George Floyd: Sanamu zilizotukuza biashara ya utumwa Marekani na Ulaya zaharibiwa

Defaced statue of King Leopold II in Antwerp, 5 June 2020

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Sanamu ya Mfalme Leopold II katika mji wa Antwerp ilichomwa moto na kupakwa rangi nyekundu

Sanamu ya mfalme wa Ubelgiji, ambaye chini ya utawala wake mamilioni ya watu waliuawa nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imeng'olewa katika mji wa Antwerp kufuatia maandamano ya Black Lives Matter.

Waandamanaji waliokuwa wakipinga ubaguzi wa rangi waliichafua sanamu hiyo ya mfalme Leopold wa pili kwa kuipaka krangi siku ya Jumatatu.

Wanaharakati nchini Ubelgiji wamekuwa wakitoa wito wa sanamu zinazotukuza kumbukumbu yake kuondolewa.

Mwandishi wa BBC alichapisha ujumbe wa Twitter wa sanamu hiyo ikiharibiwa mjini Antwerp Ubelgiji.

Mfalme huyo aliitawala Ubelgiji kuanzia 1865 hadi 1909, lakini anakumbukwa kwa uongozi wa kikatili DR Congo.

Mwaka 1885 hadi 1908 , mfalme huyo aliifanya DRC wakati huo ikijulikana kama taifa huru la Congo , koloni yake ya kibinafsi.

Aliibadilisha koloni hiyo kuwa kambi ya wafanyakazi, akijipatia faida kubwa kupitia biashara ya raba.

Wale waliokataa kushiriki katika biashara hiyo ya utumwa waliuawa kwa kupigwa risasi, huku wanajeshi wa leopold wakitakiwa kukusanya mikono ya waathiriwa wao.

Maelezo ya picha,

Mchoro ya Graffiti ilionekana katika sananu ya ukumbusho ya Melville

Wakati waandamanaji nchini England walipoangusha sanamu ya karne ya 17 kuhusu biashara ya utumwa katika maji ya kina kirefu ujumbe ulikuwa wazi.

Meli za Edward Colston zinaaminika kuwasafirisha wanaume, wanawake na watoto 80,000 kutoka Afrika katika mataifa ya America.

Lakini kumbukumbu hii imeheshimika kwa karne kadhaa katika mji wa nyumbani kwao wa Bristol , ambao ulifaidika kwa utajiri wake.

Huku serikali ikishutumu kitendo hicho siku ya Jumapili, waandamanaji walisema kwamba wanatumai kitaleta mabadiliko.

''Sanamu zina maana ya kwamba mtu huyo alikuwa mtu mzuri na alifanya vitu vikubwa. Hilo sio kweli, alikuwa mfanyabiashara wa biashara ya utumwa na muuaji'', alisema mwanahistoria David Olusoga akizungumza na BBC.

Maandamo yaliofanyika kote duniani, kama yale ya Bristol , yameangazia historia ya biashara ya utumwa na watu walioongoza biashara hiyo.

Sanamu katika mji mkuu wa Uskochi Edinburgh inayotoa kumbukumbu ya mwanasiasa ambaye alichelewesha kufutwa kwa bishara ya utumwa imepakwa rangi yenye maneno ya 'George Floyd' na 'BLM' (for Black Lives Matters).

Sanamu hiyo yenye urefu wa futi 150ft (46m) katika bustani ya St Andrew mjini Edinburgh ilisimamishwa mwaka 1823 ili kumkumbuka Henry Dundas.

Dundas alikuwa mwanasiasa aliyekuwa na ushahiwshi mkubwa katika karne ya 18 na 19 na alikuwa amepewa jina la utani ''mfalme asiye na taji ".

Aliwasilisha marekebisho ya muswada ambao ungesitisha biashara ya utumwa 1972, na badala yake akasema suala hilo linapaswa kufuatiliwa polepole.

Hatua hiyo iliruhusu biashara hiyo kuendelea kwa zaidi ya miaka 15 zaidi kinyume na ilivyotarajiwa.

Henry Dundas

Chanzo cha picha, PA Media

Maelezo ya picha,

Hatua ya Henry Dundas' ilihakikisha utumwa unaendelea kwa muda mrefu

Sanamu katika mji mkuu wa Uskochi Edinburgh inayotoa kumbukumbu ya mwanasiasa ambaye alichelewesha kufutwa kwa bishara ya utumwa imepakwa rangi yenye maneno ya 'George Floyd' na 'BLM' (for Black Lives Matters).

Sanamu hiyo yenye urefu wa futi 150ft (46m) katika bustani ya St Andrew mjini Edinburgh ilisimamishwa mwaka 1823 ili kumkumbuka Henry Dundas.

Dundas alikuwa mwanasiasa aliyekuwa na ushahiwshi mkubwa katika karne ya 18 na 19 na alikuwa amepewa jina la utani ''mfalme asiye na taji ".

Aliwasilisha marekebisho ya muswada ambao ungesitisha biashara ya utumwa 1972, na badala yake akasema suala hilo linapaswa kufuatiliwa polepole.

Hatua hiyo iliruhusu biashara hiyo kuendelea kwa zaidi ya miaka 15 zaidi kinyume na ilivyotarajiwa.

Robert E Lee

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Sanamu ya ukumbusho wa Robert E Lee mjini Virginia ilichorwa

Jimbo la Virginia nchini Marekani linaondoa sanamu ya Confederate ya jenerali Robert E Lee, ambayo imeharibiwa katika maandamano ya George Floyd.

Akitangaza uamuzi wa kuiondoa sanamu hiyo yenye tani 12 iliosimamishwa 1890, gavana Ralph Northam alisema: Hatuzungumzii tena uongo wa historia yetu.

''Sanamu hiyo imekuwepo katika eneo hilo kwa muda mrefu . Lakini ilikuwa makosa wakati huo na ni makosa wakati huu, Hivyobasi tunaiondoa''.

Ni miongoni mwa sanamu tano za Confederate katika barabara ya kumbukumbu, katika mji mkuu wa jimbo hilo wa Richmond, ambayo imepakwa maneno machafu wakati wa maandamano , ikiwemo ujumbe wa kusitisha ubabe wa watu weupe.

Robert Lee alikuwa kamanda wa jeshi lililokuwa likiunga mkono biashara ya utumwa.

Lee alifunga ndoa na mwanamke kutoka familia tajiri iliohusika na biashara ya utumwa mjini Virginia na kujiondoa katika jeshi hilo ili kuendesha mali ya familia hiyo kufuatia kifo babake mkewe.

Alipata pingamizi kutoka kwa watumwa waliotarajia kufunguliwa.

Nakala zinaonyesha kwamba alipendelea wafungwa waliotaka kutoroka kuadhibiwa vilivyo. Pia anadaiwa kuvunja familia za watumwa.

Wengi nchini Marekani wanamuona Lee kama ishara ya historia ya utumwa katika taifa hilo na ukandamizaji wa kibaguzi. Sanamu nyengine za Confederacy pia zimepakwa rangi na waandamanaji.

Baadhi ya wale wanaounga mkono sanamu hizo kusalia wanasema kwamba zinasimamia historia ya Marekani na tamaduni za kusini.

Winston Churchill

Chanzo cha picha, PA Media

Maelezo ya picha,

Sanamu ya Winston Churchill mjini London wilipulizwa maneno "alikuwa mbaguzi"

Sanamu ya aliyekuwa waziri mkuu wa zamani mjini Londonwa Uingereza Winston Churchill iliharibiwa kwa kupakwa maandishi machafu kwa kuitangaza kuwa ya kibaguzi.

Churchill anapongezwa kwa kuongoza Uingereza kupata ushindi katika vita vya pili vya dunia.

Ameelezewa katika tovuti ya serikali ya Uingereza kama kiongozi aliyewavutia wengi , mwandishi, msemaji na kiongozi.

Na alichaguliwa kuwa Muingereza mwenye umaarufu mkubwa zaidi katika kura ya BBC iliofanyika 2002. lakini kwa wengine anasalia kuwa mtu aliyezongwa na utata kutokana na maoni yake ya kibaguzi.

''Bila shaka hakuna wasiwasi kwamba Churchil alikuwa mbaguzi'', alisema mwanahistoria Richard Toye , mwanzilishi mwenza wa kitabu kinachotarajiwa kuzinduliwa The Chuirchil Myths.

''Aliwataja watu weupe kuwa juu zaidi ya wengine. Alitoa matamshi yasiofurahisha kuhusu Wahindi aliosema ni watu wanyama walio na dini ya kinyama, mbali na kutoa matamshi ya chuki dhidi ya Wachina''.