Waandamanaji wakabiliana na polisi mjini London

Flares and smoke bombs have been thrown in Trafalgar Square

Chanzo cha picha, Reuters

Polisi walishambuliwa kwa chupa wakati wa makabiliano kati yao na mamia ya waandamanaji mjini London, ambao walipuuza agizo la kutoshiriki maandamano.

Makundi ya watu yalikusanyika katikati ya mji mkuu,wakidai kuwa wanalinda sanamu dhidiya wanaharakati wanaopinga ubaguzi wa rangi.

Maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi pia yamefanyika katika miji tofauti nchini humu ikiwa ni pamoja na mii wa London.

Polisi wameweka masharti dhidi ya makundi kadhaa, kufuatia vurugu mbaya zilizoshuhudiwa wikendi iliyopita.

Makundi kadhaa kutoka sehemu tofauti nchini, pamoja na wanaharakati wa mrengo wa kulia, yalisema yamekuja mjini London kulinda alama ya historia ya Uingereza.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Mamia ya watu wengi wao wazungu walikusanyika katika ukumbi wa ukumbusho wa Cenotaph katika eneo la Whitehall amble linapakana na sanamu ya Winston Churchill iliyopo karibu bunge.

Mamia ya watu wengi wao wazungu walikusanyika katika ukumbi wa ukumbusho wa Cenotaph katika eneo la Whitehall amble linapakana na sanamu ya Winston Churchill iliyopo karibu bunge.

Makabiliano yameripotiwa kati ya polisi na waandamanaji ambao walikuwa wakisema kwa pamoja "England" huku wakiinua mikono yao kuelekea walipo maafisa wa polisi.

Baadhi yao walifanikiwa kuvunja uzio wa chuma unaozunguka Cenotaph katika eneo la Whitehall na kuanza kuwarushia polisi milingoti ya umeme na vifaa vingine walipokuwa wakijaribu kuwadhibiti.

Waadamanaji hao baadae walielekea Trafalgar Square, ambapo walianza kurusha fataki kuelekeakwa makundi ya yatu.

Polisi walikuwa na kibarua kigumu kuwazuia wasifike katika bustani ya Hyde Park ambako kulikuwa na mandamano ya amani ya watu wanaopinga ubaguzi wa rangi.

Wasimamizi wa vugu vugu la Black Lives Matter walikuwa wametoa kwa watu kutoshiri maandamano ya kupinga ubaguzi yaliyopangwa wikendi hii kwa kuhofia huenda yangegongana na makundi ya marengo wa kulia.

Chanzo cha picha, PA Media

Maelezo ya picha,

Polisi wakikabiliana waandamanaji nje ya bunge

Chanzo cha picha, Getty Images

Akitumia kanda ya video inayoonesha makabiliano kati ya polisi na waandamanji hao kwenye Twitter, Waziri wa ndani Priti Patel alisema ni "ujambazi usiokubalika".

"Mtu yeyote atakaye chochea vurugu ama kuharibu mali atachukuliwa hatua kali za kisheria ," aliandika.

"Ukatili dhidi ya maafisa wetu wa polisi hautavumiliwa."

Chanzo cha picha, AFP

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Maandamano huko Newcastle

Chanzo cha picha, PA Media

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mijini Glasgow

Sanamu ya Churchill imekingwa kwa kuhofia isiharibiwe , baada ya waandamanaji kusema kuwa inaashiria ''ubaguzi wa rangi'' katika maandamano ya wikendi iliyopita.

Mamia ya watu pia walikusanyika katika miji ya Glasgow, Bristol na Belfast Kama sehemu ya mpango wa ''kulindaa'' historia.

Maandamano kadhaa ya kupinga ubaguzi wa rangi pia yameandaliwa katika maeneo tofauti Uingereza, ikiwemo Brighton, Newcastle,

Maelezo ya video,

Umeshawahi kujiuliza kama sanamu zinastahili kuwepo?