Uchaguzi wa Marekani :Joe Biden anaweza kumuondoa Trump madarakani?

Hili ni jaribio la tatu kwa Joe Biden kuwania urais nchini Marekani

Chanzo cha picha, Reuters

Joe Biden aliyekuwa makamu rais wa Marekani sasa yupo katikati ya Donald Trump na miaka minne ijayo katika Ikulu ya Marekani.

Biden amechaguliwa rasmi kupeperusha bendera ya chama cha Democratic katika uchaguzi wa urais utakaofanyika Novemba.

Kwa wanaomuunga mkono yeye ni mtaalamu mwenye tajiriba ya miongo mingi Marekani mzungumzaji mzuri anayeweza kuwasiliana kwa urahisi na wananchi wa kawaida na mwanaume ambaye ameishi kwa kupitia changamoto nyingi tena mbaya mno maishani.

Kwa wapinzani wake, ni mtu mzee ambaye makosa anayofanya yanawafanya watu kuhisi aibu.

Je ana uwezo wa kumuondoa Trump kutoka Ikulu ya Marekani?

Joe Biden ni mtu anayesimama dhidi ya Donald Trump kwa nafasi ya urais kipindi cha miaka minne

Makamu wa rais wa Barack Obama ambaye awali alimchaguliwa kuwa mgombea wa nafasi ya urais.

Kwa watu wanaomuunga mkono ni mtaalamu wa sera za mambo ya nje akiwa na uzoefu mkubwa

Biden sio mgeni kisiasa hasa katika kampeni za uchaguzi - taaluma yake Marekani ilianza kama alipokuwa Seneta 1973 miaka 47 iliyopita na kampeni yake ya kwanza katika uchaguzi wa urais ni 1987 miaka 33 iliyopita.

Yeye ni mtu mwenye ushawishi mkubwa kwa wapiga kura na wakati huohuo mwenye uwezo wa kusababisha athari siku za baadae.

Chanzo cha picha, Getty Images

Kuonesha hisia zake kinagaubaga mbele ya umati kulimaliza kampeni yake ya kwanza ya urais (hii ni mara yake ya tatu) hata kabla haijaanza.

Akiwa kwenye mkutano wa kampeni alidai: "Mababu zangu walifanyakazi katika migodi ya mawe -mashariki mwa Pennsylvania" na kuonesha hasira eti kwasababu hawakupata fursa walizostahili.

Lakini hakuna hata mmoja katika kizazi chake aliyefanya kazi katika mgodi wa mawe - alikuwa ameigiza maneno hayo ( na mengine mengi) kwa hotuba ya mwanasiasa wa Uingereza Neil Kinnock, ambaye jamaa zake walikuwa wachimbaji migodi.

Na huo ulikuwa mwanzo wa matukio mengi ambayo yalibainika kama "Mabomu ya Joe".

Akisifu tajiriba yake ya kisiasa 2012 aliiambia hadhira: "Watu wangu, naweza kuwaarifu kwamba nimejuana na marais wanane, watatu kwa karibu," kwa bahati mbaya akimaanisha kwamba alikuwa na uhusiano wa kimapenzi nao badala ya marafiki wa karibu.

Kama makamu raia wa Obama, 2009, alitahadharisha watu akisema kwamba kwa asilimia 30 hawataweza kufaulu kiuchumi.

Na pia alikuwa na bahati kuchaguliwa kama makamu wa raia wa kwanza mweusi baada ya kumuelezea kama raia wa kwanza Mmarekani mweusi mwenye maelezo ya ufasaha, mwenye akili, msafi na mtanashati.

Licha ya matamshi hayo, watu weusi wamekuwa wakimuunga sana mkono wakati wa kampeni za uchaguzi lakini hivi karibuni katika kipindi cha redio cha moja kwa moja, alijipata matatani baada ya kudai kwamba: "Ikiwa una matatizoz ya kubaini kama wewe ni mfuasi wangu au wa Trump, basi wewe sio mtu mweusi,"

Maneno hayo pekee yaligonga vichwa vya habari, na kupelekea timu yake ya kampeni kujaribu kuonesha kwamba hakuwa anachukulia kwa urahisi wapiga kura Wamerekani weusi.

Ni rahisi kuona kwanini mwanahabri wa jarida la NY mwaka jana aliandika kwamba "Biden kuzungumza maneno yasiyostahili kunaonekana kupewa kipaumbele zaidi katika kulizuia na timu yake ya kampeni kwa gharama yoyote ile."

Chanzo cha picha, Getty Images

Kampeni ya Biden

Lakini kuna upande wa pili wa ustadi wake wa kuzungumza - yeye hujitokeza kuwa mhalisia.

Anasema kwamba kumbukumbu ya utoto wake ni kwamba hapendi kuzungumza kwa kusukumwa badala yake anazungumza kutoka moyoni.

Biden anaweza kurusha mijeledi katika mkutano wa wafanyakazi wa kazi ngumungumu kisha baada ya hadhara akajumuika nao - akawapa mikono, akawashika mgongoni na kupiga nao picha kama nyota fulani vile wa muziki wa rock.

"Anaweza hata kuwapiga pambaja na kuwapa maneno matamu," aliyekuwa waziri wa mambo ya nje na mgombea wa urais John Kerry aliliambia gazeti la New Yorker, "Ni mwanasiasa stadi na mkweli."

Lakini vile kiwango ambacho amekuwa akigusa hisia za watu, hilo limekuwa tatizo.

Madai

Mwaka jana wanawake wanane walijitokeza na kumshutumu Biden kwa kuwashika, kuwakumbatia na kuwapiga busu na vituo vya habari vya Marekani vikaonesha picha ya vile anavyosalimia wanawake kwa ukaribu katika matukio - ambapo wakati mwingine alionekana hata akinusa nywele zao.

Biden aliahidi kuwa makini sana jinsi anavyochangamana.

Hata hivyo, mwezi Machi, Tara Reade, alidai kwamba alimshika kwa lazima na kumnyanyasa kingono akiwa kwenye miaka yake ya 30, wakati anafanya kazi kama msaidizi katika ofisi yake.

Biden amekanusha madai hayo na timu yake ya kampeni ilitoa taarifa ikisema: "Bila shaka hili halikutokea."

Chanzo cha picha, MEGYN KELLY

Wanademocrats wakimtetea tumaini lao katika uchaguzi wa urais watasema kwamba zaidi ya wanawake 10 wamejitokeza hadharani kumshtumu Rais Trump kama aliwanyanyasa kingono katika matukio mbalimbali lakini unaweza kuangalia madai haya kama mchezo fulani unaoendelea.

Tangu vuguvugu la #MeToo movement lilipoanzishwa, Democrats - akiwemo Biden - wamekuwa wakisisitiza kuwa jamii zinastahili kuamini wanawake, na juhudi zozote za kuzima madai yanayoibuliwa dhidi yake hakufurahiwi na wanaharakati.

Katika mahojiano kwenye televisheni, Reade alisema: "Wafuasi wake wamekuwa wakisema mambo mabaya kunihusu kwenye mitandao ya kijamii''.

"Yeye mwenyewe hajawahi kusema lolote, lakini kuna unafiki fulani katika kampeni yake inayosema kuwa ni salama - ilihali sio salama."

Hata hivyo kampeni ya Biden imekanusha madai hayo.

Historia ndefu ya Biden

Biden amekuwa akihusishwa au kusema kitu kuhusu kila tukio kubwa linalotokea katika miongo ya hivi karibuni iliyopita na uamuzi huo huenda usiwe wa kuridhisha katika mazingira ya kisiasa sasa hivi.

Miaka ya 1970 aliunga mkono waliopinga watoto kujiunga na shule jirani ili shule za Umma ziweze kusajili wanafunzi kwa misingi ya kibaguzi. Amekuwa akishambuliwa kwa hatua hii kila mara wakati wa kampeni yake.

Republicans huwa wanapenda kusema kwamba Robert Gates, aliyekuwa waziri wa ulinzi wakati wa utawala wa Obama, alisema Biden ni mtu ambaye ni vigumu kuendana naye na kwamba alikosea kwa karibu kila sera ya mambo ya kigeni na masuala ya usalama wa taifa kwa kipindi cha miongo minee iliyopita.

Bila shaka chama cha Democratic kinaweza kutaraia mengi ya aina hii katika kampeni yake.

Chanzo cha picha, Getty Images

Msiba wa Familia uliomkuta

Kwa bahati mbaya Biden anaonekana kuwa mbali na wengine ukilinganisha na wanasiasa wengine ni kwasababu amekutwa na msiba ambacho pia kinatuathiri sote.

Wakati anajitayarisha kuapishwa, muda mfupi baada ya kushinda katika uchaguzi wa kwanza kama seneta, mke wake Neilia na binti yake Naomi wapata ajali ya ndege ambayo pia ilijeruhi vijana wake wawili Beau na Hunter.

Baadae Beau aifariki baada ya kupata uvimbe wa kwenye ubongo 2015, akiwa na umri wa miaka 46.

Kupoteza watu wake wengi wa karibu akiwa na umri mdogo kumefanya raia wengi wa Marekani kumhusisha na kuwa licha ya nguvu yake kisiasa na utajiri wake bado amekumbwa na mikasa mingi ya vifo.

Hata hivyo sehemu ya simulizi yake maishani ni tofauti, ile yake na kijana wake Hunter.

Madaraka, ufisadi na uongo?

Hunter alikuwa wakili na mshawishi kabla ya kushindwa kudhibiti maisha yake.

Mke wake alisemekana kutumia dawa za kulevya, anayekunywa pombe na kutalikiana na pia alifurushwa jeshini baada ya kugundulika kuwa ni mtumiaji wa dawa za kulevya.

Kupitia gazeti la New Yorker alikubali kwamba kuna wakati alipewa Almasi na tajiri mmoja wa China wa masuala ya kawi, ambaye baadae alichunguzwa na mamlaka ya China juu ya shutuma za ufisadi.

Aidha Hunter ameamua kuishi maisha ya siri na mwaka jana inasemekana alioa mke wake wa pili wiki moja baada ya kukutana nae huku kupata kiwango kikubwa cha pesa kumechangia kupata sifa hasi upande wa baba yake.

Masuala ya mambo ya nje

Moja ya shutuma kubwa zilinazomkabili Biden nje ya nchi ni kuharibu sifa yake kidiplomasia. Alikuwa mwenyekiti wa kamati yenye kuhusika na masuala ya nje na amekuwa akijisifu kuwa amekutana na wakubwa wengi katika kipindi cha miaka 45 iliyopita.

Wakati hili linahakikishia wapiga kura kwamba ana tajriba ya kuwa rais, ni vigumu kutabiri vile wapiga kura watakavyochukulia rekodi yake hiyo.

Kama siasa zake nyingine hilo linaweza kusemekana uzito wake ni wastani tu.

Alipiga kura kupinga vita vya ghuba vya 1991, kisha akaunga mkono kuvamiwa kwa Iraq 2003 lakini akawa mkosoaji wa vile Marekani ilivyojihusisha na uvamizi huo.

Pia alimshauri Obama dhidi ya kupeleka vikosi maalum vya uvamizi ambavyo vilisabbaisha mauaji ya Osama Bin Laden.

Chanzo cha picha, Getty Images

Kupata au kokosa

Kura ya maoni kawaida huwa inamuweka Baiden katika alama tano hadi 10 mbele ya Rais Trump katika kiny'anganyiro cha kuingia Ikulu lakini uchaguzi wa Novemba bado uko mbali na bila shaka kuna mengi yatakayotokea kati ya wawili hao.

Wagombea hao wawili tayari wameshakwaruzana juu ya suala la kuunga mkono maandamano yanayopinga vitendo vya polisi kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya raia weusi na namna serikali ilivyokabiliana na virusi vya corona.

Hata uvaaji wa barakoa imebadilika na suala la kisiasa huku mara nyingi Biden akionekana hata akipigwa picha huku akiwa amevalia barakoa yake ilihali Bwana Trump akiamua kuchukua msimamo tofauti.

Ikiwa Biden atashinda itakuwa wakati wa kipekee uliosubiriwa kwa muda mrefu katika taaluma yake ya kisiasa; na ikiwa atashindwa atasubiri kwa kipindi kingine cha miaka minne.

Miaka michache iliyopita, akiwa anafikiria kama atajiunga kwenye kinyang'anyiro cha urais 2016, Biden alisema: "Naweza kufa nikiwa mwenye furaha kwa kutokuwa rais."

Lakini sasa hili limebadilika.