Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 15.06.2020: Grealish, Sancho, Aubameyang, Alonso, Havertz, Ndidi

Aston Villa celebrate

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Jack Grealish (kulia) aliwahi kuchezea Ireland katika timu za U17, U18 na U21

Manchester United itaongeza jitihada kuhakikisha inamsajili kiungo wa kati Jack Grealish, 24, kwa kitita cha pauni milioni 75 baada ya kuambiwa wamsubiri kwa miezi 12 mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Jadon Sancho, 20 (Daily Star)

Tottenham Hotspur, West Ham na Chelsea wanamtaka mlinda mlango wa Uhispania Pau Lopez. Roma itamuuza mchezaji huyo, 25 kwa kitita cha pauni milioni 36 (Estadio Deportivo-in Spanish)

Newcastle United wana mpango wa kumnasa mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa Chelsea Marcos Alonso .Mustakabali wa mchezaji huyo, 29, ndani ya kikosi hicho ukiwa bado haujulikani huku Chelsea ikihusishwa na taarifa za kupata mchezaji wa nafasi ya ulinzi Leicester Ben Chilwell,23. (Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Havertz alipata goli baada ya kupata penalti, mbele ya wachezaji wa Borussia Monchengladbach

Chelsea wako tayari kutoa ofa ya pauni milioni 75 kwa ajili ya Kai Havertz, lakini Bayer Leverkusen wamesema thamani ya kiungo huyo wa kati ni pauni milioni 90. (Express)

Manchester United imemuongeza kiungo wa Leicester Wilfred Ndidi , 23, katika orodha yao ya uhamisho, huku Real Madrid na Paris St-Germain pia wakimtolea macho Mnaijeria huyo. (Express)

Arsenal wamedokezwa kumsajili kiungo Thomas Partey wa Ghana na klabu ya Atletico Madrid imekubali kumruhusu mchezaji huyo, 27, kuondoka kwenye klabu hiyo. (COPE, via Caught Offside)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang

Pierre-Emerick Aubameyang, 30, amesema uamuzi wa kujiunga na Arsenal ''inawezekana ukawa uamuzi bora'' kuufanya katika maisha yake ya kazi ya soka. (Telefoot-in French)

Arsenal pia ina nia ya kumsajili Axel Disasi, 22, wa Reims na mwenzake wa nafasi ya ulinzi Dayot Upamecano, 21, ambaye huenda akawa ghali kumnunua kutoka RB Leipzig ( Goal via Express)

Chelsea pia inafikira uhamisho wa mlinda mlango wa Southamptons Fraser Forster, 32. (Football Insider)