Virusi vya corona: Asiyeonesha dalili za kuwa na virusi anaweza kuambukiza wengine?

Virusi husambazwa baada ya kutolewa kwa matone madogomadogo ya mate ya mtu aliye na virusi anapokohoa bila kufunika mdomo

Chanzo cha picha, Getty Images

Ni kiasi gani cha maambukizi ya virusi vya corona kinatoka kwa watu ambao hawana dalili za virusi hivyo licha ya kwamba wana corona, bado takwimu hiyo haifahamiki, wanasayansi wa shirika la afya duniani wamefafanua.

Dr Maria Van Kerkhove anasema huwa si rahisi kwa mtu ambaye ana virusi vya corona lakini hajaonesha dalili kuweza kuambukiza ugonjwa huo kwa watu wengine.

Lakini utafiti huu unategemea kiwango kidogo cha utafiti uliofanyika.

Kuna ushahidi unasema kuwa watu wenye virusi vya corona wanaoonesha dalili ndio wenye maambukizi makubwa zaidi lakini ugonjwa unaweza kupita tu .

Hata hivyo idadi ya watu waliopimwa bila kuwa na dalili haijajulikana watu hawa wameweza kuambukiza watu wengine.

Dr Van Kerkhove alisema amekuwa akijadiliana na nchi ambazo zilifanya tafiti kupata maelezo zaidi kuhusu utafiti huo.

Ukiangalia uchunguzi ambao umefanywa katika upande wa maambukizi ya mataifa mbalimbali . Alisema watu ambao hawakuonesha dalili ni ngumu sana kujua wameambukiza watu kiasi gani kati ya wale waliokutana nao.

Lakini bado ana swali kubwa ambalo halina jibu kuhusu uchunguzi huo kama ni kweli ,kwa dunia nzima.

Hofu yake inajumuisha msisitizo wa umuhimu wa watu kuchukua hatua za kukaa ndani imeweza kupunguza idadi ya watu ambao wanaweza kuambukizwa kwa wingi," alisema Prof Liam Smeeth, mtaalamu wa masuala ya usafi na afya katika shule moja mjini London.

Anasema ameshangazwa na maelezo ya shirika la afya duniani WHO lakini hajaona takwimu ambazo wametumia.

Maelezo ya video,

Coronavirus: Utajuaje kuwa umeathirika na virusi?

Mkurugenzi wa mpango wa dharura wa afya wa WHO, Dr Michael Ryan, alisema alikuwa anahisi kabisa kuwa kuna watu wanapata maambukizi bila kuonyesha dalili na kuwaambukiza wengine, lakini swali linabaki pale pale ni kwa kiasi gani?

Dr Van Kerkhove, ambaye ni kiongozi wa WHO katika kitengo cha magonjwa ya dharura, ameweka utofauti katika vipengele vitatu.

  • Watu ambao hawaonyeshi dalili
  • Watu ambao wanaweza kupima na kukutwa na virusi wakati ambao hawana dalili lakini kadri siku zinavyokwenda, wanapata dalili za ugonjwa huo
  • Watu ambao wana dalili kidogo za ugonjwa lakini hawatambui kuwa na virusi vya corona.

Baadhi ya ripoti zimetofautisha aina hizo wengine wakisema wale ambao wako na dalili na wale ambao hawana, ingawa bado ni kundi dogo limefanyiwa utafiti na hivyo kuwawia vigumu kusema jibu ni lipi.

Lakini Dr Van Kerkhove alisema ,ukubwa wa ushahidi wa utafiti wa watu ambao hawajawahi kuwa na dalili haijaongeza maambukizi kusambaa zaidi katika sehemu ambazo utafiti ulifanyika.

Utafiti ambao uliangalia sampuli za watu ambao wana maambukizi bila dalili na vilevile kufuatilia watu waliohusiana nao, wameona kuwa walioambukizwa kutokana na wao ni wachache.

Hii imesababisha muongozo wa WHO, wa watu kuvaa barakoa ambao ulichapishwa mwishoni mwa wiki kuhitimisha kuwa watu ambao wana virusi vya corona lakini hawana dalili wanaweza kuambukiza watu wengine kwa, kiwango kidogo.

Nchini Uingereza, afisa wa takwimu za taifa (ONS) amekuwa akipima mara kwa mara sampuli za watu katika maeneo tofauti.

Wamebaini kuwa , wale ambao mpaka sasa wamepimwa Covid-19, ni 29% pekee ndio wameripotiwa kuwa hawana dalili za ugonjwa huo wakati wanapimwa na hata walivyopimwa kabla au kupimwa hata mara tatu.

Watu wenye dalili za virusi ndio walio kwenye hatari

Katika kufuatilia utafiti uliofanywa katika baadhi ya nchi umeeleza kuwa ni kweli kwamba watu ambao hawaoneshi dalili huwa ni nadra sana kuambukiza wengine, maambukizi yanatokea kabla au siku ambayo dalili zinapoanza kuonekana kwa mara ya kwanza hata kama ni kidogo sana kwa mujibu Prof Babak Javid, mshauri wa tiba ya magonjwa ya kuambukiza katika chuo kikuu cha Cambridge.

Watu wamebainika kuwa na virusi hivyo kuwa watu wasioonesha dalili wanaweza kuonekana kuwa na dalili siku tatu hivi kabla ya kuambukiza wengine haswa huwa siku moja kabla au siku moja baada ya dalili kuanza kuonekana.

Hatua za awali ni muhimu kuchukuliwa hatua kwa mtu kujitenga na wengine alisema Prof Javid.

Mtu ambaye hajawahi kupata dalili anaweza asipitie hatua zote za dalili ya ugonjwa..

Wakati watu ambao hawana dalili wanaonekana kuwa hawako kwenye hatari ya kuambukiza wengine huku utafiti wa sasa unaonesha kuwa watu wenye dalili za virusi vya corona wako kwenye hali ya hatari zaidi.

Aidha kuambiwa tu kuwa una virusi vya corona haimaanishi kuwa una virusi kiasi gani. Kile kinachofahamika ni ugonjwa wa kuambukiza - labda pale mtu anapopiga chafya na anakohoa na kuchangamana na wengine wanaweza kuambukiza wengine kirahisi zaidi.

Dr Van Kerkhove ameeleza kuwa ugonjwa huu zaidi unaambukiza kirahisi zaidi kupitia matone madogo pale mtu anapokohoa au kupiga chafya.