Virusi vya corona: Kwanini Wakenya wanamuomba Rais Kenyatta kuwapatia 'uhuru' ?

Ramadhan Issa, a Muslim motorbike taxi rider, waits for customers after performing the Eid al-Fitr prayers, marking the end of the holy fasting month of Ramadan, amid concerns about the spread of the coronavirus disease (COVID-19), in Nairobi, Kenya, May 24, 2020

Chanzo cha picha, Reuters

Katika mfululizo wa barua kutoka kwa waandishi wa habari wa kiafrika, Joseph Warungu amepata hisia kali za wakenya ambao wamekuwa wakiiomba serikali kupunguza makali ya hatua zinazochukuliwa kukabiliana na kusambaa kwa ugonjwa wa Covid-19.

''Rais , tunakuomba-tafadhali, tafadhali tuache huru!''

Haya si maneno ya watu wanaoshikiliwa au kuwa kwenye karantini ya lazima baada ya kukamatwa na polisi kwa kutovaa barakoa.

Badala yake, ni kilio cha wakenya wengi ambao hawawezi kuvumilia tena masharti ya kutotoka nje.

Kabla Rais Uhuru Kenyatta kulihutubia taifa siku ya Jumamosi, mitandao ya kijamii ilijaa ujumbe wa maneno wa kufurahisha na video kumsihi kupunguza makali ya hatua ya za kusalia majumbani.

Moja kati ya ujumbe uliosambazwa ni wa video ya kiswahili iliyotengenezwa na mchekeshaji Mtume Orroson ikimuonesha akifanya mazungumzo na rais- kwa kutumia sauti za zamani za Bwana Kenyatta lakini nje ya muktadha.

Mchekeshaji: Uhuru, lini utatuweka huru?

Rais : Baada ya wiki tatu...

Mchekeshaji: Haya ni makosa....umetuzuia kutembea usiku kisha ukatuma polisi kutupiga.

Rais: Si mimi... sijamuagiza yeyote...

Mchekeshaji: Unaweza angalau kufungua vilabu tu- kwa siku moja tu niweze kutakasa koo langu kwa bia moja. Nitafanya nini kama vilabu vyote vitafungwa?

Rais: Tumia mlango wa nyuma...

Mchekeshaji: Weee! itakuwaje kama askari wako wakinikamata?

Rais: Itakupasa ujitetee....na hawa watu hawana masihara!

Watu wengi wamejikuta katika mazingira magumu ya kuwa ndani usiku, sharti la kutotoka au kuingia kutoka na kwenda kwenye nchi nyingi, ikiwemo jijini Nairobi, na kufungwa kwa shule, vilabu na baa na maeneo ya kuabudu.

Watu karibu milioni 1.2 wamepoteza ajira zao tangu kuingia kwa janga nchini Kenya, wengine wengi wakikatwa mishahara. Biashara nyingi zimefungwa na familia zinapata changamoto ya kujikimu.

Getty Images
When we decide to sell the food, let's sell it at a very high price - hit them hard"
John Magufuli
President of Tanzania

Rais wa Tanzania, John Magufuli -aliyekataa kuweka masharti ya kusalia nyumbani, alitoa kauli zilizosababisha mjadala kuhusu mwenendo wa virusi kuwa anaamini ugonjwa wa corona umekwisha kwa uwezo wa Mungu- hivi karibuni aliwaambia Watanzania- ''Baadhi ya watu wanakabiliwa upungufu wa chakula kwa kuwa walijifungia ndani wakati tukilima.

''Sasa tukilinde chakula chetu. Na tukiamua kukiuza chakula, tukiuze kwa bei ya juu- tupige bei kweli kweli! ninasema tuwapige kweli kweli!''

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Uchumi wa Kenya umeyumba kwa sababu ya masharti ya kutotoka nje

Watu wengi nchini Kenya walikuwa na matumaini kuwa Rais Kenyatta atafungua milango kwenye sekta muhimu za kiuchumi wikiendi iliyopita.

Lakini kuchagua njia ya tahadhari, Bwana Kenyatta alipunguza muda wa kuwa nje kutoka saa 10 mpaka saa saba na kupunguza makali ya masharti ya kutembea katika baadhi ya maeneo.

Rais alionekana usiku

Hatahivyo, sekta ambayo imehuishwa haraka, kiasi cha kuwaudhi watu wengi ni siasa, huku Wakenya wakishuhudia matukio ya kushangaza juma lililopita.

Picha ya video ya CCTV ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mahasimu wa zamani Bwana Raila Odinga (kulia) na Kenyatta (kushoto)

Iliwaonesha wanaume wawili ambao kwa ukaribu wanafanana na Bwana Uhuru Kenyatta na Waziri Mkuu wa zamani na kiongozi wa upinzani, Raila Odinga wakitoka ndani ya gari usiku kutazama kazi ya ujenzi wa barabara iliyokuwa ikiendelea katika barabara ya Kenyatta jijini Nairobi, karibu na ofisi ya rais.

Gari iliyokuwa imewabeba ilikuwa imesindikizwa na msafara mdogo ulikuwa na magari kadhaa aina ya SUV na polisi waliokuwa na silaha nzito.

Waziri Mkuu wa zamani si miongoni mwa watu walio kwenye kundi la wafanyakazi muhimu wanaopaswa kuwa na barua kuonesha polisi kuwa anaruhusiwa kutoka nje usiku.

Tukio hili lilionekana kuwa ishara ya kuwa shughuli za kisiasa zinaanza, pamoja na masharti ya kutotoka nje.

Chanzo cha picha, AFP

Tangu katikati mwa mwezi Machi Kenya iliporipoti mgonjwa wa kwanza wa virusi vya corona, wanasiasa wamekuwa wakijifichwa nyuma ya barakoa na sauti zao kuzimwa kutokana na dharura ya kiafya iliyoikabilili Kenya.

Mazishi ambayo wanasiasa walitumia kama majikwaa ya kujijengea sifa, yamekumbwa na masharti makali yaliyowekwa na serikali ili kudhibiti maambukizi ya Covid-19.

Lakini mwezi uliopita, siasa zimeibuliwa. Hii ni kwasababu kuwa Bwana Kenyatta ana haraka. Anatakiwa kuondoka madarakani mwaka 2022, na anataka kulinda hiba yake kama mshindi katika masuala ya kulileta taifa pamoja na maendeleo.

Bwana Kenyatta na Odinga wamekuwa wakifanya kazi pamoja tangu tukio la kihistoria la kupeana mikono mwezi Machi mwaka 2018 kumaliza mzozo na vurugu za wakati wa chaguzi zilizotokea wakati watu hawa wawili walipokuwa wakiwania nafasi ya juu ya uongozi.

Naibu Rais William Ruto ana hofu kuwa mahusiano haya ya karibu yanaweza kuharibu juhudi zake za kumrithi Kenyatta.

Matokeo yake rais amechukua hatua za kuwaondoa katika nafasi muhimu wanasiasa walio na ushirika na Ruto, akiwashutumu kupinga ajenda za serikali

Joseph Warungu
Joseph Warungu
Many are hoping that politicians will continue to mask their mouths and keep a distance even after Covid-19 is tamed"
Joseph Warungu
Journalist

Jitihada za Bw Kenyatta za kuendelea kuilinda hiba yake zimesababisha shutuma kuwa anadhoofisha uhuru na uhuru wa bunge na mahakama.

Siku ya Jumatatu, Jaji Mkuu David Maraga alijitokeza na kupaza sauti yake kwa wale wanaosisitiza kumtaka Rais Kenyatta 'tuweke huru'.

Akikosoa ofisi ya rais kwa kutotii maagizo ya korti na kutenda kinyume na katiba, alisema: "Itakuwa dharau ya jukumu langu ikiwa sitaongeza Wanjiku [kumbukumbu ya raia wa kawaida] kwenye kikoa changu."

Akikosoa ofisi ya rais kwa kukiuka amri ya mahakama na kutenda kinyume cha katiba.

Wakati haya yakiendelea, idadi ya watu wanaokutwa na maambukizi ya virusi vya corona imeendelea kuongezeka nchini Kenya.

Serikali imesema kuwa inawezekana mwezi Agosti au Septemba nchi hiyo ikashuhudia wagonjwa mpaka 200 kwa siku.