George Floyd: Je, Trump ameiwezeshaje jamii ya watu weusi ?

Black Trump supporter

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Rais Trump anatafuta namna ya kupata kura za watu weusi katika uchaguzi wa rais wa mwaka 2020

Maandamano yanaendelea katika maeneo mbalimbali nchini Marekani kutokana na kifo cha Mmarekani mweusi , George Floyd, Rais Donald Trump alisema kuwa amefanya mambo mengi kwa watu watu weusi hata zaidi ya rais yeyote yule tangu wakati wa Abraham Lincoln".

Aliandika kwenye kurasa wake wa twitter, akisema kuwa katika historia ya Marekani, amewezesha watu weusi kupata ajira, umaskini na uhalifu kupungua.

Je amefanyaje hayo anayoyasema?

1. Je ni kweli idadi ya Wamarekani weusi wasio na ajira imepungua katika historia?

Ukosefu wa ajira kwa Wamarekani weusi , umefika 16.7% mwezi Aprili mwaka huu - kiwango ambacho ni kikubwa tangu Machi 2010.

Mabadiliko hayo yameshuka ghafla kutokana na athari za virusi vya corona katika uchumi wa Marekani.

Na hali hiyo imewaathiri sana Wamarekani weusi - asilimia mbili ya kiwango cha ukosefu wa ajira kimeongezeka zaidi katika takwimu.

Lakini ni muhimu kusema kuwa kiwango hicho kimeshuka mpaka 5.5% mwezi Septemba mwaka jana - Idadi ndogo ambayo ilirekodiwa katika idara ya ajira katika takwimu zilizokusanywa tangu mwaka 1970.

Kutokea kwa janga la virusi vya corona, kumekuwa na kushuka kwa asilimia ya ajira kwa Wamarekani weusi chini ya uongozi wa rais Trump.

Lakini ni mabadiliko ambayo yalianza kuonekana tangu wakati wa uongozi wa Barack Obama, ambaye aliona ukuaji wa ajira kwa watu weusi ukishuka kutoka 12.6% mpaka 7.5% katika kipindi chote cha utawala wake 2009 mpaka 2017.

Hatahivyo ukiachia mbali utofauti wa mishahara kulingana na makundi ya watu.

Kipato cha kati cha Wamarekani weusi ni karibu 60% chini ya kile ambacho wanapata watu weupe, na data hiyo ikiwa inakuwa chini ya utawala wa rais Trump, kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni.

2. Je kiwango cha umasikini kwa Wamarekani weusi

Mwaka 2018, takwimu zilizokuepo zilionesha Wamarekani weusi wana umaskini wa kiwango cha 20.8% - kiwango ambacho kiko chini kwenye rekodi, ukilinganisha na miaka ya nyuma tangu mwaka 1960.

Hii inawakilisha kuwa Wamarekani weusi milioni 8.9 ni masikini , kwa mujibu wa sensa ya Marekani.

Sensa rasmi ya Marekani imepiga mahesabu ya umaskini kwa kuangalia idadi ya kipato kwa familia ni pungufu ya kile ambacho familia ina uhitaji nacho, hivyo basi kila mtu anatambulika kuwa masikini.

Umasikini kwa watu weusi ulipungua wakati wa utawala wa rais Obama,na ilikuwa 21.8% kwa mwaka 2016 - kwa mwaka mzima.

3. Je ni kweli uhalifu ambao unaofanywa na raia weusi Marekani umepungua?

Jambo hili ni gumu kujibu kwa uhakika.

Kuna takwimu za uhalifu ambazo zinatafutwa na shirika la kijasusi la FBI, lakini takwimu ambazo zimeandikwa kulingana na rangi ya mtu.

Uhalifu ulianza kupungua wakati wa utawala wa Trump, na kuendelea tangu mwaka 1991 hali ilivyokuwa tata.

Ukiangalia idadi ya Wamarekani weusi ambao wamekamatwa - ambao unaweza kuainisha - utaona idadi ya raia weusi wa Marekani ambao wamekamatwa ni wachache kwa miaka ya hivi karibuni.

Kumekuwa ndogo kwa kipindi cha miaka minne iliyopita.

Takwimu za kuanzia mwaka 2018 zinaonesha kuwa Wamarekani weusi 2,115,381 walikamatwa, kwa mujibu wa takwimu za FBI.