Virusi vya corona: Uhasama kati ya Marekani na China wajitokeza katika kukabiliana na mlipuko huo Afrika

File photo taken in November 2017 shows US President Donald Trump (R) and Chinese President Xi Jinping attending a welcome ceremony in Beijing

Chanzo cha picha, Getty Images

Huku Afrika ikijiandaa kwa ongezeko la idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya corona , China na Marekani zinadai kuwa msaidizi mkubwa wa bara hili, lakini kuna mengi ambayo hayajaangaziwa katika uhasama huo zaidi ya kukabiliana na virusi hivyo kulingana na mwandishi wa BBC Andrew Harding.

Waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Mike Pompeo alisema kwamba hakuna taifa litakaloshindana na kile ambacho Marekani inakifanya katika kusadia Afrika kukabiliana na Covid-19.

Na aliendelea kusema kwamba hakuna taifa ambalo limesaidia ama litafanya zaidi ya kusaidia Afya duniani.

Bwana Pompeo alikuwa akizungumza katika mkutano na kundi dogo la wanahabari wa Afrika pamoja na wale waliopiga kambi barani Afrika.

Nilikuwa miongoni mwao.

Wakati huo - mwezi uliopita - Nilichukulia tamko lake la 'hakuna taifa litakavyofanya zaidi', sawa na matamshi yanayotumiwa kila siku na utawala wa rais Trump, ambao ulikuwa unajaribu kuimarisha uhusiano wake wa kimataifa kufuatia uamuzi wake wa kukata uhusiano na Shirika la Afya Duniani WHO katikati ya mlipuko mkubwa zaidi duniani.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Hawa watoto walikuwa wakimkaribisha Ghana Mama wa taifa wa Marekani Melania Trump mwaka 2018.

Inasikitisha kusema kwamba $170m (£134m) za msaada ambazo bwana Pompeo anajigamba kuipatia Afrika zilishindwa na msaada wa bilionea mmoja wa China uliotolewa na Jack Ma.

lakini siku chache zilizopita, niliona habari kuhusu Afrika katika chombo kimoja cha habari kinachodhibitiwa na serikali, The global Times na nilikumbushwa kuhusu matamshi ya bwana Pompeo na kikanishangaza jinsi bara hili lilivyosukumwa katika kona moja ndogo ya vita baridi kati ya Washington na Beijing na kama ilivyokuwa awali katika vita vya baridi vilivyokuwa rasmi- mgogoro wa ghafla, kama ule wa virusi vya corona sasa umebadilishwa na kuwa mzozo fulani.

Shinikiza dhidi ya demokrasia ya vyama vingi

Habari hiyo ya Chombo cha habari cha Global Times ilijigamba kwamba mfumo wa China wa Kisiasa , ulifanikiwa katika kukabiliana na Virusi vya corona.

Na Baadaye likaendelea kusema kwamba huu ndio wakati ambao mataifa ya Afrika yanapaswa kusitisha utumizi wa mfumo wa vyama vingi unaotumiwa na mataifa ya magharibi - mfumo ambao chombo hicho kinasema kwamba umesasabisha ukosefu wa usawa kikabila na kidin, ghasia uharibifu wa maisha na mali. Badala yake Afrika inapaswa kufuata mfumo wa chama kimoja wa China.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

China ni mwekezaji mkuu katika miradi ya ujenzi wa miundo mbinu Afrika

Muda mchache baadaye niliona taarifa nyengine katika gazeti jingine linalodhibitiwa na serikali ya China , China Daily , lililosifu mchango wa China kujenga barabara barani Afrika , uwekezaji mkubwa na mkakati ambao ulikuwa unaliponya bara hili kutokana na utumwa wa muda mrefu wa ukoloni mambo leo na sasa janga la virusu vya corona.

Jibu la bwana Pompeo kwa hilo lilikuwa wazi. Chama tawala cha China kilikuwa kinailimbikizia Afrika madeni kwa masharti ya kuvutia hatua ambayo itaathiri raia wa Afrika kwa kipindi cha muda mrefu.

Siku chache baadaye nilipiga simu na kujiunga katika majadiliano ya mtandao wa Zoom kuhusu uhusiano wa Marekani na China barani Afrika -ulioelezewa na wasimamizi wa mkutano huo kama makabiliano hatari - na kumsikiza profesa mmoja wa China akisema kwamba virusi vya corona vilikuwa vinasaidia waandishi wa Afrika kuelewa umuhimu wa waandish wa China waliodhibitiwa.

Vyombo vya habari vya magharibi vinaangazia mabaya, habari hasi, alisema professa Zhang Yanqiu, lakini wasomaji walitaka kupatiwa habari njema zaidi wakati wa mlipuko huu.

Ili kuelewesha , alimaanisha kwamba anataka mfumo wa uandishi wa habari wa China unaongazia mambo mema .

Alisema kwamba hivi karibuni alivutiwa na mfumo wa waandishi wa Ethiopia.

lakini je uandishi wa Afrika unashawishika kwa urahisi?

Nilipomuuliza bwana Pompeo iwapo anadhani kwamba sura ya Marekani barani Afrika imeharibiwa na matamshi ya hivi karibuni ya rais Trump kuhusu matumizi ya dawa za kuuwa vidudu na mwanga wa miale ya UV kutibu corona, waziri huyo wa maswala ya kigeni hakujibu moja kwa moja lakini akasema kwamba matamshi ya bwana Trump hayakueleweka na yalibadilishwa na vyombo vya habari vinavyodhibitiwa na serikali.

Ulikuwa muda usio wa kawaida katika mkutano huo wa zoom.

Reuters
Listening to Mr Pompeo, it suddenly felt like Beijing and Washington's views about 'constructive journalism' were no longer so far apart"
Andrew Harding
BBC Africa correspondent

Kwa miongo kadhaa diplomasia ya Maredkani imekuwa ikikuza na kulinda uhuru wa wanahabari Afrika dhidi ya uatawala wa kiimla na serikali zinazowadhibiti wanahabari.

Lakini sasa rais wa Marekani amekuwa akiwashutumu waandishi wa taifa lake kuwa feki, maadui wa watu na wasiofata maadili ya uandishi usiopendelea upande wowote.

Nikimsikikliza bwana Pompeo , nilihisi kwamba maoni ya Beijing na Washington kuhusu uandishi unaojenga hayana tofauti kubwa.

Trump 'anaeleweka vibaya'

Ni sawa kusema kwamba Marekani - kupitia mpango wa dharura wa rais wa zamani George Bush kuhusu msaada Pepfar umesaidia pakubwa kukuza afya barani Afrika.

lakini ni wazi kwamba China inatumia mlipuko wa corona na maovu yanayofanywa na Marekani ili kukuza ajenda yake ya kisiasa barani Afrika kwa ujasiri- nashuku na ufanisi.

Hio sio kusema kwamba kwamba mataifa ya Afrika - ama waandishi hutumika na mataifa yenye uwezo mkubwa.

lakini ni serikali ngapi barani Afrika, ambazo zinadaiwa na benki za China mbali na kuwa chini ya shinikizo la virusi vya corona zinaweza kujaribu kuufuta mfumo wa vyama vingi uliofeli na kuanza kutekeleza mfumo wa chama kimoja unaotumika na China?