Africa Eye: Mapato kupitia corona

Africa Eye: Mapato kupitia corona

Uchunguzi wa BBC Africa Eye umebaini kuwa baadhi ya wafanyakazi katika hospitali nchini Ghana wamekua wakiuza vifaa kinga dhidi ya corona kwa maslahi ya kibinafsi. Zaidi ya wahudumu wa afya 2,000 nchini Ghana wameambukizwa virusi vya corona. Nchi hiyo inakabiliwa na uhaba mkubwa wa vifaa kimnga kama vile barakoa na suti maalum ya kuvalia wanapowahudumia wagonjwa. Mwandishi mpekuzi, Anas Aremeyaw Anas anaonesha jinsi baadhi ya maafisa wanavyojinufaisha huku wakihatarisha maisha ya wafanyakazi wenzao.