'Viwango vya juu zaidi vya joto duniani'Marekani vyagonga nyuzi joto 54.4

Picha ya bonde la Death Valley, California, iliyopigwa Julai 2020

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Viwango vya joto ambavyo huenda vilivunja rekodi vilishuhudiwa katika bonde la Death Valley, California

Kiwango cha joto ambacho huenda ni cha juu zaidi kuwahi kushuhudiwa duniani - nyuzi joto 54.4- huwenda vimeshuhudiwa may have katika bonde la Death Valley lilipo katika mbuga ya kitaifa ya wanyama, California.

Rekodi hiyo inachunguzwa na mamlaka ya kitaifa ya mambo ya hewa nchini Marekani.

Viwango hivyo vya juu vya joto vimefikiwa huku pwani ya magharibi ya Marekani ikikabiliwa na wimbi la joto, na viwango vya joto vinatarajiwa kupanda zaidi juma hili.

Hali hiyo imetokana joto kali lililoshuhudiwa katika kipindi cha siku mbili California, baada ya mtambo wa umeme kushindwa kufanya kazi siku ya Jumamosi

Rekodi zilizopita zilikuaje?

Rekodi ya juu zaidi ilifikiwa siku ya Jumapili katika bondo la Death Valley.

Kabla ya hapo, kiwango wa juu cha joto kurekodiwa duniani kilikuwa nyuzi juto 54 - pia katika bonde la Death Valley, 2013.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Kibao kinachowatahadharisha waendeshaji magari kuhusu joto kali

Karne moja iliyopita viwango vya joto vilivyofikia nyuzijoto 56.6, pia vilishuhudiwa katika bonde la Death Valley, licha rekodi hiyo kutiliwa sahaka. Wataalamu wa kisasa wa hali ya hewa wanaamini kulikuwa na dosari katika rekodi hiyo, kwani viwango vingine vya joto vilivyokuwa na utata pia vilirekodiwa msimu huo wa joto.

Kwa mujibu wa uchambuzi mwaka 2016 kutoka mwanahistoria wa Christopher Burt, viwango vya joto katika eneo hilo vilirekodiwa 1913 haviendeni na vile vya bonde la Death Valley.

Kiwango kingine cha juu cha joto ambacho kilifikia nyuzi joto 55 kilirekodiwa nchini Tunisia mwaka 1931, lakini Bw. Burt anasema kiwango hicho cha joto na vingine vilivyorekodiwa Africa katika enzi ya ukoloni vilikuwa na "tashuwishi".

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

"Ukungu mkubwa" ulionekana siku ya Jumamosi

Je tunafahamu nini kuhusu wimbi la joto?

Wimba la sasa la joto limefikia Arizona kusini -magharibi, kuelekea pwani hadi jimbo la Washington kaskazini -magharibi.

Wimbi hilo la joto linatarajiwa kufikia kilele chake Jumatatu na Jumanne , kabla ya viwango vya joto kuanza kushuka baadae wiki hii. Hata hivyo joto kali litaendelea kushuhudiwa kwa karibu siku 10.

Huku viwango vya joto vikiendelea kupanda California, ''ukungu'' mkubwa kama moshi ulionekana angani siku ya Jumamosi katika kaunti ya Lassen.

Nini athari ya joto kupita kiasi?

Maafisa wanasema kuwa joto la juu kupita kiasi katika kipindi cha siku mbili au tatu linapita chuzi joto 932.

Kituo cha Marekani cha kudhibiti na kuzuia magonjwa (CDC) kinasema kuwa wimbi la joto limewaua watu zaidi ikilinganishwa na kipindi kingine chochote kilichoshuhudia hali hiyo nchini.

Athari ya moja kwa moja ya wimbi la joto katika mwili wa binadamu ni ngozi kupasuka pasuka, ukosefu wa maji mwilini na hatari mtu kupatwa na kiharusi kinachotokana na joto jingi.

Kiwango cha joto kupita kiasi mwilini pia kinaweza kuwa kudhoofisha hali ya mtu ambaye anakabiliwa na changamoto zingine za afya, ikiwa ni pamoja na matatizo ya kupumua ,matatizo ya moyo na figo,Shirika la Afya Duniani (WHO) linasema.

Pia inaweza kuathiri miundo mbinu pia, Kama vile vifaa vya kusambaza umeme na kusababisha umeme kupotea, joto kupita kiasi pia inaweza kutatiza ndege kupaa, lami kwenye bara bara kuyeyuka, na kufanya magari kuwa moto kupita kiasi na kusababisha hatari kwa kwa waliomo ndani.

Wimbi la joto pia linaweza kuwa na athari katika shughuli za kilimo- kwa mfano kuzifanya mboga kunyauka na kufa ama kusababisha kusambaa kwa magonjwa ya mimea.