Kwanini jua wakati mwingine huwa jekundu?

Red sun setting over the sea, orange skies

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Je kuna utofauti wowote ambao umeubaini siku za hivi karibuni?

Muonekano huu wa kupendeza hufahamika lakini je unajua kwanini?

Mara nyingi huwa unaweza kuonekana wakati jua linatua ama machweo.

Jua hubadilika na kuwa jekundu, na anga inakuwa na muonekano wa rangi ya chungwa.

Inapendeza sana… lakini juu ya yote ni sayansi.

Tazama mwenyewe, ila pia kumbuka, usilitazame jua moja kwa moja!

Na pia hata usifikirie eti utatumia darubuni - inaweza kuharibu uwezo wako wa kuona na kusababisha upofu.

Muonekano bora mjini

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Katika baadhi ya sehemu za dunia, machweo na macheo umekuwa na muonekano wa kuvutia siku za hivi karibuni

Muonekano wa macho huenda ukakuacha bila cha kusema, ila kuna mawil ya msingi:

Yote hayo yanahusu fizikia ya kitambo "kuhusu sifa za jua linalopita hadi anga ya dunia," amesema mtaalamu wa anga za juu Edward Bloomer, kutoka makavazi ya Royal Greenwich.

Kwanza tunahitajika kuelewa mwanga, umetengenezwa kwa rangi zote kwa mpangilio wa nuru nyekundu, rangi ya machungwa. Kijani, samawati na zambarau.

"Inahusisha mwanga uliotawanyika - na mtawanyiko wake hauna usawa," amesema Bloomer.

Kila rangi ina kiwango cha wimbi lake, na hilo ndio hufanya kila moja wao kuonekana ilivyo.

Kwa mfano, mwanga wa rangi ya zambarau una wimbi fupi ukilinganisha na rangi nyekundu.

Hatua nyingine ni kuelewa anga, matabaka ya gesi - ikiwemo oksijeni tunayotumia kupumua - ambayo huzunguka sayari yetu na kuwezesha maisha.

Mwanga uliotawanyika

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Rangi nyekundu yenye muonekano wa moto

Wakati mwanga unapita matabaka tofauti tofauti - kila moja ikiwa na gesi ya uzito tofauti - unapinda na kugawanyika kana kwamba unapita kwenye mche.

Pia, kuna chembe zilizopo kwenye anga ambazo zinafanya mwanga uliogawanyika kugonga na kuakisi.

Wakati jua linapochomoza au linapotua, miale yake inapiga tabaka la juu la anga katika muonekano wa pembe fulani... na hapo ndipo miujiza inapoanza.

Wakati miale ya jua huchoma matabaka ya juu umbali wa mwaga wa samawati hugawanywa na kuakisiwa badala kunyonywa.

"Jua linapokuwa chini kwenye upeo wa macho, rangi ya samawati na kijani hutawanyika, na kupata muonekano wa rangi ya chungwa na mng'ao wa rangi nyekundu," amesema Bloomer.

Hiyo ni kwasababu mwanga wa umbali mfupi (zambarau na samawati) hutawanywa zaidi kuliko mwanga wa umbali mrefu (rangi ya machungwa na nyekundu)… na matokeo yake ni muonekano wa rangi za kuvutia katika anga.

Lakini anga linaonekana jekundu kweli!

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kukiwa na mchanga kwenye anga, unaweza kuona anga la rangi ya waridi na nyekundu mfano wa sayari ya Mahiri

Ndio, inaweza kuonekana hivyo lakini muonekano wake ulionesha kwamba jua halijabadilika hata kidogo. Inategemea ulipo duniani, anga yenu inaweza kuwa na muonekano mzuri zaidi sasa hivi kwasababu ya hali ya kawaida.

"Mawingu ya vumbi, moshi na vingine kama hivyo vinaweza kuathiri muonekano wa anga pia," amesema Bloomer.

Kwahiyo ikiwa unaishi India, California, Chile, Australia au maeneo mengine ya Afrika - au mahali popote karibu na mchanga mwekundu - mazingira yanaweza kuwa mazuri na akisi ya mwanga ikitegemea na hali ya hewa.

"Inaweza kuwa kama inavyotokea kwenye sayari ya Mars, pale vumbi jekundu linapokuwa kwenye anga, itatoa muonekano kwamba anga ni jekundu hivi na rangi ya waridi," amesema Bloomer.

Na hata ikiwa unaishi mbali na jangwa (au sayari ya Mars!), bado unaweza kuona muonekano wa anga ya aina hii - na mara nyingi katika mchanga wa eneo la Sahara unakwenda kwenye tabaka la mbali la anga na kusafiri hadi Ulaya na zaidi ya Siberia na Marekani.

Kwanini hili linatokea?

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Hatua ya kutotoka nje imefanya watu kupata fursa ya kutazama uhalisia wa dunia kwa karibu zaidi

Pengine kinachotokea sio kigeni lakini kilichobadilika ni kwamba tunaona vitu kwa namna tofauti.

"Kipindi chote cha kufungwa kwa shughuli kwasababu ya corona watu wamekuwa wakitoa angalizo kwa anga," amesema Bloomer akiwa anatabasamu, "Pengine kwasababu hakuna cha zaidi kinachoweza kufanywa!"

Kuwa na rangi ya upinde

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Upinde, upinde mara mbili na anga la samawati

Ikiwa, chembe za mwanga zilizotawanyika pia kuelezea kwanini anga mara nyingi huwa na muonekano wa rangi ya samawati zaidi katikati ya mchana.

Jua likiwa juu kwenye anga, mwanga wake unapita kwenye anga bila kugawanywa, na unanyonywa kadiri unavyoendelea kujitokeza na kuonekana kwa uzuri na wingi zaidi kwa rangi ya samawati.

Lakini bila shaka, mambo yanaweza kubadilika ikitegemea na hali ya anga.

Ikiwa kutanyesha kama jua linawaka, kisha mwanga unagawanywa kwa umbali tofauti na kila tone la mvua, na matokeo yake ni mwanga wa rangi zote kutawanyika kwenye anga.

Tunajua hilo kwasabau katika karne ya 19, mwanafizikia Lord Rayleigh alijitolea mmuda wake kufuatilia mwanga wa jua na anga na ilikuwa alikuwa mtu wa kwanza kuja na maelezo ya kwanini anga ni rangi ya samawati.