'Nilipatana na baba yangu Facebook'

Farhiya and her father reunited in Oslo

Chanzo cha picha, Farhiya

"Pongezi! tumempata baba yako!" ulisema ujumbe wa barua pepe aliopokea Farhiya.

"Sikuamini mara ya kwanza nilipopata ujumbe huo." alisema. "Ilikuwa kama ndoto. Lakini nilikuwa na imani siku hii ingeliwadia."

Alipokua mtoto, Farhiya alipenda sana kumuuliza mama yake kumhusa baba yake.

"Alikua akiniambia angalia ndani ya kioo," anasema Farhiya. "Unazungumza kama yeye, kutembea kama yeye, na pia mbishi kama yeye," mama yake alimjibu.

Lakini alikuwa na picha chache za kitambo ambazo, alitumia kumkumbuka baba yake.

Farhiya mwenye umri wa miaka 39 alizaliwa- 1976 na mama Mrusi na baba Msomali katika mji wa Leningrad - ambao sasa unafahamika kama Petersburg.

Chanzo cha picha, Farhiya

Maelezo ya picha,

Farhiya alifahamu kuhusu baba yake (aliyesimama wa mwisho kulia) kupitia picha ya zamani

Siid Ahmed Sharif alikuwa mmoja wa maafisa wa SomaliA waliopewa mualiko wa masomo na Muungano wa Sovieti wakati ambapo USSR ilikuwa ikipania kuimarisha ushawishi wake barani Afrika.

Yeye na mama yake Farhiya walipanga kuoana, lakini mwaka mmoja baada ya Farhiya kuzaliwa, Somalia iliingia vitani na jirazi yake, Ethiopia - na Kremlin ikaunga mkono Ethiopia.

Kutokana na hatua hiyo Somalia iliwafurusha washauri wa Sovieti nchini humo na wanafunzi wote wa Somalia katika muungano wa USSR, miongoni mwao baba yake Farhiya, waliagizwa kurudi nyumbani.

"Mimi na mama yangu wakati huo tulikuwa tumeenda kumtembelea bibi yangu magharibi mwa Siberia tuliposikia mara ya kwanza redioni tangazo kuhusu vita hivyo," anasema.

"Nakumbuka mama yangu baadae aliniambia kuwa mara moja alijuwa hatua hiyo inamaanisha nini kwa familia yetu, hasa ilimaanisha nini kwa baba yangu."

Sharif alikua na saa 24 kufunganya virago vyake. Hakua hata na muda wa kuwaaga wapendwa wake lakini aliacha ujumbe uliokuwa na anauani ya wazazi wake' mjini Mogadishu.

"Nilijua kuwa hakutuacha, na wala hakututoroka," anasema Farhiya. "Alituacha kutokana na sababu ambazo hazikuweza kuepukika."

Lakini sababu hizo pia ziliwafanya washindwe kuwasiliana.

Familia hiyo ilitengana kwa karibu miongo minne.

Chanzo cha picha, Farhiya

Maelezo ya picha,

Farhiya akiwa na mama yake alipokua mtoto

Licha ya hayo, maisha ya utotoni ya Farhiya yalikuwa ya furaha.

"Nilizungukwa na upendo wa mama yangu. Jamaa zake walinipenda sana na kunijali, nilijihisi kuwa mtu maalum," anasema.

"Nilijivunia urithi wangu, na nilijivunia kuonekana tofauti… wanafunzi wenzangu darasani, waalimu wangu shuleni na hata chuo kikuu waliniambia Nilikuwa maalum."

Farhiya alikuwa akijiuliza baba yake alikuwa wapi na muonekano wake ulika vipi.

"Niliingiwa nahamu ya kumtafuta baba yangu tangu nilipokuwa na miaka 12, Nilijiambia lazima nifanye kila juhudi kumpata," she says.

Kufikia wakati ambapo hali ya kisiasa ilibadilika - sera ya Mikhail Gorbachev ya glasnost (uwazi) ilikuwa inatekelezwa lakini Farhiya hakua na hofia kumuandikia baba yake barua.

Lakini barua alizotuma kupitia anuani iliyoachwa na baba yake zilikua zinarudishwa bila haijafunguliwa. Hakujua hata kama ziliwahi kufika Somalia.

Aliwasiliana na mashirika ya USSR ambayo tyalisaidia watoto kuwatafuta baba zao na kuwaunganisha hata Shirika la Msalaba Mwekundu, ambalo lilikua likitoa huduma kama hiyo. Lakini juhudi zake ziligongwa mwamba.

Chanzo cha picha, Farhiya

Maelezo ya picha,

Farhiya akiwana watoto wanafunzi wenzake (mstari wa mbele, wa pili upande wa kulia)

"Watoto wengine wa Urusi walifanikiwa kuwapata wazazi wao katika nchi za Afrika. Nchi hizo zilikua na uhusia wakidiplomasia na Urusi na Ubalozi wao nchini humo pamoja na wafanyakazi waliokua wakifanya kazi Urusi ambao walikuwa wakisafiri kuenda nchiza Afrika na kurudi. Lakini Somalia, mawasiliano yalikua magumu," anasema.

Mara kwa mara aliasitisha juhudi za kumtafuta baba yake lakini hakuacha kabisa wazo la kumpata.

"Ilikuwa kama jaribio la kufanya kitu na kufeli kisha unapioteza matumaini ya kumtafuta kwa miaka michache kisha unaanza tene juhudi hizo," aliendelea kusema.

Somalia ilipokubwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 1991, ilikuwa niliathirika sana

Vita hivyo viliendelea kwa karibu miongo miwili, lakini vilipokaribia kuisha, mitandao ya kijamii ilikuwa imeanza kutumika hali ambayo ilimpatia Farhiyamatumaini mapya.

Katika moja ya mitandao ya kijamii ya Urusi, Vkontakte, alikutana na mwanamke ambaye amekuwa akiwaunganisha watu na wazazi wao wanaoishi ng'ambo, likini hakupata msaada aliotarajia.

"Nilimuandikia ujumbe na kumfahamisha kuwa namtafuta baba yangu nchini Somalia lakini hakuweza kunisaidia," Farhiya anasema.

Baada ya hapo akaanza kutafuta picha ya Somalia katika mtandao wa Instagram.

Chanzo cha picha, Deeq M Afrika

Maelezo ya picha,

Picha ya Mogadishu liyochapishwa na Deeq M Afrika katika mtandao wa Instagram

Baadhi ya picha alizopenda katika mtandao huo zilikuwa zikiwekwa na kijana wa Kisomalia liyekua anajiita Deeq ambaye alionekana kuwa na ushawishi mkubwa, kwa hivyo alaimua kumuandikia ujumbe kuona kama atamsaidia.

Deeq alikuwa na mtandao mkubwa wa marafiki nchini Somalia kutokana na ziara zake Amerika Kaskazini, Ulaya na Upembe wa Afrika. Pia alikuwa anajuana na watu kadhaa katika serikali ya Somali kutokana na kazi yake katika ubalozi wa nchi hiyo mjini Dubai.

Machi 16 aliweka ujumbe wa Farhiya katika mtandao wake wa Facebook akiomba msaa kwa niaba yake.

Watu walianza kujibu na moja kati ya ujumbe uliomvutia ulitokea Norway .

"Huyo ni dada yetu Farhiya," ujumbe huo uliandikwa.

Uliandikwa na mmoja wa ndugu wa kambo wa Farhiya, wanaoishi Oslo, na baba yao wakati huo.

Chanzo cha picha, Farhiya

Maelezo ya picha,

Picha ya baba yake baba yake Farhiya iliyoambatanishwa na ujumbe

Wiki moja baada ya mawasiliano kadhaa ya simu kupitia mtandao wa Skype, Farhiya, mama yake na baba wakambo wa Farhiya walisafiri hadi Norway kukutana na baba yake mzazi.

"Anafanana na mimi," anasema. "Tunafanana hadi kwa mwendo. sauti zetu pia zinafanana. Sikuamini macho yangu - yaani hatimaye tumekutana baada y amiaka hiyo yote!"

Alikutana na watatu kati ya dada zake wa kambo, na kaka yake mmoja alipowasili kutoka Sweden, ambako baba yake huishi muda mwingi. Mjomba wake wa kambo pia alisafiri hadi mjini Oslo kujumuika na familia.

Farhiya alifahamu kuwa baba yake pia alikuwa akimtafuta .

"Tulipowasiliana mara ya kwanza kwenye Skype, aliniambia kuwa yeye pia amekuwa akitutafuta bila mafanikia," alisema.

Lakini yeye bna mama yake walikuwa wamehama baada ya mama kuolewa na Sharif hakuwa na anuwani yao mpya.