedhihirika kuwa sugu.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Katika Los Angeles, mabango yaliyoandika Black Lives Matter - vuguvugu lililo katika maandamano ya kupinga mauaji ya polisi dhidi ya watu weusi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mwanaume mmoja na mtoto wake wa mwaka mmoja walikua miongoni mwa waandamanaji katika jiji la Californian la Pasadena

Vilevile, watu wameendelea kukutana katika mji wa Floyd, Houston, Texas, na kufanya maandamano ya amani na familia ya marehemu Floyd. Watu hadi 20,000 wanatarajiwa kushiriki maandamano hayo, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya eneo.

Roxie Washington, Mke wa George Floyd akizungumzia mtoto wao wa kike wa miaka sita aliyeachwa bila baba, Gianna, katika mkutano na wanahabari huko Minneapolis, "Gianna hana tena baba," alisema."Baba yake hata muona tena akikua, akihitimu shule, wala kumshika mkono siku ya harusi yake. Ikiwa ana tatizo lenye kumuhitaji baba yake, hayupo tena duniani.

"Niko hapa kwa ajili ya mtoto wangu na mume wangu George kwasababu ninataka haki itendeke. Ninataka haki itendeke kwasababu alikuwa mtu mzuri haijalishi mwengine anafikiria nini."

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Maafisa wa usalama wakipiga goti pamoja na waandamanaji Atlanta

Maafisa wa polisi na jeshi wamejitokeza katika miji tofautitofauti wakipiga goti pamoja na waandamanaji kama ishara ya kuonesha mshikamano.

Katika mji wa Los Angeles, waandamanaji walikuwa wanashabikia wanajeshi pale walipopiga goti.

Waandamanaji waliwataka wanajeshi kufanya maandamano nao, lakini wakasema kwamba wanahitaji kusalia sehemu moja.

Mwandishi wa BBC Phoebe Frieze alikuwa katika kumbukumbu ya Lincoln Washington DC kabla tu ya kuanza kwa muda wa kutotoka nje saa moja jioni ambapo mamia ya waaandamanaji walikuwa wamepiga magoti mbele ya sanamu la Lincoln na kukaa kimya, huku vikosi vya taifa vilivyojihami vikiwa vimepanga mstari mbele vikitazama waandamanaji.

Barabara nyingi zinazoelekea kwenye kumbukumbu hiyo zilikuwa zimefungwa na vizuizi vya polisi na pia helicopter inayoshika doria ilisikika kwa juu.

Waandamanaji walitaja majina ya watu wengine waliokufa kwa njia tatanishi mikononi mwa polisi kama vile Tamir Rice, 12, aliyeuawa Cleveland, Ohio, 2014.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Waandamanaji walitawanywa kwa gesi za kutoa machozi muda wa amri ya kutotoka nje ulipoanza

Ni katika ukumbi wa Lincoln mwaka 1963 ambapo Martin Luther King Jr alitoa hotuba yake maarufu ya "I have a dream" yaani nina ndoto.

Dakika 15-20 kabla ya muda wa kusalia ndani kuanza waandamanaji walianza kuondoka.

Trump atoa heshima kwa mkuu wa polisi aliyepiga risasi

Wakati hayo yakijiri Rais Donald Trump ametoa heshima kwa David Dorn, mkuu wa polisi mweusi aliyepigwa risasi wakati wa maandamano katika eneo la St Louis, Missouri.

Dorn, 77, alipatikana amekufa mbele ya duka la moja ambalo liliporwa saa za asubuhi Jumanne.

Alistaafu katika kituo cha polisi cha St. Louis, 2007, na tagu wakti huo amekuwa akihudumu kama mkuu wa polisi kwenye mji huo mdogo, kwa mujibu wa shirika la habari la ABC News.

Trump alisema: "Heshima yetuni kwa familia ya David Dorn, msimamizi bora wa kituo cha polisi cha St. Louis."

Rais alisema Dorn alipigwa risasi na kuuawa na waporaji hao".

Hadi kufikia sasa hakuna aliyekamatwa kuhusiana na mauaji hayo, polisi imesema.