Shakuntala Devi: Mwanamke aliyeushangaza ulimwengu kwa kipaji cha kutatua hesabu kwa kasi zaidi duniani

Shakuntala Devi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Shakuntala Devi alianza kutatua hesabu akiwa na umri wa miaka 3

Huo ndio uliokuwa uwezo wa Shakuntala Devi kufanya hesabu kwa kutumia ubongo wake kwa sekunde kadhaa hali iliowafanya wale waliomfahamu kumuita 'Kompyuta'.

Talanta yake na nambari ilimsaidia kujipatia nafasi katika rekodi za dunia za Guiness na kumfanya kuwa mtu maarufu aliesafiri kote duniani akionesha uwezo wake wa kutatua hesabu katika vyuo vikuu, kumbi za filamu, katika radio na katika studio za runinga.

Maisha ya mwanamke huyu wa India , aliefariki 2013 akiwa na umri wa miaka 83, yalioneshwa katika filamu ilio na jina lake ambayo ilitolewa hivi karibuni katika ukumbi wa Amazon.

Vidya Balan, Muigizaji wa filamu za Bollywood anayeigiza kama jini, alimtaja kama msichana kutoka mji mdogo wa India aliyeushangaza ulimwengu.

''Hakuwa na elimu, lakini alikuwa na kipaji cha kutatua hesabu ngumu zaidi kwa kutumia ubongo wake kwa kasi ya kushangaza. Alikuwa na kasi kama ya kompyuta'' ,Balan aliambia BBC.

Ili kuandaa jukumu lake , muigizaji huyo alijifunza miongoni mwa masuala mengine kanda ya video kutoka kwa runinga ya Canada ambapo Devi anaonekana akiliuliza jopo iwapo linataka kupatiwa majibu kuanzia kushoto hadi kulia , au kutoka kulia hadi kushoto.

Sekunde chache kabla, mmoja ya wanajopo hilo alikuwa amemuuliza kuzidisha nambari mbili za nambari nane. Devi aliwapatia jibu mara moja.Kanda hiyo ya video imesambazwa zaidi ya mara nusu milioni tangu ilipochapishwa mwaka 2013.

Zawadi ya Mungu

Katika mahojiano Devi alisema kwamba alifanya hesabu katika kichwa chake tangu alipokuwa na miaka mitatu.

Babake ambaye alikuwa mchezaji wa sarakasi, aligundua kipawa hicho wakati walipokuwa wakicheza karata na kubaini kwamba msichana huyo mdogo alikuwa akimshinda kwasababu alikuwa na uwezo wa kukariri karata zake.

'Ni zawadi kutoka kwa Mungu', alikuwa akisema alipoulizwa kuelezea kipawa hicho cha ajabu.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Devi aliweza kufanya hesabu ngumu kwa kichwa tu bila kuhitaji kuandika mahali popote.

Devi alikuwa na uwezo wa kufanya hesabu ngumu bila ya kuhitaji kuandika chini.

''Hakuna hata mtu mmoja katika familia yao alikuwa na kipaji chochote cha nambari, licha ya kwamba babake alikuwa akfanya mazingaombwe'', alisema.

Akiwa na umri wa miaka 6 , ambapo alikuwa ametambulika kama mtoto aliependa hesabu, alionyesha ujuzi wake kwa mara ya kwanza katika hafla ya umma katika mji wa Mysore, Karnataka, Mji wa India alikozaliwa.

Devi pia alijifunza mwenyewe kusoma na kuandika.

Kasi ya ajabu

Mwaka 1950 , aliposhiriki katika kipindi cha runinga cha BBC, alitoa jibu la hesabu ambayo haikuwa sawa na ile ya mwandalizi wake.

Hii ni kutokana na makosa katika hesabu hiyo, Devi alisema. Wataalamu walipoangazia tena nambari hiyo walikubaliana naye.

Mwaka 1977, mjini Dallas, Marekani , Devi aliishinda Univac, mojawapo ya kumyuta zilizokuwa na kasi zaidi kuwahi kuundwa duniani.

Na katika shindano la kuingia katika vitabu vya dunia vya Guiness , alishinda kwa kuzidisha nambari mbili za nambari 13 zilizochaguliwa kutoka maeneo tofauti na kompyuta mbele ya umati wa watu 1000 katika chuo cha Imperial mjini London.

Alichukua sekunde 28 kukamilisha hesabu hiyo ikiwemo muda aliochukua kusoma jibu la nambari 26.

Pia unaweza kusoma:

Alivutiwa na mambo mengine

Mbali na kuwa na kipaji cha kufikiria kwa kasi , Devi alianza kuwa mnajimu .

Chanzo cha picha, IDMB

Maelezo ya picha,

Vidya Balan huwa anafanya hesabu Amazon.

Aliandika vitabu kuhusu unajimu, upishi, hesabu, na uhalifu.

Pia alipigania kuhalalishwa kwa mapenzi ya jinsia moja, ambapo 1970 lilikuwa tatizo kuu la ulimwengu kwa jumla.

Alikuwa mtu mwenye mambo mengi. Aliishi maisha yake kulingana na masharti yake yeye mwenyewe.

Hakuogopa, hakuomba msamaha. Na kufikiri ilikuwa miaka 50 iliopita, Balan anasema.

Muigizaji huyo aliandaa jukumu lake kwa kutazama kanda za video na kusoma habari kumuhusu Devi, pamoja na kusikiliza hadithi za Anupama Banerji, mtoto wa kike wa pekee anayeishi na familia yake mjini LOndon.

"Yote haya yalinipatia wazo kuhusu maisha yake . Kile kilichonivutia mimi ni kwamba watu uhusisha mchekeshaji na hesabu na hubadilisha wazo hilo kabisa'', anasema.

"Alicheza na nambari, uliweza kuona akifurahi ndani yake alipofanya hesabu'', alipenda sana. kuigiza.

Katika utafiti wa mwaka 1990, Authur R Jensen , mtafiti wa intelijensia ya binadamu katika chuo kikuu cha California ,USA, alimtaja kuwa "makini, anayetumia muda wake mwingi vizuri, mwenye tabia njema na mtu fasaha.

Chanzo cha picha, IMDB

Maelezo ya picha,

Devi anasema hakuna yeyote kwenye familia yake alikuwa na kipaji au alipenda hesabu.

Hatahivyo hakuwa na furaha moyoni mwake , anasema mwandishi na mtengenezaji filamu Pritish Nand

Baadhi zilikuwa sababu za kibinafsi , lakini kitu muhimu zaidi ni kwamba alikuwa na kipaji ambacho hakuweza kukifanya kumpatia fedha, aliambia BBC.

Katika mahojiano yake mengi , Devi alielezea kwamba akiwa mtoto alikuwa chini ya shinikizo kupata fedha kama mtu aliekuwa akiilisha familia yake.

Na baadaye katika maisha yake, hakufurahi baada ya kufunga ndoa na mpanzi wa jinsia moja ambaye hakuwa amejitangaza.

''Nina shahada ya udaktari katika hesabu na sijui kugawanya na takwimu tatu au jinsi ya kuhesabu mraba kwa mkono".

Balan anatumai filamu hiyo itawaburudisha wakati ambapo watu wengi wapo majumbani mwao kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.

lakini antumai pia italeta mabadiliko jinsi watu wanavyofunza hesabu , kulifanya kuwa somo la kuvutia na kuondoa hofu ambayo watu huwa nayo mbali na kuwapatia wengine motisha ya kujifunza.

Pia unaweza kutazama:

Maelezo ya video,

Sibahle Zwane: Mtoto bingwa wa maswali ya hesabu kutoka Afrika Kusini