Kwanini mfanyabiasha tajiri wa Hong Kong anayeunga mkono demokrasia - Jimmy Lai amekamatwa?

Jimmy Lai. pocha ya maktaba

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Jimmy Lai amesema "mamlaka inachukia ukakamavu wangu", ana kwamba yuko tayari kwenda jela

Mfanyabiasha maarufu wa Hong Kong Jimmy Lai amekamatwa akishukiwa kula njama na vikosi vya kigeni, amesema mshirika wake.

Mark Simon alisema kuwa mfanyabiashra huyo alipamatwa chini ya sheria yenye utataya usalama iliyowekwa na China mwezi Juni.

Bwana Lai amekua mfuasi maarufu wa maandamano ya kutaka demokrasia yaliyoibuka Hong Kong mwaka jana.

"Jimmy Lai amekamatwa kwa kula njama na mataifa tajiri ya kigeni wakati huu," alisema Bwana Simon,afisa mtendaji katika kampuni ya habari ya Bwana Lai -Next Digital.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo, Polisi mjini Hong kong pia waliingia katika kampouni yake ya habari , wakafanya msako katika ofisi.

Polisi wamethibitisha kuwa watu saba walikamatwa Jumatatu wakishukiwa kuvunja sheria ya usalama wa taifa , lakini bado hawajamtaja Bwana Lai.

Kukamatwa kwa watu hao Jumatatu ni wimbi la tatu ya wimbi la kuwakamata na kuwafunga chini ya sheria mpya ya usalama wa taifa. Kesi ya Bwana Lai itakua ndio kesi maarufu zaidi hadi sasa na itakayomuhusisha mtu mwenye uraia wa kigeni

Jimmy Lai ni nani?

Bwana Lai anakadiriwa kuwa na utajiri wa thamani ya dola zaidi ya bilioni 1 (£766m).

Baada ya kupata utarajiri wake katika sekta ya nguo, baadae aliingia katika masuala ya habari na kuanzisha gazeti linalofahamika kama Apple Daily, ambalo mara kwa mara limekua likiikosoa serikali ya Hong Kong na uongozi wa China.

Na pia binafsi amekua mwanaharakati dhidi ya hatua ya Beijing kuiwekea vikwazo vya sheria kali Hong Kong . Mwaka 2019 aliunga mkono maandamano ya kudai mageuzina akashiriki binafsi maandamano hayo.

Wakati aliposhitakiwa mapema mwaka huu kwa kuhusika na maandamano hayo vyombo vya habari vya taifa la China vilimuita ''Mpangaji wa maandamano ya ghasia'' ambaye "amesambaza wimbi la chuki na taarifa potofu juu ya China bara mchana na usiku.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

2019, kulishuhudiwa msururu wa maandamno ya kupinga Beijing mjini Hong Kong

Tarehe 30 Juni, wakati sheria ya usalama ilipopitishwa, Bwana Lai aliiambia BBC kuwa hii "inamaanisha kifo kwa Hong Kong".

Alionya kuwa Hong Kong itakua na ufisadi sawa na China bara kwasababu "bila utawala wa sheria, watu wanaofanya biashara hapa hawatakua na kinga ".

Katika mahojiano tofauti na shirika la habari la AFP, Bwana Lai alisema : "Nimejiandaa kwa jela. Kama itakuja , nitakua na fursa ya kusoma vitabu ambavyo sijavisoma. Kitu ninachoweza kukifanya tu ni kuwa na mtizamo chanya."

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Hong Kong wamevamia jumba moja karibu na ofisi za Next Digital na Apple Daily

Sheria mpya ya usalama ni nini?

Hong Kong imejitawa kwa kiasi kikubwa tangu iliporejeshwa kwa utawala wa Kichina mwaka 1997, na wakazi wake wamekua na kiwango cha hali ya juu cha uhuru wa kuongea na wa habari kuliko upande wa bara.

Lakini kipengele muhimu cha sheria kinajumuisha uhalifu wa kujiondoa kama sehemu ya nchi,But the law's key provisions include that crimes of secession, ukosefu wa utiiifu kwa mammlaka, ugaidi, kushirikiana na vikosi vya kigeni, uhalifu ambao adhabu yake ni kifungo cha maisha jela.

Sheria hiyo inarahisisha kuwaadhibu waandamanaji, na kupunguza uhuru wa kujitenga wa Hong kong.

Pia inaipatia mamlaka Beijing ya kudhibiti maisha katika koloni la zamani la Uingereza kwa namna ambayo haikuwezekana awali.

Wakosoaji wanasema imefanikiwa kuzuwia maamdamano na uhuru wa kujieleza-China imesema kuwa sheria mpya itarejesha uthabiti katika eneo hilo baada ya mwaka mmoja wa ghasia.