Virusi vya corona : Idadi ya watu waliokufa yapita 100,000 na hakuna dalili ya kupungua kwa mlipuko

A man holds Brazilian flag between red balloons in Rio de Janeiro

Chanzo cha picha, Anadolu Agency/Getty

Maelezo ya picha,

Shughuli ya kutoa rambirambi kwa waathiriwa ilifanyika katika ufukwe wqa Rio de Janeiro' wa Copacabana

Brazil imerekodi zaidi ya vifo 100,000 vilivyotokana na Covid-19, ikiwa ni idadi ya pili kwa ukubwa, huku mlipuko nchini humo ukiwa hauoneshi dalili ya kupungua.

Virusi viliwauwa watu 50,000 katika kipindi cha miezi mitatu , lakini idadi hiyo iliongezeka mara dufu katika kipindi cha siku 50 pekee. Watu zaidi ya milioni tatu wamethibitishwa kupata virusi vya corona nchini humo hadi sasa.

Janga bado halijafikia kilele chake lakini maduka na migahawa tayari vimefunguliwa.

Rais wa Brazili Jair Bolsonaro amepuuza athari za virusi na amepinga hatua za kudhibiti maambukizi ambazo zinaweza kuathiri uchumi.

Kiongozi huyo wa mrengo wa kulia, ambaye binafsi alipatwa na maambukizi ya corona, alipinga masharti yaliyowekwa na magavana wa majimbo ya kukabiliana na Covid-19, na mara kwa mara alijiunga umati wafuasi, wakati mwingine bila kuvaa barakoa.

Wataalamu wamelalamika juu ya ukosefu wa mpango ulioratibiwa wa sertikali ya Bolsonaro ambapo maafisa wa nchi hiyo sasa wanaangazia jinsi ya kufungua shughuli za kiuchumi, ambazo huenda zikachochea zaidi kusambaa kwa virusi.

Jinsi Brazil inavyoshughulikia mzozo wa virusi ?

Wizara ya afya inaongozwa na Jenerali wa jeshi ambaye hana uzoefu katika masuala ya huduma ya afya kwa umma. Awali wawili , wote madaktari , waliacha kazi baada ya kuindwa kukubaliana na rais juu ya hatua za kukaa mbali baina ya watu na matumizi ya dawa ya Mawaziri hydroxychloroquine kama tiba.

Rais Bolsonaro - ambaye aliuita ugonjwa wa Covid-19 "mafua madojgo" na ambaye amekuwa akikosolewa nyumbani na nje ya nchi kwa namna alivyoushughulikia mlipuko wa corona- alisema kuwa alipona maambukizi ya corona kwa kutibiwa na dawa ya malaria.

"Ujumbe wa serikali leo hii ni kwamba : 'Pata virusi vyako vya corona na kama utaugua sana , kuna kitengo cha wagonjwa mahututi .' Kwa kifupi hiyo ndio sera yetu leo." Dkt José Davi Urbaez, afisa wa ngazi ya juu wa taasisi ya udhibiti wa magonjwa ya maambukizi-Infectious Diseases Society, ameliambia shirika la habari la Reuters

Brazil imekua na vifo 100,477 vya virusi vya coronana wagonjwa wa ugonjwa huo 3,012,412 , kwa mujibu wa wizara ya afya, ingawa idadi inaaminiwa kuwa ni ya juu zaidi kwasababu watu hawapimwi vya kutosha . Ni Marekani tu ambayo ina idadi kubwa zaidi ya watu wenye virusi vya corona zaidi ya Brazil kwa sasa.

Ni wapi kuna maambukizi zaidi ?

Idadi ya wagonjwa imeongezeka katika wiki za hivi karibuni katika maeneo ya vijijini hususan katika majimbo ya kusini na magharibi mwa nchi , huku hali ikionekana kuboreka katika jiji la São Paulo, ambalo ni maarufu zaidi.

Wakati huo huo, idadi ya maambukizi imepungua katika majimbo ya kaskazini- ikiwa ni pamoja na Amazon ambalo awali lilikua ni kitovu cha maambukizi na katika Rio de Janeiro, ambako picha za umati wa watu waliokuwa wanavinjari kwenye baa na fukwe ziliwashangaza wengi mapema wiki hii.

Katika rambirambi zilizotolewa kwa waathiriwa wa corona Jumamosi, kikundi kisicha cha kiserikali cha Rio de Paz kiliweka misalaba kwenye mchanga juu ya mwenge wa Rio wa ufukwe wa na kuachilia tufe nyekundu 1,000 angani.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Rais Bolsonaro akisalimiwa na wafuasi wake katika ziara yake ya kwanza baada ya kupona Covid-19 mwezi uliopita.

Virusi vimewaathiri sana watu weusi na wakazi wa maeneo masikini yanayofahamika kama favelas , na kuna hofu kwamba vitaendelea kusambaa miongoni mwa jamii za wazawa. Takriban wazawa 22,300 wameathiriwa huku 633 wakifa, limesema shirikisho kuu la watu wa jamii ya wazawa nchini Brazil -Apib

Sipka wa bunge la seneti nchini humo Davi Alcolumbre alitangaza siku nne za maombolezo na katika Congresi lakini Rais Bolsonaro hajatoa kauli yoyote. Mapema wiki hii alisema kuwa anasikitika kwa wale wote waliokufa lakini akasema: ''lazima tuendelee na maisha yetu".