Mtoto akutana na wazazi wake miezi 10 baada ya kuzaliwa

Mtoto akutana na wazazi wake miezi 10 baada ya kuzaliwa

Nchini Ukraine, juhudi zinaendelea za kukutanisha watoto wachanga waliozaliwa na kina mama wa kukodi na wazazi wao wa kibaolojia yaani wazazi halisi. Mwezi uliopita, maafisa walisema kwamba zaidi ya watoto mia moja katika mji wa Kyviv hawajui hatma yao baada ya hatua zilizochukuliwa kama njia ya kuzuia maambukizi ya virusi vya corona ambazo zinazuia wazazi wao halisi kote duniani kufika nchini Ukraine na kuwachukua. Lakini sasa hivi baadhi ya masharti hayo yameanza kupunguzwa na ndege maalum kuanza kuruhusiwa kufanya safari. Mwanahabari wa BBC Johan Fisher alizungumza na baadhi ya wanandoa ambao hatimae wamefanikiwa kufika Kyiv kukuna na kijana wao aliyezaliwa miezi kumi iliyopita.