Virusi vya corona: Tunatathmini ukweli kuhusu taarifa gushi Afrika

  • Na Jack Goodman, Peter Mwai na Flora Carmichael
  • BBC Reality Check
Two African women in colourful face masks speaking to each other on the street.

Chanzo cha picha, Reuters

Huku idadi ya watu wenye maambukizi ya virusi vya corona ikizidi watu milioni moja, tumeangalia baadhi ya taarifa gushi ambazo zilishirikishwa kwa kiasi kikubwa juu ya janga la corona barani Afrika.

Madai : Rais wa Ghana ameidhinisha video yenye nadharia potofu

Jibu: Sio kweli

Sauti ilirekodiwa ikiidhinisha nadharia potofu juu ya janga la corona ilisemekana kuwa ni ya rais wa Ghana. Hatuna uhakika ni naani anayeongea . Ana lafudhi ya Afrika magharibi, lakini sio rais wa Ghana Nana Akufo-Addo.

Waziri wa habari wa Ghana amethibitisha kuwa sauti hiyo ilikua sio ya ''rais na akasema kuwa madai hayo sio sahihi''

Ujumbe huo unatoa madai yasiyo na ushahidi juu ya asili za virusi vya corona, mkiwemo nadharia potofu ambazo zimekua zikisambaa kwamba janga la corona lilipangwa katika kile kinachoitwa 'plandemic'.

Pia inaelezea madai yasiyo sahihi juu ya chanjo ya lazima ambayo inasemekana Bill Gates anaidhibiti.

Awali tuliandika kwa kina juu ya tetesi za nadharia kuhusu chanjo ya lazima na taarifa ya upotishaji kuhusu janga la corona kupangwa.

Sehemu tofauti za sauti hiyo zimekua zizunguka katika mataifa ya Ulaya, Marekani na Afrika.

Moja ilitumwa kwenye mtandao wa YouTube nchini Nigeria , na imetazamwa na watu zaidi ya 400,000.

Mwanaume anayemiliki mtandao huo wa You Tube anasema alibadili kichwa cha habari cha video na kuwa "Africa Leader...Exposes Bill Gates Deadly Vaccine For Africa" au ''Viongozi wa Afrika…Waianika Chanjo hatari ya Bill Gate- kwa ajili ya Waafrika'' baada ya watu katika jumbe zao chini ya video hiyo kumtaja kwa makosa rais wa Ghana.

Hatahivyo, picha ya Nana Akufo-Addo bado inaonekana.

Madai: Kunywa pombe kunaweza kumaliza virusi vya corona

Jibu : Madai haya yasiyo sahihi yalikuwa na lengo la kueneza uvumi, lakini yamesambazwa kwa kushirikishwa barani Afrika

Video ya uvumi ya mwanamume aliyechukizwa na kuwekwa kwa marufuku tena ya mauzo ya pombe kwenye televisheni ya habari ya Afrika Kusini yametazamwa na maelfu ya watu katika mtandao wa Facebook na kushirikishwa kwenye WhatsAp

Video imehaririwa kumuondoa mwakilishi wa Chama cha wauzaji wa pombe wa Afrika Kusini (ambaye alikua akihojiwa), na badala yake akawekwa mchekeshaji.

Mchekeshaji Thandokwakhe Mseleku alituma video ya sura yake katika televisheni katika mitandao ya Instagram na YouTube.

Katika video anasema : "Vitakasa mikono vina asilimia 70 ya kileo, kwahiyo kama unakunwa pombe ni kama unasakasa ndani ya mwili wako.

Ukitazama maoni ya watu kwenye video hiyo, watu walidhani ni kweli.

Baadae mchekeshaji huyo aliita video hiyo 'mzaha'. Tumemtaka Thandokwakhe Mseleku toe maoni .

Unywaji wa kileo kilichomo kwenye vitakasamikono ni hatari sana na vimekwezga sababisha vifona. Hakiwezi kukukinga na virusi vya corona.

Madai : Kula vyakula vyenye asidi inaweza kumaliza virusi

Jibu : Sio sahihi.

Tangazo linalopotosha linalodai kutoa ushahidi kutoka ndani ya vyumba vya kujitenga vya hospitali juu ya nini cha kufanya kumkinga mtu na virusi vya corona limekua likisambaa katika mitandao ya kijamii barani Afrika.

Linadai kuwa kuwa 'asidi'ya virusi inaweza kumalizwa na ulaji wa vyakula vyenye aside, na kuorodhesha aina mbali mbali za matunda yenya viwango vya juu vya pH.

Viwango vya pH vinaanzia kutoka sifuri (aside yenye nguvu zaidi) hadi 14( vyenye aside kali) . pH ya 7 ni ya kiwango cha kawaida.

Baadhi ya viwango katika ujumbe ulioshirikishwa viko nje ya kiwango : Parachichier 15.6 na Watercress 22.7. Hii sio sahihi

Lakini je vyakula vya aside vinaweza kuua virusi?

Sehemu tofauti za mwili zina aina yake asilia tofauti za pH ambazo kwa kawaida kuwa katika uwiano unaotakikanana haiwezi kubadilika kupitia chakula. Kwa mfano , damu ina aside kidogo, tumbo lako pia lina aside.

Kwahiyo kula vyakula vya aina fulani hakuna athari yoyote kwa viwango vya pH ndani ya seli.

"Ikizingatiwa kuwa haiwezekani kuongeza pH za seli zako, basi itakua haina maana kuzungumzia kwamba kiwango fulani cha pH kitaua virusi ", anasema Connor Bamford, mtaalamu wa virusi katika Cho Kikuu cha Queen cha Belfast.

Kwa mujibu wa Lee Mwiti, Mhariri mkuu wa , Africa Check, kusambaa kwa taarifa potofu kwenye WhatsApp ni changamoto kwa wachunguzaji wa

App ya ujumbe ni maarufu sana barani Afrika , lakini kutokana na kwamba ni jukwaa la mawasiliano baina ya mtu na mtu ni vigumu kupima usambaaji wa taarifa feki na kuzikusanya. Anasema kazi ya kitengo cha kuchunguza ukweli juu ya taarifa barani Afrika inayopata taarifa kupitia kwa watu na podcast inamaanisha kuwa "wanaamini kwamba ni chanzo thabiti cha taarifa za upotoshaji ".

Madai: Jaribio la chanjo barani Afrika limesababisha vifo vya watoto wawili children

Jibu: Si sahihi

Wakati madaktari wawili wa Ufaransa waliposema kwenye televisheni ya Ufaransa mwezi Aprili kwamba majaribio ya awali yanapaswa kufanyika Afrika, kauli zao zilisababisha hasira, mkiwemo Waafrika wanaoishi ng'ambo.

Mwanablogi mwenye makao yake London-aliwajibu madaktari wa Ufaransa kwa madai yasiyo sahihiakidai kwamba majaribio ya chanjo tayari yamekua yakiendelea Guionea, na akatoa madai mengine yasiyo sahihi kwamba watoto wawili walikufa kutokana na majaribio hayo.

Video ilielezeakile kilichodaiwa kuwa ni taarifa za eneo iliyoonyesha ripoti ya maandamano katika mitaa na mahojiano na watoto waliougua.

Ukweli ni kwamba, ripoti hiyo ya habari ilikua ni ya mwaka 2019, kabla mlipuko wa corona haujaanza, na tukio hilo halikua na uhusiano wowote na chanjo.

Wizara ya afya ya Guinea ilitoa taarifa kwa umma wakati huo ambayo ilielezea baadhi ya watu walikua na madhara baada ya kupewa dawa ya tiba ya wadudu.

Kwa mujibu wa maafisa waliohojiwa katika ripoti yenyewe na makala nchini humo, hapakua na kifo kilichoripotiwa kutokana na tiba hiyo.

Madai katika video ya kwanza mwezi Mei yaliondolewa wakati huo, lakini yameendelea kuenea katika Facebook na makundi ya WhatsApp na yametazamwa na watu wapatao 25,000 katika mtandao wa YouTube.

Wachunguzi wa ukweli juu ya taarifa hii nchini Guinea wanafanya juhudi ili kukanusha haya na taarifa nyingine za uongio zinazoenezwa mtandaoni.

Lee Mwiti Kutoka Africa Check anasema kuwa taarifa zinazosambazwa zaidi na za uongo ndio ambazo zimekwama katika shauku ya watu ambao hawana la kufanya na "ukosefu wa udhibiti katika wakati ambao haukutarajiwa".