Diamond Platnumz analinganishwaje na nyota wengine wa Afrika katika mtandao wa YouTube?

Diamond Platnumz akishangazwa na wazalishaji wake wa muziki nyumbani kwake

Chanzo cha picha, wcb_wasafi

Diamond Platinumz alishangazwa na wazalishaji wake wa muziki mwaka 2020 walipoingia katika nyumba yake na keki iliokuwa na nembo ya kuadhimisha hatua muhimu ya nyota huyo wa Tanzania.

Huku akipigwa picha akivalia nguo , mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 30 aliambiwa na kundi lake kwamba ndiye msanii wa kwanza katika jangwa la sahara kupata views bilioni moja katika chaneli ya Youtube.

Katika kipindi cha miaka 10 iliopita, mwanamuziki huyo alieshinda mataji kadhaa amekuza muziki wa bongo fleva kuwa maarufu - muziki wa kipekee wa Tanzania unaotoa nyimbo za kimapenzi zilizochanganywa na midundo ya kisasa inayotokana na muziki wa jadi wa taarab kutoka pwani ya Afrika.

Diamond Platinumz ni mwanamuziki alie na bidii na maonyesho yake huvutia mashabiki wengi, kulingana na DJ Edu, ambaye amekuwa mtangazaji wa kipindi cha runinga cha kila wiki cha muziki wa Afrika cha BBC.

Huku akiwa na asilimia 43 ya mashabiki miongoni mwa raia milioni 55 nchini Tanzania wanaoweza kuingia katika mtandao, kupitia simu aina ya smartphones, kuna mashabiki wengi wanaopenda muziki wa bongo fleva walio tayari kusikiliza muziki wake wa mapenzi.

Wanamuziki wengine kama Harmonize pia nao wamebobea katika YouTube.

Je Views bilioni moja ni nyingi kiasi gani katika YouTube?

Ni vigumu kubaini umuhimu hasa wa nambari bilioni moja , ikizingatiwa kwamba Diamond Platinumz ana wafuasi wengi katika mtandao wa Instagram ikilinganishwa na wafuasi wake katika YouTube ambao ni milioni 9.7 ikilinganishwa na milioni 3.7.

DJ Edu anasema kwamba Instagram ni mtandao wenye ushawishi mkubwa kuhusu mtindo wa maisha na majukwaa mengine kama vile TikTok , ambayo inaruhusu sekunde 30 za hakimiliki ya utumizi wa bure wa nyimbo - ni njia nzuri ya kuwanasa wafuasi vijana.

''Nyimbo nyengine zinasambaa sana kupitia TikTok , kama wimbo mpya wa Diamond Platinumz kwa jina Quarantine'', anasema

''Hii inaweza kuwavutia wafuasi katika mtandao wa YouTube , ambapo fedha zinaweza kupatikana kupitia matangazo.

Muhumu zaidi kwa wanamuziki barani Afrika , katika muongo mmoja uliopita YouTube imewaruhusu kuingia moja kwa moja kupata mashabiki , badala ya kutegemea stesheni za runinga.

Je analinganishwaje na nyota wengine wa Afrika?

Diamond Platnumz bado yuko nyuma ya wanamuziki wengine wa eneo la Afrika ya kaskazini ambao wana mashabiki wengi katika eneo la mashariki ya kati.

Na vilevile kuna wasanii wanaoishi Afrika kama mwanamuziki aliyezaliwa Mali Aya Nakamura , ambaye anampiku mwanamuziki huyo wa Tanzania kwa Views zaidi ya bilioni 1.7 katika YouTube

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Aya Nakamura alijipatia umaarufu wake kupitia wimbo wake Djadja

Msichana huyo alielekea Ufaransa wakati alipokuwa msichana mdogo na kujipatia umaruufu mkubwa kupitia wimbo wake wa 2018 Djadja.

Na Akon mwanamuziki wa Senegal aliyebadilika na kuwa Rappa wa Marekani anawashinda wote kwa Views bilioni 3.5.

Katika Afrika ya jangwa la sahara, washindani wa Diamond Platinumz katika mtandao wa You Tube ni wasanii wa Nigeria.

  • P Square - 810 million
  • Davido - 618 million
  • Flavour - 617 million
  • Tekno - 574 million
  • Burna Boy - 507 million
  • StarBoy TV (AKA Wizkid) - 480 million

Takwimu za wasanii Davido na Burna Boy ndio zinazovutia zaidi ikizingatiwa kwamba walifungua chaneli zao za YouTube mwaka 2018.

Diamond amekuwa katika ukumbi huo tangu 2011.

Maelezo ya video,

Nyota wa Nigeria Wizkid

Na kampuni ya kurekodi muziki ya Wizkid , StarboyTV - unapoongezea takwimu kwa chaneli zake nyengine ana takriban Views Milioni 802.

Nyota wengine hupendelea kuwa na chaneli zao wenyewe ili kukuza nyimbo zao na kuondoa urasimu kwa kuwa kampuni nyingi za muziki huchukua muda mrefu kutoa nyimbo mpya.

Majina mengine maarufu ni Magic System ya Wizkid .

Nyota wengi hupendelea kumiliki chaneli zao wao wenyewe ili kukuza nyimbo zao na kupunguza urasimu kwa kuwa kampuni hizo za kurekodi muziki huchukua muda mrefu kutoa nyimbo mpya. Kampuni nyengine maarufu ni Magic System ya Ivory Coast ilio na zaidi ya views milioni 477.

Kundi hilo ni maarufu hususan katika maeneo ya magharibi mwa Afrika ambapo wenyeji huzungumza Kifaransa.

Ufuasi huu unatokana na wimbo wao Gaou- ni wimbo mmoja ambao umefanikiwa kuliunganisha bara zima , kulingana na DJ Edu.

Huku takwimu za chini za You Tube miongoni mwa wasanii wa Afrika Kusini zikiponza umaarufu wao, wana uwezo wa kujipatia fedha kupitia kampuni zao wenyewe za muziki , anasema Dj Edu. Na kama unavyojua YouTube sio chaneli ya pekee ilio na huduma ya streaming.

Wizkid alifanya kazi na rapa wa Canada Drake mwaka 2016 - ambapo wimbo wao wa One dance - ulioonyeshwa zaidi ya bilioni 1,8, lakini hakutolewa rasmi katika mtandao wa YouTube.