Barua kutoka Afrika : Jinsi ukarimu wa Waafrika ulivyomfanya mwalimu wa Nigeria aangue kilio

Congolese artist Chris Shongo paints a mural in Kinshasa.

Chanzo cha picha, AFP

Katika msururu wa barua zetu kutoka kwa waandishi wa habari wa kiafrika, Mwandishi wa habari wa Kenya , Joseph Warungu anaangalia vitendo vya ukarimu vilivyofanyika kuwasaidia watu wa kawaida kupitia nyakati ngumu.

Wakati Covid-19 ilipolikumba bara la Afrika, athari zake zilikua mbaya sana- lakini baadhi ya watu wameathirika zaidi kuliko wengine, kwa ugonjwa lakini pia hatua za kukabiliana na ugonjwa wenyewe.

Waalimu wa shule za kibinafsi, ambao nguvu kazi kubwa katika elimu, wameathiriwa kwa namna ya kipekee na kufungwa kwa shule kwasababu hazina usalama na baya zaidi hakuna tarehe ya kufunguliwa kwa shulre hadi leo iliyokwisha kutrangazwa=.

Wengi wamegeuka na kuwa wakulima, kufanya shughuli za usafi na uuzaji wa bidhaa mitaani au wamachinga.

'Usilie, ni sawa'

Ugumu wa maisha umekua sio wa kuvumilika, na umewafanya wengi watoe machozi- miongoni mwao ni -Akindele Oluwasheun Oladipupo katika mji mjuu wa nigeria, Abuja.

Yeye pamoja na waalimu wengine, walikua na matumaini makubwa mwezi Julai wakati serikali ya Nigeria iliposema kuwa itaruhusu shule kufunguliwa kwa ajili ya mitihani. Lakini uamuzi huo ulisitishwa, uchungu ukapita kiasi.

Akindele, ambaye ameoa akiwa na watoto watatu wote chini ya miaka minane, alimuambia mwandishi wa makala haya katika mahojiano ya njia ya simu kwamba alikaa tu kwa mshituko alijaribu kutafakari taarifa hiyo, kabla kuanza kutiririka kwenye uso wake.

"Mke wangu aliniambia, 'Usilie, ni sawa, tutaweza, kwa namna fulani .' Lakini nilikua ninafikiria juu ya waalimu wengiwengi ambao hawana chakula cha kulisha familia . Mara nyingi , wote mwanamke na mwanaume unakuta ni waalimu. Hiyo inamaanisha kuwa pato lote la familia limeenda- kabisa''

Chanzo cha picha, Akindele Oluwasheun Oladipupo

Maelezo ya picha,

Akindele Oluwasheun oladipopu anasema ilikua ni vigumu kuwaona waalimu wazee waliohudumu miaka mingi wakiomba msaada wa chakula

Alishindwa kuyabeba magumu yake binafsi na ya waalimu wengine, alielekea kwenye simu yake na kumwaga majonzi yake.

Rafiki yake aliona video ikirekodiwa na akamuomba aitume kwenye mtandao. Ilisambaa sana, na kumpatia jiana la bandia "mwalimu anayelia".

Akindele anasema alirekodi vido hiyo kwa matumaini ya kuwashawishi watu kuwasaidia waalimu wa shulre za kibinafsi wanaohitaji msaada.

Mwandishi wa habari wa Nigeria Lara Wise alianzisha kampeni ya mtandao wa kijamii wa Facebook kumtafuta Akindele na kumuomba atume sehemu ya pili ya video na maelezo ya akaunti yake ya benki. Misaada ilimwagika kutoka kila pembe ya dunia :

Kwa kuzidiwa na ukarimu , Akindele alimua kukugawa zaidi ya Naira milioni 1.2 ($3,100; £2,400) kwa makumi ya waalimu wanaohitaji msaada.

" Nilijiambia mwenyewe-sasa kwamba Mungu amenijaribu na akafungua njia kwa ajili ya pesa kuingia, kama nikikalia pesa hizo, ina maanisha kuwa ninakal;ia hatma ya watoto wangu.

"Hivyo ndivyo tulivyoanza kuwatafuta waalimu waliokua wakihangaika> Tuliwafikia zaidi ya waalimu 200 na tukawapatia chakula cha kutosha ikiwa ni pamoja na mchele na tambi. Pia tuliweka pesa kiasi kwenye bahasha na tukawapatia ."

Chanzo cha picha, Akindele Oluwasheun Oladipupo

Akindele alipoanza kugawa mifuko ya misaada ndipo alipobaini ukubwa wa tatizo. Waalimu wengi kutoka maeneo mbalimbali ya Nigeria waliomba msaada kutoka kwake.

"Ilikua ni vigumu kusema kweli kuwaona waalimu wazee ambao wamehudumu kwa miaka mingi wakiomba chakula ."

Facebook w ilikua imejaa jumbe zilizooonyesha kilio cha waalimu huku pia wakiilaani serikali kwa kuwapuuza waalimu wa shule za kibinafsi.

'Mungu mbariki Akindele'

Mnaigeria mmoja alisema: "Aibu kwa wanasiasa ambao wanakula nchi hii na kuimaliza. Kama mwanaume ambaye alipata baraka kutoka kwa Mungu anaweza kufanya hili, wanaume wote waliovalia agbadas (nguo kubwa za kinigeria ) na wanawake wanaojificha ndani ya (mitandao ya kijamii ), wanapaswa kuzika sura zao ndani ya aibu."

"Mungu mbariki Akindele sana," aliandika mwingine. "Mungu awakumbuke na kuwasaidia wengi ambao wanaaibishwa na kulia mbele ya umma...wanaokufa kimya ."

Licha ya vmatendo yanayowajali wengine yanayofanywa na wahudumu wanaowashughulikia moja kwa moja wagonjwa husususan wahudumu wa afya wanaonusuru maisha ya watu wakati wa janga , watu wengi kote barani Afrika wanaweza kumudu maisha kutrokana na ukarimu wa Waafrika wa kawaida.

Huku akisubiri kuona kama tarehe ya kufunguliwa kwa shule iliyotangazwa itatimizwa baadae mwezi Agosti , Akindele anasema roho ya ubuntu (roho ya utu) na uwajibikaji -ilimshitua . ilimshangaza.

"Waafrika ni watu wazuri. Hilo ndilo nililoliona katika kipindi cha wiki hizi tatu," anasema.

"Watu ambao sijawahi kukutana nao maishani mwangu-hawanifahamu, hawajui ni wapi ninakotoka, hawajui kama mimi na tapeli au mwizi- lakini wamekua wakinitumia pesa kwenye akaunti. Ninawashukuru sana wote ."

'Kuhangaika kwangu kuliibua huruma'

Nchini Kenya Michael Munene pia amekua akisifiwa kwa roho yake ya kutoa wakati wa janga la corona.

Akiwa ni mtu aliyezaliwa katika familia masikini ambayo ilikua na ugumu wa kupata mlo mmoja kwa siku, anafahamu fika hisia za umasikini na njaa .Alipoanza kazi za vibarua alikua anapata shida ya kulipa kodi ya nyumba.

Alimwambia mwandishi wa makala hii juu ya tukio lililoibua ubuntu(utu) ndani yake.

" Mapema siku moja asubuhi mwenye nyumba alimnisubiri nitumie bafu ambalo lilikua nje ya nyumba, halafu akanifungia mlamgo haraka mara moja nje ya nyumba yake kwasababu ya madeni ya kodi ya nyumba.

"Nikiwa nimekwama nje bila nguo, na pesa, niliapa kwake kwamba sitakubali mtu yeyote aaibishwe kama nilivyoaibika."

Michael Munene
Michael Munene
It's tough for my business but I can't bear the sight of homelessness"
Michael Munene
Landlord

Leo Michael ni mmiliki wa nyumba za kupangisha kwa karibu miaka 30 akikodisha nyumba. Wakati mapato ya wapangaji wake yalipopungua aliwapa likizo ya malipo ya kodi yao, ambayo hawajalipa tangu mwezi Mei.

"Ni jambo gumu kwa biashara yangu , lakini siwezi kuvumilia kuwaona watu wakiwa hawana nyumba. Nimewaambia wapangaji wangu kwamba kwa sasa wanapaswa kuelekeza juhudi zao zaidi katika kuzitafutia familia zao chakula."

Katika mji mkuu wa Ghana Accra, wakati amri ya kukaa nyumbani ilipotangazwa , ya Elizabeth Yawsony alielekeza mawazo yake kwa watu masikini wanaoishi mitaani.

Woman at a microphone
Elizabeth Yawson
People responded generously and we were able to feed about 100 people for one week"
Elizabeth Yawson
Radio journalist

Wakati mwandishi wa habari wa redio alipoanzisha kampeni ya mtanaoni kuwasaidia watu wasio na makazi, mwitikio ulikua ni wa shauku kubwa.

"Watu wa;lijibu kwa ukarimuna waliweza kuwalisha watu wapatao100 kwa wiki.

"Naadae nilipata msaada wa migahawa miwili na tukafikia wahudumu wa afya 30 katika hospitali ya Kasoa, katika jimbo la kati la Ghana, tukawapatia chakula kwa wiki nzima ."

Kile ambacho Akindele, Michael na Elizabeth wamekionesha ni kwamba ingawa jogoo ni wa nyumba moja, inapowika husikika katika kijiji kizima.

Unaweza pia kutazama:

Maelezo ya video,

Unawezaje kunawa mikono licha ya upungufu wa maji?

Taarifa za matendo yao na wengine kama wao zimeangazia roho nyingi kote barani Afrika.