Maisha yanakuwaje kwa Waafrika wanaoishi Japan ambako 98% ya watu ni wazawa?

Danielle Thamas,28, aliwasili Japan mwaka 2016

Chanzo cha picha, DANIELLE THOMAS

Wakati Samuel Lawrance raia wa Nigeria alipowasili nchini Japan akiwa na umri wa miaka17, maisha katika nchi hiyo yalikuwa magumu sana na matatizo ya lugha na utamaduni wa Wajapan ulimtisha.

Akiwa na umri wa miaka 34, Samuel sasa ni mhandisi mwenye mafanikio anayeishi mjini Tokyo na anaelezea jinsi alivyokabiliana na ubaguzi shuleni, Chuo kikuu ambavyo vilimsaidia kuwa katika nafasi aliyonayo sasa.

"Nilipokuwa kijana nilie balehe, nilipitia hali ngumu sana, kama vile watu kukwepa kuketi karibu na mimi katika treni kwa hiyo kila mara kulikua na kiti kitupu karibu yangu lakini hakuna yeyote aliyetaka kukaa na mimi. Watu waliona afadhali wasimame ndani ya treni , wakiwemo wazee kuliko kunikaribia . Nilijihisi vibaya sana nilitamani nisimame ili watu waweze kukaa aliiambia BBC.

Samuel anasema anaamini Japan imekuwa na mabadiliko kidogo na sasa limekua taifa linalowatambua watu wengine, ingawa hali kama hizo katika treni hujitokeza mara chache.

Chanzo cha picha, SAMUEL LAWRANCE

Hakuna makadirio ya idadi ya watu weusi nchini Japan, kwani ofisi ya takwimu ya nchi hiyo huchukua data kwa utaifa. Wageni ni sawa na 1.7% ya idadi ya watu.

Mnamo mwaka 2015, wakati mwanamitindo Ariana Miyamoto, binti yake mwanamke wa Kijapani na baba Mmarekani mweusi , aliposhinda tuzo ya mlimbwende la Miss Universe Japan, suala la ubaguzi zilijadiliwa baada ya watu kumkosoa kutokana na rangi yake.

Ingawa Ariana alizaliwa na kulelewa nchini , alishambuliwa kwa maneno na watu waliosema kuwa hakuwa "Mjapani vya kutosha " kuiwakilisha nchi.

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Mwezi Januari 2019, tatizo jingine la ubaguzi wa rangi lilijadiliwa . Mchezaji wa kifahari wa tenisi -Naomi Osaka alionyeshwa akiwa na ngozi nyeupe katika kibonzo cha matangazo cha kampuni Nissin company, inayotengeneza tambi za noodles, kinyume na muonekano wake. Jambo hilo lilizua gumzo, na baadae kampuni ikaomba msamaha kwa kitendo hicho.

Kifo cha Mmarekani mweusi George Floyd, ambaye alikufa baada ya polisi mzungu kushindilia goti kwenye shingo yake, kiliibua wimbi la maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi mwezi Juni na kuibua mijadala ya kimataifa juu ya ubaguzi wa rangi.

Kulingana na Yasuko Takezawa, profesa katika Chuo kikuu cha Kyoto, tatizo la ubaguzi wa rangi pia ni tatizo katika jamii ya Wajapan.

"Wajapani wengi hawana uzoefu wa moja kwa moja na watu weusi. Picha ya watu weusi nchini Japan inaonekana kupitia vyombo vya habari, vipindi vya tamthilia ,sinema, na watu maarufu wa Afrika, au wachekeshaji wanaoigiza ubaguzi. Ni picha ambayo si sahihi na mwishowe huishawishi jamii "Takezawa anaeleza.

Udadisi usio wa kupita kiasi

Mwezi Januari 2019, Mhandisi wa magari Stephen Estelle, mwenye umri wa miaka 25 aliondoka nchini Marekani kujaribu maisha nchini Japan.

Bila kuzungumza Kijapan, aliishi mwaka mmoja mjini Tokyo, ambako alipata uzoefu wa Wajapan na baadae alihamia kusini zaidi mwa nchi, kufanya kazi katika Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Okinawa.

Stephen anasema alikua na uzoefu mzuri kuliko mbaya na Wajapan na kwamba mazungumzo na Wajapan mara nyingi huwa ni kutokana na udadisi walionao .

Chanzo cha picha, STEPHEN ESTELLE

"Ninahisi kuwa watu wanataka zaidi kuzungumza na mimi ili wanidadisi. Wanauliza maswali, wanataka kujua kuhusu nywele zangu na utamaduni wangu. Ninadhani ni kitu kizuri, kwasababu wanajifunza, na kwahiyo wanaweza kutatua ubaguzi ," anasema Estelle.

" Kuna watu ambao huvuka mipaka na kuingilia maisha yako ya kibinafsi, nilibaini kuwa tulikua na uzoefu unaofanana. Nilipozungumza na marafiki zangu weusi , niligundua kuwa tuna uzoefu unaofanana, tunapokwenda kwenye vyoo vya Umma unakuta mtu usiyemjua anajaribu 'kukuchunguza'. Hii ni kutokua na heshima, kunakopita kiwango, "alikosoa.

"Sipaswi kuwa na hofu juu ya ghasia za polisi hapa, lakini Marekani kuna uungaji mkono zaidi, marafiki Wamarekani weusi, jamii, familia . Kama nikiondoka nyumbani peke yangu ninaweza kusimamishwa na polis

Jamaican Danielle Thomas, mwenye umri wa miaka 28, aliwasili nchini Japan mwaka 2016 na akaanza kufanya kazi kama mwalimu wa shule ya chekechea katika mkoa wa Ibaraki, uliopo kilomita 82 kutoka Tokyo.

Akiwa anawashughulikia watoto wa Kijapan, Danielle ansema kuwa amekuwa na uzoefu "kufurahisha ", kama vile mvulana aliyemwambia mama yake kwamba mwalimu wao ana "uso wa kahawia" na mvulana mwingine aliyemuita "mwalimu wa rangi ya kahawia ."

Chanzo cha picha, Getty Images

Udadisi pia ni sehemu ya maisha yake ya kila siku nchini Japan

"Kila mara ninajibu maswali yale yale juu ya nchi yangu na hasa kuhusu nywele zangu. Inanichosha, lakini sijali."

"Nchini Jamaica kila mtu alikua kama mimi, na nilipofika Japan, pia nilishangazwa na nywele za Wajapan, Pia nilitaka kuzigusa, kwa hiyo ninawaelewa," anatania.

Ugumu wa kuzoea maisha

Mbrazili Lorraine Eduarda Vital Cota Nakamura, mwenye umri wa miaka 28, alikwenda Japan akitokea São Paulo miaka miwili iliyopita baada ya kuweza kushinda hofu ya kuhamia sehemu nyingine ya dunia

"Wakati huo mume wangu anayezungumza Kijapan hakuwa na kazi na wazo la kwenda Japan likaja. Niliogopa sana . Niliamini kuwa Wajapan ni wabaguzi na nilihofia sana maisha ya binti yangu ambaye alikuwa na umri wa miaka 6 ," anasema.

Lorraina aliishi na familia yake katika mkoa wa Mie Prefecture, katikati mwa Japani. Mbrazili huyo anasema alianza kufanya kazi katika viwanda na alihisi kukaribishwa, lakini alikabiliwa na ugumu wa kuyazoea maisha, hasa kwasababu hakuifahamu lugha.

Lorraine alifungua saluni ya urembo, iliyojikita zaidi katika ususi wa nywele , rasta na nywele za kushonwa kichwani (weave). Anasema binti yake Helena ambaye sasa ana umri wa miaka 8 ameweza kuyazowea vyema maisha ya shule nchini Japan , lakini alikabiliwa na kipindi cha unyanyasaji.

"Mwanafunzi wa Kijapan anayesoma nae darasa moja alimkejeli juu ya nywele zake na haraka tukaenda shule kutatua hali hiyo.

Kuhusu ubaguzi wa rangi, Lorraina anasema alipitia hali ngumu, hasa wakati alipokua akifanya kazi katika nguo za mitumba na kuwaomba baadhi ya watoto wajiangalie kwenye kioo

"Mama mmoja kati ya wakinamama waliokuwepo alisema 'abunai, abunai' (ikimaanisha hatari kwa Kijapani) na sikuelewa. Ni kama alikuwa anawaambia watoto kuwa mimi ni hatari kwao ," anakumbuka.

Licha ya hayo anasema uzoefu wake kwa ujumla nchini Japan umekua ni mzuri.

Mfumo wa Japan

Mnaigeria Samuel Lawrance, ambaye amekuwa nchini Japan kwa zaidi ya miaka 15 na ameweza kujichanganya binafsi katika jamii ya Wajapani na mfumo wa nchi katika jamii ya Wajapani, kwani ni kitu fulani ambacho hutokea kwa siri.

"Nimefanya kazi na kampuni ya Kijapani miaka michache iliyopita na nikapitia hali ngumu sana, kumuona mtu ambaye hajafikia kiwango na uzoefu kuniliko akiwa bosi wangu kwasababu tu ni Mjapani.

Hisia ni kwamba hata niwe na ujuzi bora wa aina gani , nifanye chochote kile siwezi kupanda cheo kwasababu mimi ni mgeni au kwasababu mimi ni mweusi, "anasema

Samweli kwa sasa anafanya kazi katika kampuni ya kigeni ambayo inatengeneza teknolojia ya akili bandia katika mafunzo ya gofu na tenisi

"Nimeulizwa aina zote za maswali , hata kama ni juu ya kiyoyozi nchini Nigeria. Inaweza kukukasirisha, lakini ninadhani kazi yangu ni na kuwasilisha taarifa sahihi kwa yeyote anayeniuliza. Ninataka Wajapani wajue nchi yangu na utamaduni wangu ukoje "