Tetesi za soka Ulaya Jumapili tarehe 09.08.2020: Lacazette, White, Walker-Peters, Sancho, Wilson

Arsenal watamuuza Alexandre Lacazette, kama Alexandre Lacazette atakubali mkataba mpya
Maelezo ya picha,

Arsenal watamuuza Alexandre Lacazette, kama Alexandre Lacazette atakubali mkataba mpya

Arsenal watamuuza Mshambuliaji wa Mfaransa Alexandre Lacazette, mwenye umri wa miaka 29, kwa Atletico Madrid kwa pauni milioni 30 mara tu baada ya Mshambuliaji kutoka Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, mwenye umri wa miaka 31, atakapoukubali mkataba mpya. (Star Sunday)

Brighton wamekataa dau la pauni milioni 22 kwa kiungo wa safu ya kati -nyuma kutoka Leeds mwenye umri wa miaka 22 Muingereza Ben White, ambaye msimu uliopita alicheza kwa deni katika klabu ya Elland Road. (Sky Sports)

Maelezo ya picha,

Liverpool wanania na ya White

Liverpool wanania na White, lakini Chelsea wanajiandaa kuipiku timu hiyo na kumuuza Mjerumani anayecheza safu ya kati-nyuma Antonio Rudiger, mwenye umri wa miaka 27, ili kupata pesa. (Star Sunday)

Difenda Muingereza Kyle Walker-Peters, mwenye umri wa miaka 23, anakaribia kabisa kuondoka Tottenham kwa pauni milioni 12 baada ya kuafiki makubaliano binafsi na Southampton, ambao aliwachezea kwa katika kipindi cha nusu ya msimu uliopita kwa deni (Sunday Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Chelsea pia wanamkodolea macho difenda wa Manchester City John Stones

Chelsea pia wanamkodolea macho difenda wa Manchester City John Stones na wanatumai kusaini mkataba na mchezaji huyo wa kimataifa wa England mwenye umri wa miaka 26 kwa pauni milioni 20 (Sunday Mirror)

Arsenal wamejiunga katika kinyang'anyiro cha kusaini mkataba kiungo wa kati wa Marseille Morgan Sanson, huku Tottenham na West Ham pia wakimtaka kijana huyo Mfaransa mwenye umri wa miaka 25 . (Le10 Sport, via Sunday Express)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Arsenal wameanza kumsaka mlindalango mpya atakayeziba pengo la Emiliano Martinez

Arsenal wameanza kumsaka mlindalango mpya atakayeziba pengo la Emiliano Martinez huku wakitaka wakitaka kufahamu ni kw amuda gani wa kawaida chaguo lao la kwanza Bernd Leno atakua nje ya uwanja kutokana na jeraha la goti. (Sun on Sunday)

Leicester na Liverpool wanamtaka kiungo wa kati kushoto wa Olympiakos na Ugiriki Kostas Tsimikas, mwenye umri wa miaka 24, ambaye wanaweza kumpata kwa pauni milioni 12. (Mail on Sunday)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Borussia Dortmund watatoa ofa ya mkataba mpya mnono kwa winga wa England Jadon Sancho kama Manchester United hawatahimili malipo anayotaka

Borussia Dortmund watatoa ofa ya mkataba mpya kwa winga wa England Jadon Sancho, mwenye umri wa miaka 20, na kumuongeza mshahara mkubwa kama Manchester United hawatafikia kiwango cha pauni milioni 100 kufikia tarehe 10 Agosti. (Bild - in German)

Newcastle wamemchagua mshambuliaji wa Bournemouth na England striker Callum Wilson, mwenye umri wa miaka 28, kama mtu wanaelenga kumhamisha. (Mail on Sunday)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Bayer Leverkusen hawatamuuza Kai kwa bei ya chee

Mkurugenzi wa michezo wa Bayer Leverkusen Rudi Voller ameionya Chelsea kuwa klabu yake haitakubali pesa yoyote chini ya bei ya pauni milioni 90- wanazotaka kumuuza kiungo wa kati wa Ujerumani Kai Havertz, mwenye umri wa miaka 21. (La Gazzetta dello Sport - in Italian)

Kiungo wa kati wa Barcelona na Brazil Philippe Coutinho, mwenye umri wa 28, ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo katika klabu ya Bayern Munich, hatafanya uamuzi wowote juu ya hali yake ya baadae hadi Championi Ligi imalizike . (Sport)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Crystal Palace wako tayari kumkosa mshambuliaji muingereza Eberechi Eze.

Crystal Palace wako tayari kumkosa mshambuliaji muingereza Eberechi Eze. QPR wanataka malipo ya pauni milioni 20 kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22, lakini the m Eagles wanamthamanisha kwa pauni milioni 10 pekee. (Sun on Sunday)

=Ham haijapokea ombi la kumuuza beki wa kati wa England mwenye umri wa miaka 21 Declan Rice , kulingana na meneja

Tottenham itaanza kumuangazia mshambuliaji wa England na Bournemouth mwenye umri wa miaka 28 Callum Wilson. (Express)

Chanzo cha picha, Getty Images

Manchester United itasikiza ofa za kumuuza kiungo wa kati wa England Jesse Lengard mwenye umri wa miaka 27 . (Guardian)

Klabu mpya ilioteuliwa katika ligi kuu ya Premia Leeds United wanapanga uhamisho wa mshambuliaji wa Argentina na Stuttgart Nicolas Gonzalez 22 utaogharimu £20m. (Mirror)

Manchester United walikuwa na hamu ya kumsajili beki wa Uholanzi Nathan Ake ,25, kabla ya kujiunga na Manchester City kutoka Bournemouth wiki hii.. (Sky Sports)

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

kiungo wa kati wa Real Madrid Dani Ceballos ni miongoni mwa wachezaji watatu wanaowindwa na Arsenal

Arsenal wanataka kuwagarimia kiungo wa kati wa Real Madrid Dani Ceballos mwenye umri wa miaka 24 , kiungo wa kati wa Madrid Thomas Partey, 27, na difenda wa Lille Gabriel, 22, pauni 100 msimu huu lakini wtahitaji kuwauza wachezaji ili kufanya hivyo . (Sun on Sunday)

Timu mpya iliyopanda daraja West Brom have ilifanya mazungumzo na klabu ya Brighton juu ya mkataba wa difenda Shane Duffy, mwenye umri wa miaka 28 kutoka Jamuhuri ya Ireland (Mail on Sunday)