Jinsi filamu za Michelle Obama na Hillary Clinton zinaweza kutia moyo wanawake vijana

Michelle Obama and Hillary Clinton

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Wake wa waliokuwa maraisa: Michelle Obama na Hillary Clinton

'Becoming', moja ya filamu katika mtandao wa Netflix kuhusu Michelle Obama, ikiwa ni yenye kutazamwa na wengi baada ya kupeperushwa wiki chache zilizopita. Na sasa hivi, mwanamke mwingine Mmarekani, Hillary Clinton pia nae kuna filamu inayoangazia maisha yake.

Filamu hiyo ya saa nne yenye mahojiano ya Clinton na mwelekezi wa filamu na vipindi vya kwenye runinga Nanette Burstein, inaonesha maisha yote ya Hillary Rodham Clinton kuanzia yeye kuwa mwanaharakati 1960, ndoa yake na aliyekuwa rais wa Marekani Bill Clinton, hasa wakati wa ile sakata ya Monica Lewinsky na vilevile, hatua yake ya kuwania urais wa Marekani 2016, ambayo haikufanikiwa.

Hillary anaonesha nadharia ya kwamba kizazi kijacho cha viongozi wanawake walichochewa na kushindwa kwake uchaguzini, katika kupiga kura, na uchaguzi wa bunge la Congress 2018; kukiwa na rekodi iliyovunjwa ya wanawake 103 wakiwemo wanaharakati kama vile Alexandria Ocasio-Cortez, kuchaguliwa au kuchaguliwa tena katika bunge la wawakilishi.

"Najua ninachomaanisha kwa wanawake wengi, nalisikia karibu kila siku, kuna mtu atakayeniambia," Clinton ameliambia shirika la BBC News. "Ni jukumu kubwa."

"Nimejitahidi kufanya maamuzi yangu mwenyewe kama mimi na kusimamia kile ninachoamini, lakini bado tunahitaji wale wakuwaiga, kuwa kama mwongozo, 'ikiwa huyu anaweza kufanya, mwengine pia anaweza kufanya' - fikra kama hizo. Hilo nalifahamu."

Chanzo cha picha, Propagate

Filamu ya Becoming, pia inamuonesha Michelle Obama kama ilivyo kwa kitabu chake kinachouzwa kwa wingi kimataifa, pamoja na yeye kukutana na wanawake vijana Wamarekani weusi kuwahamasisha kutimiza ndoto zao.

Kulingana na mwelekezi wa filamu, Nadia Hallgren, "hakuwahi kukutana na nguvu ya aina hiyo hapo kabla."

"Kile ambacho wanawake wanaweza kuelewa na kushirikisha hisia za wengine," Hallgren aliongeza, "Ilikuwa ni simulizi yake ya kuambiwa huwezi kufanya kitu au kudunishwa katika maisha yake yote. Hili wazo la kwamba ikiwa wewe ni mwanamke, ikiwa wewe si mwanamume, ikiwa wewe sio mzungu, kama wewe haupo kwenye kundi hilo, basi huwezi."

"Nafikiri kwamba kuna uhitaji mkubwa wa simulizi kama yake kote duniani. Kumsikiliza Bi Obama akizungumzia vikwazo alivyokumbana navyo maishani mwake, na kuweza kutafakari hayo sasa, kulinifunza mengi kuhusu maisha yangu na vikwazo ambavyo nimekumbana navyo."

Nanette Burstein, mwelekezi katika filamu ya Hillary, anakubali kwamba uwezo wa kuona mbele kwa waliokuwa wake wa marais ni muhimu hasa kwa vijana.

"Nilipokuwa katika miaka yangu ya 20, na kutaka kuwa mkurugenzi, Bi. Clinton alikuwa anaanza kushikilia wadhifa huo kama mke wa rais - na kama mke wa rais tofauti kabisa, ambaye angeweza kuchukua uongozi wa masuala muhimu kama vile afya. Kwangu kama mwanamke kijana, hili lilinitia moyo na kubadilisha maisha yangu.

"Moja ya sababu iliyopelekea mimi kusema hayo ni ili watu waweze kuelewa hilo lina maanisha nini kwa wanawake vijana."

Chanzo cha picha, Netflix

Maelezo ya picha,

Mara nyingi Michelle Obama amekuwa akijielezea kuwa yeye ni bingwa wa "kukumbatia" [picha hii ni kabla ya kutokea kwa mlipuko wa virusi vya corona.

"Pia inafurahisha zaidi kujua kwamba filamu hizo za wake wa waliokuwa marais zinatengenezwa na mwanamke," Mia Bays anasema, mkuu wa Birds Eye View, shirika lisilo la kifaida ambalo limejikita katika kuangazia masuala ya wanawake kwenye sekta ya filamu.

"Nafkiri katika filamu ya Becoming inatusaidia kuanza kuakisi kwa nini Michelle Obama ni kiungo muhimu katika kutia watu moyo na kuzingatia umuhimu wa suala hili kuangaziwa zaidi hasa wakati huu."

Chanzo cha picha, NETFLIX

Maelezo ya picha,

Michelle Obama alifanikiwa kusafiri maeneo mbalimbali kama njiamoja ya kuhamasisha wengine yalyyomo kwenye kitabu chake

Tofauti, Hillary Clinton amekuwa akionekana kama mwenye historia ya kugawanya watu - 2016, kura ya maoni kuhusu uchaguzi iliyoendeshwa na Edison ulionesha kwamba ingawa asilimia 52 ya wanawake walikuwa wamemchagua Clinton, asilimia 64 ya wanawake wazungu ambao hawakupata masomo ya juu walipiga kura kumchagua Trump.

Clinton anasema anajua kwamba kuna wale wasiompenda.

"Ni jambo jema kupendwa, lakini ikiwa hilo tu ndio unataka, hautakuwa hapo kwa sababu stahiki. Kuna matukio katika filamu hii ambayo hata nilikuwa nimeyasahau.

"Ninapigania afya njema, na watu walikuwa wanachoma sanamu yangu. Watu walishikwa na hasira, hawanipendi na hawakupenda kile kinachoendelea. Mara nyingi ikiwa haupendwi, ni kwasababu unachukua msimamo.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Hillary Clinton wanahitaji kuendelea kupewa moyo katika suala la uongozi

"Wakati mwanamke anapokuwa na msimamo wake katika suala linaloangaziwa na wengi kwenye jamii na lenye kuleta utata lazima ujitayarishe kukashifiwa la sivyo, usidhubutu kuchukua msimamo wako hadharani," anasema. "Najivunia kazi ambayo nimefanya na misimamo ambayo nimechukua, na sijutii lolote kuhusu hilo."

Clinton anakubali kwamba filamu hiyo ni njia moja ya kuweka mambo wazi".

"Kuna taarifa nyingi kunihusu mimi, simulizi nyingi za kustaajabisha kunihusu mimi - maisha yangu kuoneshwa kwa namna ambayo ninajua ni hatua nzuri ya kusonga mbele," anasema.

Lakini je filamu kama hizi zinaweza kuwa zisizopendelea upande wowote? Filamu ya Becoming ilitenegnezwa na kampuni ya Obama ya kutengeneza filamu ya Higher Ground.

'Huwezi kutulia'

"Naelewa kwamba ninaweza kukosolewa kwa jinsi nilivyoelezea simulizi ya filamu hii," Nanette Burstein amejibu. "Nilijua kwamba chochote kile ambacho ningefanya, kungekuwa na ukosoaji. Kwahiyo nilihisi kwamba nahitajika kufanya utafiti mzuri kadiri ya uwezo wangu na kuwa mkweli niwezavyo."

Clinton hakubali kwamba wanawake bado wanahitaji kutiwa moyo katika uongozi - ama kupitia vyombo vya habari, katika sekta ya kiviwanda au kwenye siasa.

"Nafikiri kwa kushirikisha wengine simulizi yangu, unaweza kuona mabadiliko mengi lakini kuona changamoto zilizopo unaweza kuona," anasema.

"Unaweza usipumzike na pia inachosha kuwa mkweli. Ni kama, subiri kidogo, tumevunja kizuizi hicho na kubadilisha sheria hiyo - kwanini hilo bado ni suala gumu? Kwanini hakuna watu wanaokubali au kuheshimu wanawake na fursa walizonazo kuchangia?

"Kwanini unajua, bado mapambano yanaendelea."